Pages

Monday, 2 April 2012

                              KWAME NKRUMAH
Kwame Nkrumah alizaliwa mwaka 1909 katika eneo la Nkroful nchini Gold Coast.
Alimaliza masomo yake ya msingi katiika shule ya Achimota iliyoko Accra mwaka 1930, kisha akasomea katika shule ya katoliki ya Roman Catholic Seminary, ambako baadaye alianza kufunza shule moja ya kikatoliki iliyoko Axim.
Katika mwaka 1935, alienda kuendeleza masomo yake katika Chuo Kikuu cha Pennsylvania na kuhitimu masomo yake mwaka 1942.
Kwame alirudi Ghana na kufanywa kuwa katibu mkuu wa chama cha 'United Cold Coast Convention'. Mzozo uliibuka mwaka 1948 tarehe 28 mwezi Februari nchini Chana ambao ulimsababisha kutiwa mbaroni kwani, ilishukiwa kuwa chana cha UGCC ndicho  kilichoanzisha mzozo huo.
Baada ya kuwekwa huru, alifanywa kuwa kiongozi wa Chama cha Vijana mwaka 1948.
Katiba ilirekebishwa  katika mwaka 1952 mwezi Marchi tarehe 10 na Nkrumah akafanywa kuwa waziri mkuu wa kwanza nchini Ghana.
Katika mwaka 1966 mwezi Februari, akiwa bado akizuru nchini Vietnam na China, serikali ya Ghana ikapinduliwa katika mapinduzi ya kijeshi yaliyoanzishwa na Emmanuel Kwasi Kotaka na Baraza la National Liberation Council.
Nkrumah hakurudi Ghana na kuishi uhamishoni nchini Guinea, kama mgeni wa rais wa Guinea, Ahmed Sekou Toure.
Katika mwaka 1972 mwezi Aprili, Nkruma aliugua saratani ya ngozi na kuaga dunia akiwa na umri wa miaka 62.

No comments:

Post a Comment