Pages

Thursday, 5 April 2012

Jakaya Kikwete


Jakaya Mrisho Kikwete alizaliwa Octoba 7 1950 ni mtoto wa sita kwa familia ya watoto 9, ni rais wa 4 na wa sasa wa jamhuri ya Tanzania.Alizaliwa huko Msoga, Bagamoyo Tanganyika ambayo sasa ni Tanzania. Alikuwa pia mwenyekiti wa Umoja wa Afrika toka Januari 31 2008 hadi Februari 2 2009.
Alifuzu na digri ya Uchumi mwaka wa 1975 na kuamua kufanya kazi ya mapato duni kwa chama kilichokuwa kikitawala cha TANU ambapo kikawa ccm, hii ilimpa nafasi kufanya kazi katika maeneo ya vijiji na wilayani.
Kisha slijiunga na Jeshi na kuanza mazoezi katika kambi ya taifa ya Ruvu mwaka 1972. Baada ya kumaliza mazoezi na masomo yake ya kijeshi alikuwa Luteni 1976. Katika kazi yake ya jeshi alipanda ngazi hadi Lieutenat – Colonel. Kuanzia mwaka 1984 hadi 1986, Kikwete alikuwa Mkuu wa Siasa Mwalimu na Commissar wa Siasa katika Chuo cha Kijeshi.
Aliondoka jeshi kama kanali Luteni-wakati vyama vingi vilianza kuingia Tanzania mwaka 1992 na kuamua kuwa mwanasiasa kamili.
Katika siasa za vyama , Kikwete alianza kungaa mwaka 1982 ,wakati alichaguliwa kwa kura nyingi kwa chama cha CCM kuwa mjumbe wa kamati kuu ya taifa sera ya juu na kuwa muamuzi wa chama hicho. Tangu achaguliwe amekuwa akichaguliwa kila baada ya miaka mitano.
Rais Ally Hassan Mwinyi alimteua kuwa mbunge na wakati huo huo, naibu wa Nishati na Madini Novemba 7 1988. Mwaka 1990alipandishwa cheo na kuwa Waziri kamili wa Nishati, Maji na Madini. Baadaye mwaka huo huo, alifanikiwa kugombea kiti cha ubunge katika jimbo la Bagamoyo anapotoka.
1994 akiwa miaka 44 alikuwa waziri wa Fedha nyanga kuwahi kuhudumu katika historia ya Tanzania. Kwenye hazina ya Tanzania aliasisi nidhamu katika usimamizi wa fedha za umma na uwajibikaji hadi leo,yeye hukumbukwa kwa kuanzisha mfumo wa bajeti ya fedha na kufufua miundo ya ukusanyaji wa mapato, mbinu ya taasisi, ikiwa ni pamoja na maandalizi kwa ajili ya malezi.
Desemba 1995, alikuwa Waziri wa Mambo ya Kigeni na ushirikiano wa Kimataifa,akiteuliwa na Rais Benjamin William Mkapa wa serikali awamu ya tatu. Alishikilia wizara hii kwa miaka kumi hadi pale alipote chaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Desemba 2005 hivyo kuwa waziri kuwahi kuhudumu katika wizara hiyo kwa muda mrefu katika historia ya Tanzania. Tanzania ilijishugulika kuleta amani katika kanda ya Maziwa Makuu,hususan katika Burundi na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. Kikwete pia alikuwa mmoja wa wa wale walioshiriki katika mchakato wa kujenga upya ushirikiano wa kikanda katika Afrika Mashariki.
Utawala wake kama Rais umeshutumiwa kwa kiasi kikubwa cha hongo na kutoshughulikia maswala yanayo wakumba raia wa nchi hiyo.
Ametuhumiwa pia kwa kuchaguwa marafiki wake wa karibu kuwa mawaziri jambo ambalo linamfanya kutowarekebisha wanapoenda kinyume na maadili mema.
Alipokuwa mwenyekiti wa AU changamoto yake kubwa ilikuwa jinsi alivyo shughulikia ghasia zilizo ikumba nchi yetu mwaka 2008.


Amemuowa Mama Salma Kikwete na wana watoto 8.

No comments:

Post a Comment