
Steven Charles Kanumba alikuwa msanii wa maigizo na filamu kutoka nchini Tanzania. Katika historia ya tasnia ya filamu nchini Tanzania, Kanumba ndiye aliyekuwa msanii wa kwanza nchini kufanya kazi nje ya nchi na kuweza kuwavuta wageni kutoka nchi mbalimbali kuja kuigiza Tanzania. Hasa walikuwa Wanigeria kama vile Mercy Johnson, Emmanuel France, Nkiru Silvanus, Ramsey Nouah, na wengine wengi tu. Kanumba pia ameweza kuwaleta waongozaji filamu kadhaa was Kinigeria nchini.
Steven alizaliwa huko Shinyanga Januari 8 1984, alianza masomo yake katika shule ya msingi ya Bugoyi, na kuendela na masomo ya sekondari huko Mwadui na baadae kupata uhamisho katika shule moja jijini Dar es Salaam iitwayo Dar Christian Seminary. Alivyomaliza kidato cha nne akaendelea na masomo ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari ya Jitegemee ilioko huko huko Dar es salaam.
Kanumba
alieanza shughuli za kuigiza miaka mingi kwenye miaka ya "90".
Ila kufahamika zaidi alianza mwaka 2002
mara
tu baada ya kujiunga na kundi la sanaa ya maigizo maarufu kamaKaole
Sanaa Group.

Steven
Kanumba alitangaza
hivi karibuni nia ya kuwa mgombea katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka
2015.
Aliaga dunia tarehe 7
Aprili,
2012)
na kuzikwa hapo jana ma mia ya waombolezaji wakiwemo watu mashuhuri
serikalini pamoja na Mama Salma Kikwetu walihudhuria na kumuaga.
No comments:
Post a Comment