Friday, 13 April 2012
Winnie Madikizela-Mandela

Winnie Mandela alizaliwa Nomzamo Winfreda Madikizela tarehe 26 Septemba 1936, ni mwanasiasa kutoka Afrika ya Kusini na alishikilia nyadhifa mbalimbali serikalini na pia alikiongoza African National Congress ya Wanawake. Hivi sasa ni mwanachama wa ANC Kamati Kuu ya Taifa.Ingawa bado alikuwa ameoleka na Nelson Mandela wakati alikuwa rais wa Afrika Kusini mnamo Mei 1994,wanandoa hawa walikuwa wametengana miaka miwili baadaye. Talaka yao ilimaliza 19 Machi 1996, na makazi isiyojulikana nje ya mahakama. Jaribio la Winnie Mandela kupata makazi ya hadi dola milioni 5, nusu ya yale alidai ni thamani ya mume wake wa zamani, yalitupiliwa mbali na mahakama kwa kutoonekana mahakamani.

Machi 2009 tume ya Uchaguzi ilitoa uamuzi kuwa Winnie Mandela ambaye alichaguliwa kama mgombea wa ANC, anaweza kuwania Uchaguzi mkuu wa Aprili 2009, licha ya kuwa na kesi kotini na udanganyifu.
Jina lake Nomzamo linalomaanisha ''ajaribuye kitu'', alikutana na wakili na pia mwanaharakati Nelson Mandela 1957, Walioona 1958 na wana wasichana wawili. Juni 2010 alitibiwa kwa mshutuko wa moyo baada ya kusikia mjuku wake amefariki kwa ajali ya barabara usiku wa kufungua Kombe la Dunia. Ana ugonjwa wa Kisukari.
Licha ya vikwazo vya elimu kwa watu weusi wakati wa ubaguzi wa rangi,alipata shahada katika kazi za kijamii kutoka Jan Hofmeyer huko Johannesburg.
Bi. Mandela alijitokeza kama mpinzani kiongozi kwa wazungu wachache waliokuwa utawalani wa serikali katika miaka ya kifungu cha mumewe toka Agosti 1963 – Februari 1990, katika miaka hii alikuwa akikimbilia uhamishoni Brandfort isipokuwa ile tu siku aliyokubaliwa kumtembelea mumewe katika gereza la Roben Island.
Sifa yake iliharibika wakati akitoa hotuba yake Aprili 13 1986 wakati alitetea na kukubali watu kuchomwa wakiwa hai wakitumia gurudumu za gari ili kumaliza ubaguzi wa rangi. Fauka ya hayo hathi yake iliendelea kuharibika pale mlinzi wake, Jerry Musivuzi Richardson alisema eti Winnie aliamurisha utekaji nyara na mauaji.Desemba 29 1988 Richardson ambaye alikuwa kocha wa klabu ya mpira ya Mandela United ambayo ndiyo ndiyo ilikuwa kama ulinzi wa kibinafsi wa Bi. Mandela alisema kwamba ndiye aliyemuuwa kijana wa miaka 14 James Seipei ama Stompie Moeketsi miongoni mwa vijana wengine watatu.
Vituko
Mwanamke mmoja ampiga mmewe kisa na maana alipokuwa akienda kitandani wakati wa kulala Mme wake hakuenda kitandani naye bali alibaki aki facebook.
Thursday, 12 April 2012
Joyce Banda

Alikuwa pia mbunge na waziri wa jinsia, watoto na mambo ya Huduma za jamii. Kabla ya kushiriki katika siasa alikuwa mwanzilishi wa Joyce Banda Foundation, Mwanzilishi wa Chama cha Taifa cha Wafanyi biashara Wanawake (NABW), Viongozi Wanawake wachanga na mtandao wa mradi wa njaa. Alitajwa katika Forbes Magazine 2011 kama mwanamke wa tatu maarufu na mwenye nguvu zaidi katika Afrika.

Katika umri wa miaka 25 alikuwa tayari kashapata watoto watatu na alikuwa anaishi Nairobi Kenya. Yeye ni dada kwa Anjimile Oponyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Academy ya wasichana iliyoanzishwa na mwimbaji Madonna.
Ameolewa na Richard Banda,aliyekuwa Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Malawi.
Ana zawadi zaidi ya 10 kutoka nchini malawi na kimataifa.
