PEPEA AFRIKA
Friday, 13 April 2012
Winnie Madikizela-Mandela

Winnie Mandela alizaliwa Nomzamo Winfreda Madikizela tarehe 26 Septemba 1936, ni mwanasiasa kutoka Afrika ya Kusini na alishikilia nyadhifa mbalimbali serikalini na pia alikiongoza African National Congress ya Wanawake. Hivi sasa ni mwanachama wa ANC Kamati Kuu ya Taifa.Ingawa bado alikuwa ameoleka na Nelson Mandela wakati alikuwa rais wa Afrika Kusini mnamo Mei 1994,wanandoa hawa walikuwa wametengana miaka miwili baadaye. Talaka yao ilimaliza 19 Machi 1996, na makazi isiyojulikana nje ya mahakama. Jaribio la Winnie Mandela kupata makazi ya hadi dola milioni 5, nusu ya yale alidai ni thamani ya mume wake wa zamani, yalitupiliwa mbali na mahakama kwa kutoonekana mahakamani.
Ni
mwanaharakati matata, ni maarufu miongoni mwa wafuasi wake, ambao
humuita ''Mama wa Taifa'' hasa kutokana na ushiriki wake katika madai
ya ukiukaji haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na utekaji nyara wa
1988 ambapo mwanaharakati mmoja wa miaka 14 wa chama cha ANC Stompie
Moeketsi aliuawawa.Machi 2009 tume ya Uchaguzi ilitoa uamuzi kuwa Winnie Mandela ambaye alichaguliwa kama mgombea wa ANC, anaweza kuwania Uchaguzi mkuu wa Aprili 2009, licha ya kuwa na kesi kotini na udanganyifu.
Jina lake Nomzamo linalomaanisha ''ajaribuye kitu'', alikutana na wakili na pia mwanaharakati Nelson Mandela 1957, Walioona 1958 na wana wasichana wawili. Juni 2010 alitibiwa kwa mshutuko wa moyo baada ya kusikia mjuku wake amefariki kwa ajali ya barabara usiku wa kufungua Kombe la Dunia. Ana ugonjwa wa Kisukari.
Licha ya vikwazo vya elimu kwa watu weusi wakati wa ubaguzi wa rangi,alipata shahada katika kazi za kijamii kutoka Jan Hofmeyer huko Johannesburg.
Bi. Mandela alijitokeza kama mpinzani kiongozi kwa wazungu wachache waliokuwa utawalani wa serikali katika miaka ya kifungu cha mumewe toka Agosti 1963 – Februari 1990, katika miaka hii alikuwa akikimbilia uhamishoni Brandfort isipokuwa ile tu siku aliyokubaliwa kumtembelea mumewe katika gereza la Roben Island.
Sifa yake iliharibika wakati akitoa hotuba yake Aprili 13 1986 wakati alitetea na kukubali watu kuchomwa wakiwa hai wakitumia gurudumu za gari ili kumaliza ubaguzi wa rangi. Fauka ya hayo hathi yake iliendelea kuharibika pale mlinzi wake, Jerry Musivuzi Richardson alisema eti Winnie aliamurisha utekaji nyara na mauaji.Desemba 29 1988 Richardson ambaye alikuwa kocha wa klabu ya mpira ya Mandela United ambayo ndiyo ndiyo ilikuwa kama ulinzi wa kibinafsi wa Bi. Mandela alisema kwamba ndiye aliyemuuwa kijana wa miaka 14 James Seipei ama Stompie Moeketsi miongoni mwa vijana wengine watatu.
Vituko
Mwanamke mmoja ampiga mmewe kisa na maana alipokuwa akienda kitandani wakati wa kulala Mme wake hakuenda kitandani naye bali alibaki aki facebook.
Thursday, 12 April 2012
Joyce Banda
Ni
mwanasiasa kutoka malawi ambaye pia amekuwa rais nchini humo tangu
Aprili 7 2012.Msomi na mwanaharakati, alikuwa waziri wa nchi za
kigeni toka 2006 hadi 2009 na Makamu wa Rais wa nchi hiyo tangu Mai
2009 hado Aprili 1012. Alikuwa rais kutokana na kifo cha gafla cha
Bingu wa Mutharika. Ni mwanamke wa kwanza kuwa rais na makamu wa rais
nchni Malawi.Alikuwa pia mbunge na waziri wa jinsia, watoto na mambo ya Huduma za jamii. Kabla ya kushiriki katika siasa alikuwa mwanzilishi wa Joyce Banda Foundation, Mwanzilishi wa Chama cha Taifa cha Wafanyi biashara Wanawake (NABW), Viongozi Wanawake wachanga na mtandao wa mradi wa njaa. Alitajwa katika Forbes Magazine 2011 kama mwanamke wa tatu maarufu na mwenye nguvu zaidi katika Afrika.
