Pages

Tuesday, 3 April 2012


Joseph Kabila

Joseph Kabila Kabange alizaliwa kama Hippolyte Kanambe Kazemberembe Kabange Mtwale Juni 4 1971 ni rais wa nne wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Aliingia katika uraisi baada ya kifo cha babake Rais Laurent-Desiree Kabila aliyeuawa na wanajeshi tar. 16 Januari 2001. Wanasiasa wengine walimteua mwana kuwa raisi baada ya baba.



Katika uchaguzi wa kitaifa wa 30 Julai 2006 alipata kura nyingi kuwa raisi lakini hakufikia nusu ya kura zote. Katika uchaguzi wa pili kati yake na Jean-Pierre Bemba alishinda akathebitishwa kuwa rais tar. 17 Novemba 2006. Joseph Kabila ni rais wa kwanza wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo aliyechaguliwa na wananchi wote katika uchaguzi huru.

Joseph Kabila alizaliwa mjini Hewa Bora mkoani wa Kivu Kusini katika mashariki ya Kongo. Babake alikuwa mwanasiasa na kiongozi wa kikundi cha wanamgambo waasi waliopinga serikali ya Mobutu Sese Seko.
Joseph alihamia Dar es Salaam (Tanzania. Alisoma shule ya msingi na ya sekondari katika Dar es salaam na Mbeya na pia alisomea Chuo Kikuu cha Makerere na alisomea Uanajeshi. Octoba 1996 alikuwa Commanda wa kundi la "Kadogos" ambalo ni jeshi la watoto Inasemekana alitumia wakati ule jina la Hippolyte Kanambe Kazemberembe Kabange Mtwale kwa sababu za usalama.


Baada ya ushindi wa wapinzani dhidi ya Mobutu babake alikuwa rais na Joseph alipelekwa masomoni kwenye chuo cha kijeshi huko Uchina. Wakati wa kurudi alipewa cheo cha jenerali jeshini na mwaka 2000 alipandishwa cheo kuwa mkuu wa jeshi.
Alikuwa rais Januari 26 2001 baada ya kifo cha babake Laurent-Desiree Kabila, na kumfanya kuwa rais wa kwanza duniani aliyezaliwa katika miaka ya 1970s. Alikuwa rais mchanga Ulimwenguni hadi januari 2004.
Desemba 2002 alikubali mapatano ya amani kati ya serikali na waasi yaliyokuwa msingi kwa ajili ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa na maandalizi ya uchaguzi wa mwaka 2006.
juni 11 2004 mapinduzi ya kijeshi wakiongozwa naye Meja Eric Lenge walijaribu kuchukuwa madaraka na kutangaza kwa radio ya taifa kwamba shughuli zote za serikali zimesitishwa lakini walichindwa na askari wa Kabila.
Desemba 2005 kura ya maoni ya kupitisha katiba mpya ilifanyika na uchaguzi wa rais ulifanyika Julai 30 2006 baada ya kusitishwa kwa tarehe ya hapo awali. Kabila alishinda kwa asilimia 45% naye mpinzani wake na makamu wa rais na mwaasi wa zamani Jean-Pierre Bemba alipata asilimia 20%, Matokeo hayo yalikataliwa na kura zilirudiwa kati ya Kabila na Bemba Oktoba 29.Novemba 15,tume ya uchaguzi ilitangaza matokeo rasmi na Kabila kutangazwa kuwa mshindi na asilimia 58.05% za kura. Matokeo hayo yalithibitishwa na Mahakama Kuu Novemba 27 2006 na kabila kuapishwa Desemba 6 2006 kama rais.
Desemba 2011 Kabila alichaguliwa kwa kipindi cha pili kama rais. Baada ya matokeo kutangazwa tarehe 9 Desemba, kulikuwa na vurugu katika machafuko huko Kinshasa na Mbuji-Mayi ambapo ndiyo iliyo kuwa ngome kuu ya mpinzani wa Kabila Etienne Tshisekedi
Juni Mosi baada ya uvumi mbalimbali kutolewa na maafisa wa nyadhifa za juu serikalini kuhusu ndoa yake,mkuu wa Kaya ya rais, Balozi Theodore Mugalu alitangaza rasmi harusi ya rais na Olive Lembe di Sita.Harusi hiyo ilitendeka Juni 17 2006 wana msichana aliyepewa jina Sifa, jina la mamake Kabila







No comments:

Post a Comment