Vituko
Mtoto mwenye umri wa miaka 15 ameokolewa na mwa wa jirani wao, baada ya kukimbizwa na kahaba mwanamke aliyekuwa anamdai. Mtoto huyo alikuwa anatoka dukani alipokuwa ametumwa na mamaye mwendo wa saa kumi na mbili jioni, hapo ndipo mwanamke huyo alipomuona na kuanza kumkimbiza, ndipo mbwa wa jirani alipomuona na kuanza kumkimbiza mwanamke huyo.
Ukweli Barani
Libreville, Gabon ndio nchi ya 5 Duniani ya gharama ya juu ama kubwa kuishi. Tokyo ndio ya kwanza.
Wednesday, 11 April 2012
Steven Kanumba

Steven Charles Kanumba alikuwa msanii wa maigizo na filamu kutoka nchini Tanzania. Katika historia ya tasnia ya filamu nchini Tanzania, Kanumba ndiye aliyekuwa msanii wa kwanza nchini kufanya kazi nje ya nchi na kuweza kuwavuta wageni kutoka nchi mbalimbali kuja kuigiza Tanzania. Hasa walikuwa Wanigeria kama vile Mercy Johnson, Emmanuel France, Nkiru Silvanus, Ramsey Nouah, na wengine wengi tu. Kanumba pia ameweza kuwaleta waongozaji filamu kadhaa was Kinigeria nchini.
Steven alizaliwa huko Shinyanga Januari 8 1984, alianza masomo yake katika shule ya msingi ya Bugoyi, na kuendela na masomo ya sekondari huko Mwadui na baadae kupata uhamisho katika shule moja jijini Dar es Salaam iitwayo Dar Christian Seminary. Alivyomaliza kidato cha nne akaendelea na masomo ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari ya Jitegemee ilioko huko huko Dar es salaam.
Kanumba
alieanza shughuli za kuigiza miaka mingi kwenye miaka ya "90".
Ila kufahamika zaidi alianza mwaka 2002
mara
tu baada ya kujiunga na kundi la sanaa ya maigizo maarufu kamaKaole
Sanaa Group.

Steven
Kanumba alitangaza
hivi karibuni nia ya kuwa mgombea katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka
2015.
Aliaga dunia tarehe 7
Aprili,
2012)
na kuzikwa hapo jana ma mia ya waombolezaji wakiwemo watu mashuhuri
serikalini pamoja na Mama Salma Kikwetu walihudhuria na kumuaga.
VITUKO
Mwanamke
mmoja afungwa miaka 10 gerezani kwa kumpa mtoto wake pombe aina ya
vodka. Mtoto huyo mwenye umri wa miaka 5 alipatikana hajielewi na
babake.Alipomuuliza mamake pia alikuwa amelewa chakari.
UKWELI BARANI AFRIKA
Chura
wakubwa zaidi duniani wanapatikana nchini Cameroon na ni zaidi ya
futi moja.
Tuesday, 10 April 2012
Mohamed Amin

Mohamed ''Mo'' Amin alikuwa mpiga picha maarufu zaidi kutoka Kenya alithihirisha haya kwa picha na kanda zake za video alizopiga kuhusu njaa ya Ethiopia.Alizaliwa Agosti 29 1943, kwenye mtaa wa Eastleigh Nairobi na ari yake ya picha ilianza akiwa shuleni. Ndiye mwanzilishi wa kampuni ya Camerapix mwaka 1963 huko Dar es Salaam na kuihamisha kampuni hiyo hadi Nairobi.Katika miak ya 1970 akawa wapiga wa kutegemewa zaidi kuhusu habari za Afrika,akiripoti kuhusu vita na mapinduzi barani afrika na picha zake zilitumika pia na runinga na wanahabari wa magharibi
Ushawishi wake mkubwa ulikuja wakati picha zake pamoja Micheal Buerk mpiga picha mwenza ziliripotia Njaa ya Ethiopia zilipoleta hisia kimataifa na hatimaye kusaidiya na kusababisha matamasha ya Live Aid iliofanya wimbo ''We are the World'' wake wasanii wote ulimwenguni kutungwa.