Alikuwa
mwanzilishi na mwenyekiti wa chama cha People's Party kilichoundwa
2011, na kabla ya kifo cha rais Mutharika alikuwa awanie urais wa
nchi hiyo mwaka 2014. Banda anatoka Malemia, kijiji katika Wilaya ya
Zomba ya Malawi. Ana Certificate kutoka Chuo cha Cambridge School na
shahada ya sanaa katika Elimu ya Mafunzo kutoka Chuo Kikuu cha
Columbus na stashahada katika usimamizi yaani (Management) aliyopata
nchini Italia.
Katika umri wa miaka 25 alikuwa tayari kashapata watoto watatu na alikuwa anaishi Nairobi Kenya. Yeye ni dada kwa Anjimile Oponyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Academy ya wasichana iliyoanzishwa na mwimbaji Madonna.
Ameolewa na Richard Banda,aliyekuwa Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Malawi.
Ana zawadi zaidi ya 10 kutoka nchini malawi na kimataifa.
Vituko
Mtoto mwenye umri wa miaka 15 ameokolewa na mwa wa jirani wao, baada ya kukimbizwa na kahaba mwanamke aliyekuwa anamdai. Mtoto huyo alikuwa anatoka dukani alipokuwa ametumwa na mamaye mwendo wa saa kumi na mbili jioni, hapo ndipo mwanamke huyo alipomuona na kuanza kumkimbiza, ndipo mbwa wa jirani alipomuona na kuanza kumkimbiza mwanamke huyo.
Ukweli Barani
Libreville, Gabon ndio nchi ya 5 Duniani ya gharama ya juu ama kubwa kuishi. Tokyo ndio ya kwanza.
Wednesday, 11 April 2012
Steven Kanumba

Steven Charles Kanumba alikuwa msanii wa maigizo na filamu kutoka nchini Tanzania. Katika historia ya tasnia ya filamu nchini Tanzania, Kanumba ndiye aliyekuwa msanii wa kwanza nchini kufanya kazi nje ya nchi na kuweza kuwavuta wageni kutoka nchi mbalimbali kuja kuigiza Tanzania. Hasa walikuwa Wanigeria kama vile Mercy Johnson, Emmanuel France, Nkiru Silvanus, Ramsey Nouah, na wengine wengi tu. Kanumba pia ameweza kuwaleta waongozaji filamu kadhaa was Kinigeria nchini.
Steven alizaliwa huko Shinyanga Januari 8 1984, alianza masomo yake katika shule ya msingi ya Bugoyi, na kuendela na masomo ya sekondari huko Mwadui na baadae kupata uhamisho katika shule moja jijini Dar es Salaam iitwayo Dar Christian Seminary. Alivyomaliza kidato cha nne akaendelea na masomo ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari ya Jitegemee ilioko huko huko Dar es salaam.
Kanumba
alieanza shughuli za kuigiza miaka mingi kwenye miaka ya "90".
Ila kufahamika zaidi alianza mwaka 2002
mara
tu baada ya kujiunga na kundi la sanaa ya maigizo maarufu kamaKaole
Sanaa Group.
Kwa
sasa ameanza kutangaza sanaa nchi za Afrika
ya Magharibi
ikiwemo
Nigeria
na
pia Wanigeria wamependezewa na uigizaji wake hivyo kushirikiana
pamoja naye katika filamu kadha wa kadha. Filamu ambazo wameshawahi
kushirikiana pamoja ikiwemo na ile ya Dar
to Lagos,
She
is My Sister na
nyingine ambazo bado zinajengwa.
Steven
Kanumba alitangaza
hivi karibuni nia ya kuwa mgombea katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka
2015.
Aliaga dunia tarehe 7
Aprili,
2012)
na kuzikwa hapo jana ma mia ya waombolezaji wakiwemo watu mashuhuri
serikalini pamoja na Mama Salma Kikwetu walihudhuria na kumuaga.
Subscribe to:
Comments (Atom)

