
Winnie Mandela alizaliwa Nomzamo Winfreda Madikizela tarehe 26 Septemba 1936, ni mwanasiasa kutoka Afrika ya Kusini na alishikilia nyadhifa mbalimbali serikalini na pia alikiongoza African National Congress ya Wanawake. Hivi sasa ni mwanachama wa ANC Kamati Kuu ya Taifa.Ingawa bado alikuwa ameoleka na Nelson Mandela wakati alikuwa rais wa Afrika Kusini mnamo Mei 1994,wanandoa hawa walikuwa wametengana miaka miwili baadaye. Talaka yao ilimaliza 19 Machi 1996, na makazi isiyojulikana nje ya mahakama. Jaribio la Winnie Mandela kupata makazi ya hadi dola milioni 5, nusu ya yale alidai ni thamani ya mume wake wa zamani, yalitupiliwa mbali na mahakama kwa kutoonekana mahakamani.

Machi 2009 tume ya Uchaguzi ilitoa uamuzi kuwa Winnie Mandela ambaye alichaguliwa kama mgombea wa ANC, anaweza kuwania Uchaguzi mkuu wa Aprili 2009, licha ya kuwa na kesi kotini na udanganyifu.
Jina lake Nomzamo linalomaanisha ''ajaribuye kitu'', alikutana na wakili na pia mwanaharakati Nelson Mandela 1957, Walioona 1958 na wana wasichana wawili. Juni 2010 alitibiwa kwa mshutuko wa moyo baada ya kusikia mjuku wake amefariki kwa ajali ya barabara usiku wa kufungua Kombe la Dunia. Ana ugonjwa wa Kisukari.
Licha ya vikwazo vya elimu kwa watu weusi wakati wa ubaguzi wa rangi,alipata shahada katika kazi za kijamii kutoka Jan Hofmeyer huko Johannesburg.
Bi. Mandela alijitokeza kama mpinzani kiongozi kwa wazungu wachache waliokuwa utawalani wa serikali katika miaka ya kifungu cha mumewe toka Agosti 1963 – Februari 1990, katika miaka hii alikuwa akikimbilia uhamishoni Brandfort isipokuwa ile tu siku aliyokubaliwa kumtembelea mumewe katika gereza la Roben Island.
Sifa yake iliharibika wakati akitoa hotuba yake Aprili 13 1986 wakati alitetea na kukubali watu kuchomwa wakiwa hai wakitumia gurudumu za gari ili kumaliza ubaguzi wa rangi. Fauka ya hayo hathi yake iliendelea kuharibika pale mlinzi wake, Jerry Musivuzi Richardson alisema eti Winnie aliamurisha utekaji nyara na mauaji.Desemba 29 1988 Richardson ambaye alikuwa kocha wa klabu ya mpira ya Mandela United ambayo ndiyo ndiyo ilikuwa kama ulinzi wa kibinafsi wa Bi. Mandela alisema kwamba ndiye aliyemuuwa kijana wa miaka 14 James Seipei ama Stompie Moeketsi miongoni mwa vijana wengine watatu.
No comments:
Post a Comment