Novemba 23 1996 aliabiri ndege aina ya Ethiopian Airlines Flight 961 na Brian Tetley mwenye umri wa miaka 61 kurudi Nairobi baada ya kazi ya kibiashara nchini Ethiopia ndege hiyo ilitekwa nyara na kumlazimisha rubani kuilekeza ndege hiyo mashariki mwa bara indi, alijaribu kupigana nao watekanyara hao lakini ndege hiyo ikaaisha mafuta kuanguka kwenye ufuo wa visiwa vya Comoros. Amin aliaga papo hapo akiwa na umri wa miaka 53 rafikiye pia aliaga.
VITUKO
Nusura
harusi ikatizwe wakati Bi Harusi alipokiri kwamba alikuwa na mpango
wa kando. Kulingana na walioshuhudia, mwanadada huyu alieleza kwamba
atampenda mumewe hata ingawa anao mpango wa kando...!
FACTS
Maeneo
kame kabisa duniani yanapatikana Afrika, nayo ni Al'Kufrah huko
Libya, Aswan na Luxor nchini Misri, Wadi Halfa nchini Sudan, Mwari
Point nchini Namibia na Aoelef nchini Algeria.
Thursday, 5 April 2012
Jakaya Kikwete
Jakaya Mrisho Kikwete alizaliwa Octoba 7 1950 ni mtoto wa sita kwa familia ya watoto 9, ni rais wa 4 na wa sasa wa jamhuri ya Tanzania.Alizaliwa huko Msoga, Bagamoyo Tanganyika ambayo sasa ni Tanzania. Alikuwa pia mwenyekiti wa Umoja wa Afrika toka Januari 31 2008 hadi Februari 2 2009.
Alifuzu na digri ya Uchumi mwaka wa 1975 na kuamua kufanya kazi ya mapato duni kwa chama kilichokuwa kikitawala cha TANU ambapo kikawa ccm, hii ilimpa nafasi kufanya kazi katika maeneo ya vijiji na wilayani.
Kisha slijiunga na Jeshi na kuanza mazoezi katika kambi ya taifa ya Ruvu mwaka 1972. Baada ya kumaliza mazoezi na masomo yake ya kijeshi alikuwa Luteni 1976. Katika kazi yake ya jeshi alipanda ngazi hadi Lieutenat – Colonel. Kuanzia mwaka 1984 hadi 1986, Kikwete alikuwa Mkuu wa Siasa Mwalimu na Commissar wa Siasa katika Chuo cha Kijeshi.
Aliondoka jeshi kama kanali Luteni-wakati vyama vingi vilianza kuingia Tanzania mwaka 1992 na kuamua kuwa mwanasiasa kamili.
Katika siasa za vyama , Kikwete alianza kungaa mwaka 1982 ,wakati alichaguliwa kwa kura nyingi kwa chama cha CCM kuwa mjumbe wa kamati kuu ya taifa sera ya juu na kuwa muamuzi wa chama hicho. Tangu achaguliwe amekuwa akichaguliwa kila baada ya miaka mitano.
Rais Ally Hassan Mwinyi alimteua kuwa mbunge na wakati huo huo, naibu wa Nishati na Madini Novemba 7 1988. Mwaka 1990alipandishwa cheo na kuwa Waziri kamili wa Nishati, Maji na Madini. Baadaye mwaka huo huo, alifanikiwa kugombea kiti cha ubunge katika jimbo la Bagamoyo anapotoka.
1994 akiwa miaka 44 alikuwa waziri wa Fedha nyanga kuwahi kuhudumu katika historia ya Tanzania. Kwenye hazina ya Tanzania aliasisi nidhamu katika usimamizi wa fedha za umma na uwajibikaji hadi leo,yeye hukumbukwa kwa kuanzisha mfumo wa bajeti ya fedha na kufufua miundo ya ukusanyaji wa mapato, mbinu ya taasisi, ikiwa ni pamoja na maandalizi kwa ajili ya malezi.

Utawala wake kama Rais umeshutumiwa kwa kiasi kikubwa cha hongo na kutoshughulikia maswala yanayo wakumba raia wa nchi hiyo.
Ametuhumiwa pia kwa kuchaguwa marafiki wake wa karibu kuwa mawaziri jambo ambalo linamfanya kutowarekebisha wanapoenda kinyume na maadili mema.
Alipokuwa mwenyekiti wa AU changamoto yake kubwa ilikuwa jinsi alivyo shughulikia ghasia zilizo ikumba nchi yetu mwaka 2008.
