Joyce Banda
Ni
mwanasiasa kutoka malawi ambaye pia amekuwa rais nchini humo tangu
Aprili 7 2012.Msomi na mwanaharakati, alikuwa waziri wa nchi za
kigeni toka 2006 hadi 2009 na Makamu wa Rais wa nchi hiyo tangu Mai
2009 hado Aprili 1012. Alikuwa rais kutokana na kifo cha gafla cha
Bingu wa Mutharika. Ni mwanamke wa kwanza kuwa rais na makamu wa rais
nchni Malawi.
Alikuwa
pia mbunge na waziri wa jinsia, watoto na mambo ya Huduma za jamii.
Kabla ya kushiriki katika siasa alikuwa mwanzilishi wa Joyce Banda
Foundation, Mwanzilishi wa Chama cha Taifa cha Wafanyi biashara
Wanawake (NABW), Viongozi Wanawake wachanga na mtandao wa mradi wa
njaa. Alitajwa katika Forbes Magazine 2011 kama mwanamke wa tatu
maarufu na mwenye nguvu zaidi katika Afrika.
Alikuwa
mwanzilishi na mwenyekiti wa chama cha People's Party kilichoundwa
2011, na kabla ya kifo cha rais Mutharika alikuwa awanie urais wa
nchi hiyo mwaka 2014. Banda anatoka Malemia, kijiji katika Wilaya ya
Zomba ya Malawi. Ana Certificate kutoka Chuo cha Cambridge School na
shahada ya sanaa katika Elimu ya Mafunzo kutoka Chuo Kikuu cha
Columbus na stashahada katika usimamizi yaani (Management) aliyopata
nchini Italia.
Katika
umri wa miaka 25 alikuwa tayari kashapata watoto watatu na alikuwa
anaishi Nairobi Kenya. Yeye ni dada kwa Anjimile Oponyo, Mkurugenzi
Mtendaji wa Academy ya wasichana iliyoanzishwa na mwimbaji Madonna.
Ameolewa
na Richard Banda,aliyekuwa Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Malawi.
Ana
zawadi zaidi ya 10 kutoka nchini malawi na kimataifa.
No comments:
Post a Comment