
Mohamed ''Mo'' Amin alikuwa mpiga picha maarufu zaidi kutoka Kenya alithihirisha haya kwa picha na kanda zake za video alizopiga kuhusu njaa ya Ethiopia.Alizaliwa Agosti 29 1943, kwenye mtaa wa Eastleigh Nairobi na ari yake ya picha ilianza akiwa shuleni. Ndiye mwanzilishi wa kampuni ya Camerapix mwaka 1963 huko Dar es Salaam na kuihamisha kampuni hiyo hadi Nairobi.Katika miak ya 1970 akawa wapiga wa kutegemewa zaidi kuhusu habari za Afrika,akiripoti kuhusu vita na mapinduzi barani afrika na picha zake zilitumika pia na runinga na wanahabari wa magharibi
Ushawishi wake mkubwa ulikuja wakati picha zake pamoja Micheal Buerk mpiga picha mwenza ziliripotia Njaa ya Ethiopia zilipoleta hisia kimataifa na hatimaye kusaidiya na kusababisha matamasha ya Live Aid iliofanya wimbo ''We are the World'' wake wasanii wote ulimwenguni kutungwa.

Novemba 23 1996 aliabiri ndege aina ya Ethiopian Airlines Flight 961 na Brian Tetley mwenye umri wa miaka 61 kurudi Nairobi baada ya kazi ya kibiashara nchini Ethiopia ndege hiyo ilitekwa nyara na kumlazimisha rubani kuilekeza ndege hiyo mashariki mwa bara indi, alijaribu kupigana nao watekanyara hao lakini ndege hiyo ikaaisha mafuta kuanguka kwenye ufuo wa visiwa vya Comoros. Amin aliaga papo hapo akiwa na umri wa miaka 53 rafikiye pia aliaga.
No comments:
Post a Comment