Amemuowa Mama Salma Kikwete na wana watoto 8.
Vituko
Mama
mwenye umri wa miaka 32 amekichoma chumba cha kulala cha bintiye
mwenye umri wa miaka 16, akidai kwamba basi la kumpeleka skuli
lilikuwa linamwacha. Kulingana na msichana huyo, mamake alibisha
mlango kabla ya kutengeneza shimo kwenye mlango na kisha kuwasha moto
kwa karatasi na kuingiza kwenye shimo hilo. Moto huo ulichoma kiti
chumbani humo.Mama huyo naye aliwaambia askari kwamba mtoto alikuwa
anawachwa na basi sasa alifanya hivyo ili msichana wake atoke
chumbani humo.
Ukweli Barani
Je
wajua, Watu kumi na nane kutoka Afrika wametuzwa na tuzo ya Nobel.
Nao wanatoka Algeria, Misri, Ghana, Kenya, Nigeria na Afrika Kusini.
Wednesday, 4 April 2012
Ukweli Barani
Mogadishu, Somalia ni mji wa 4 hatari zaidi dunia. Johannesburg, Afrika Kusini ni ya 10 hatari zaidi kuishi duniani.
Vituko
Ajuza
mmoja wa miaka 70 amemshangaza mtoto wake wa kiume na majirani wake
kwa kutongoza kichuna wa kijana wake, na kuvalia mavazi ya kisasa ya
kijana na kuongea kwa lugha ya Sheng akisema ''Yo Yo mresh si uko juu
manze utamanga nini kuku chipo ama''
Mzee huyo aliyekuwa amevalia Jeans na kusag na tishati kubwa alifaulu kumwingiza kidosho huyo kwenye box
MICHAEL KIJANA WAMALWA
Alikuwa mkuu wa wanafunzi na mjadili bora katika shule yake ya sekondari ya Strathmore. Aliibuka kuwa mwanafunzi mwandishi bora nchini na akawakilisha Kenya katika ushindani wa uandishi wa insha huko Uingereza.
Mwaka 1965, alipewa tuzo la masomo ya jamii na kusoma sheria katika Chuo cha Cambridge na kufuzu mwaka 1968.
Alirejea Kenya mwaka 1970 na kuwa mwalimu wa kusomesha elimu ya sheria katika Chuo Kikuu cha Nairobi.
Mwaka wa 1974, alihusika katika kampeini za uchaguzi na kufaulu katika uchaguzi wa 1979.
Alihusika tena katika kampeini za uchaguzi wa vyama na akachaguliwa kuwa mbunge wa wilaya ya Saboti pamoja na kuwa Makamu wa kwanza wa mwenyekiti wa chama chake.
Baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha Ford Kenya, Oginga Odinga, kuaga dunia, alifanywa kuwa mwenyekiti wa hicho chama mwaka wa 1994.
Wamalwa alihusika tena katika kampeini za uchaguzi wa 2002 na kufanikiwa kuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais, huku Mwai Kibaki akichaguliwa kuwa rais wa Kenya.
Katika mwaka wa 2002, baada ya rais wa Kenya, Mwai Kibaki, kuhusika katika ajali ya barabara na kupelekwa Ulaya ili apate matibabu bora, alimtembelea Mwai Kibaki hospitalini lakini kwa bahati mbaya akaugua figo.
Baada ya kupata nafuu kwa muda mfupi, alifunga pingu za maisha na Yvonne Nambia.
Miezi miwili baada ya harusi yake, akaugua tena na kupelekwa Ulaya katika hospitali ya Royal Free Hospital ambako aliaga dunia masaa ya asubuhi tarehe 23 mwezi Agosti mwaka wa 2003.
Tuesday, 3 April 2012
Vituko
Mwanamke
mmoja aliyekuwa akitafutwa sana kwa kumuuwa afisa mmoja amekamatwa
kichakani akiwa haja ndogo na kubwa.
Joseph Kabila
Joseph
Kabila Kabange
alizaliwa kama Hippolyte Kanambe Kazemberembe Kabange Mtwale
Juni
4
1971
ni rais
wa
nne wa Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo.
Aliingia
katika uraisi baada ya kifo cha babake Rais Laurent-Desiree
Kabila
aliyeuawa
na wanajeshi tar. 16
Januari
2001.
