Pages

Wednesday, 4 April 2012

MICHAEL KIJANA WAMALWA

Michael Christopher Wamalwa alizaliwa  eneo la Isiolo, wilayani Bungoma.
Alikuwa mkuu wa wanafunzi na mjadili bora katika shule yake ya sekondari ya Strathmore. Aliibuka kuwa mwanafunzi mwandishi bora nchini na akawakilisha Kenya katika ushindani wa uandishi wa insha huko Uingereza.
Mwaka 1965, alipewa tuzo la masomo ya jamii na kusoma sheria katika Chuo cha Cambridge na kufuzu mwaka 1968.
Alirejea Kenya mwaka 1970 na kuwa mwalimu wa kusomesha elimu ya sheria katika Chuo Kikuu cha Nairobi.
Mwaka wa 1974, alihusika katika kampeini za uchaguzi na kufaulu katika uchaguzi wa 1979. 
Alihusika tena katika kampeini za uchaguzi wa vyama na akachaguliwa kuwa mbunge wa wilaya ya Saboti pamoja na kuwa Makamu wa kwanza wa mwenyekiti wa chama chake.
Baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha Ford Kenya, Oginga Odinga, kuaga dunia, alifanywa kuwa mwenyekiti wa hicho chama mwaka wa 1994.
Wamalwa alihusika tena katika kampeini za uchaguzi wa 2002 na kufanikiwa kuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais, huku Mwai Kibaki akichaguliwa kuwa rais wa Kenya.
Katika mwaka wa 2002, baada ya rais wa Kenya, Mwai Kibaki, kuhusika katika ajali ya barabara na kupelekwa Ulaya ili apate matibabu bora, alimtembelea Mwai Kibaki hospitalini lakini kwa bahati mbaya akaugua figo.
Baada ya kupata nafuu kwa muda mfupi, alifunga pingu za maisha na Yvonne Nambia.
Miezi miwili baada ya harusi yake, akaugua tena na kupelekwa Ulaya katika hospitali ya Royal Free Hospital ambako aliaga dunia masaa ya asubuhi tarehe 23 mwezi Agosti mwaka wa 2003.

No comments:

Post a Comment