Wanasiasa wengine walimteua mwana kuwa raisi baada ya baba.Katika uchaguzi wa kitaifa wa 30 Julai 2006 alipata kura nyingi kuwa raisi lakini hakufikia nusu ya kura zote. Katika uchaguzi wa pili kati yake na Jean-Pierre Bemba alishinda akathebitishwa kuwa rais tar. 17 Novemba 2006. Joseph Kabila ni rais wa kwanza wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo aliyechaguliwa na wananchi wote katika uchaguzi huru.
Joseph Kabila alizaliwa mjini Hewa Bora mkoani wa Kivu Kusini katika mashariki ya Kongo. Babake alikuwa mwanasiasa na kiongozi wa kikundi cha wanamgambo waasi waliopinga serikali ya Mobutu Sese Seko.
Joseph alihamia Dar es Salaam (Tanzania. Alisoma shule ya msingi na ya sekondari katika Dar es salaam na Mbeya na pia alisomea Chuo Kikuu cha Makerere na alisomea Uanajeshi. Octoba 1996 alikuwa Commanda wa kundi la "Kadogos" ambalo ni jeshi la watoto Inasemekana alitumia wakati ule jina la Hippolyte Kanambe Kazemberembe Kabange Mtwale kwa sababu za usalama.
Baada ya ushindi wa wapinzani dhidi ya Mobutu babake alikuwa rais na Joseph alipelekwa masomoni kwenye chuo cha kijeshi huko Uchina. Wakati wa kurudi alipewa cheo cha jenerali jeshini na mwaka 2000 alipandishwa cheo kuwa mkuu wa jeshi.
Alikuwa rais
Januari 26 2001 baada ya kifo cha babake Laurent-Desiree Kabila, na
kumfanya kuwa rais wa kwanza duniani aliyezaliwa katika miaka ya
1970s. Alikuwa rais mchanga Ulimwenguni hadi januari 2004.
Desemba 2002
alikubali mapatano ya amani kati ya serikali na waasi yaliyokuwa
msingi kwa ajili ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa na
maandalizi ya uchaguzi wa mwaka 2006.
juni 11 2004
mapinduzi ya kijeshi wakiongozwa naye Meja Eric Lenge walijaribu
kuchukuwa madaraka na kutangaza kwa radio ya taifa kwamba shughuli
zote za serikali zimesitishwa lakini walichindwa na askari wa Kabila.
Desemba 2005
kura ya maoni ya kupitisha katiba mpya ilifanyika na uchaguzi wa rais
ulifanyika Julai 30 2006 baada ya kusitishwa kwa tarehe ya hapo
awali. Kabila alishinda kwa asilimia 45% naye mpinzani wake na makamu
wa rais na mwaasi wa zamani Jean-Pierre Bemba alipata asilimia 20%,
Matokeo hayo yalikataliwa na kura zilirudiwa kati ya Kabila na Bemba
Oktoba 29.Novemba 15,tume ya uchaguzi ilitangaza matokeo rasmi na
Kabila kutangazwa kuwa mshindi na asilimia 58.05% za kura. Matokeo
hayo yalithibitishwa na Mahakama Kuu Novemba 27 2006 na kabila
kuapishwa Desemba 6 2006 kama rais.
Desemba 2011
Kabila alichaguliwa kwa kipindi cha pili kama rais. Baada ya matokeo
kutangazwa tarehe 9 Desemba, kulikuwa na vurugu katika machafuko huko
Kinshasa na Mbuji-Mayi ambapo ndiyo iliyo kuwa ngome kuu ya mpinzani
wa Kabila Etienne Tshisekedi
Juni Mosi baada
ya uvumi mbalimbali kutolewa na maafisa wa nyadhifa za juu serikalini
kuhusu ndoa yake,mkuu wa Kaya ya rais, Balozi Theodore Mugalu
alitangaza rasmi harusi ya rais na Olive Lembe di Sita.Harusi hiyo
ilitendeka Juni 17 2006 wana msichana aliyepewa jina Sifa, jina la
mamake Kabila
Monday, 2 April 2012
MARY ONYANGO
i)Alikuwa makamu mwenyakiti wa tume la shikamano na ushirikiano wa kitaifa.
ii)Alihitimu masomo yke katika Chuo Kikuu cha Nairobi na kupokea shahada ya Biashara. Pia alipokea shahada ya Mambo ya Kifedha kutoka Chuo cha Maastricht nchini Ketherlands
iii)Baada ya kuugua saratani ya matiti, aliungana na marehemu bi. Julia Mulaha ambaye pia laikuwa augua saratani, na kuanzisha programu ya kuwasaidia wanawke wanaougua saratani ya matiti nchini Kenya mwaka 1999.
iv)Akiwa bado katika chuo kikuu, alikuwa muigizaji katika tamthilia mbalimbali kama vile miaha.
iv)Akiwa bado katika chuo kikuu, alikuwa muigizaji katika tamthilia mbalimbali kama vile miaha.
KWAME NKRUMAH
Kwame Nkrumah alizaliwa mwaka 1909 katika eneo la Nkroful nchini Gold Coast.
Alimaliza masomo yake ya msingi katiika shule ya Achimota iliyoko Accra mwaka 1930, kisha akasomea katika shule ya katoliki ya Roman Catholic Seminary, ambako baadaye alianza kufunza shule moja ya kikatoliki iliyoko Axim.
Katika mwaka 1935, alienda kuendeleza masomo yake katika Chuo Kikuu cha Pennsylvania na kuhitimu masomo yake mwaka 1942.
Kwame alirudi Ghana na kufanywa kuwa katibu mkuu wa chama cha 'United Cold Coast Convention'. Mzozo uliibuka mwaka 1948 tarehe 28 mwezi Februari nchini Chana ambao ulimsababisha kutiwa mbaroni kwani, ilishukiwa kuwa chana cha UGCC ndicho kilichoanzisha mzozo huo.
Baada ya kuwekwa huru, alifanywa kuwa kiongozi wa Chama cha Vijana mwaka 1948.
Katiba ilirekebishwa katika mwaka 1952 mwezi Marchi tarehe 10 na Nkrumah akafanywa kuwa waziri mkuu wa kwanza nchini Ghana.
Katika mwaka 1966 mwezi Februari, akiwa bado akizuru nchini Vietnam na China, serikali ya Ghana ikapinduliwa katika mapinduzi ya kijeshi yaliyoanzishwa na Emmanuel Kwasi Kotaka na Baraza la National Liberation Council.
Nkrumah hakurudi Ghana na kuishi uhamishoni nchini Guinea, kama mgeni wa rais wa Guinea, Ahmed Sekou Toure.
Katika mwaka 1972 mwezi Aprili, Nkruma aliugua saratani ya ngozi na kuaga dunia akiwa na umri wa miaka 62.

Alimaliza masomo yake ya msingi katiika shule ya Achimota iliyoko Accra mwaka 1930, kisha akasomea katika shule ya katoliki ya Roman Catholic Seminary, ambako baadaye alianza kufunza shule moja ya kikatoliki iliyoko Axim.
Katika mwaka 1935, alienda kuendeleza masomo yake katika Chuo Kikuu cha Pennsylvania na kuhitimu masomo yake mwaka 1942.
Kwame alirudi Ghana na kufanywa kuwa katibu mkuu wa chama cha 'United Cold Coast Convention'. Mzozo uliibuka mwaka 1948 tarehe 28 mwezi Februari nchini Chana ambao ulimsababisha kutiwa mbaroni kwani, ilishukiwa kuwa chana cha UGCC ndicho kilichoanzisha mzozo huo.
Baada ya kuwekwa huru, alifanywa kuwa kiongozi wa Chama cha Vijana mwaka 1948.
Katiba ilirekebishwa katika mwaka 1952 mwezi Marchi tarehe 10 na Nkrumah akafanywa kuwa waziri mkuu wa kwanza nchini Ghana.
Katika mwaka 1966 mwezi Februari, akiwa bado akizuru nchini Vietnam na China, serikali ya Ghana ikapinduliwa katika mapinduzi ya kijeshi yaliyoanzishwa na Emmanuel Kwasi Kotaka na Baraza la National Liberation Council.
Nkrumah hakurudi Ghana na kuishi uhamishoni nchini Guinea, kama mgeni wa rais wa Guinea, Ahmed Sekou Toure.
Katika mwaka 1972 mwezi Aprili, Nkruma aliugua saratani ya ngozi na kuaga dunia akiwa na umri wa miaka 62.
Subscribe to:
Posts (Atom)