Friday, 13 April 2012
Winnie Madikizela-Mandela

Winnie Mandela alizaliwa Nomzamo Winfreda Madikizela tarehe 26 Septemba 1936, ni mwanasiasa kutoka Afrika ya Kusini na alishikilia nyadhifa mbalimbali serikalini na pia alikiongoza African National Congress ya Wanawake. Hivi sasa ni mwanachama wa ANC Kamati Kuu ya Taifa.Ingawa bado alikuwa ameoleka na Nelson Mandela wakati alikuwa rais wa Afrika Kusini mnamo Mei 1994,wanandoa hawa walikuwa wametengana miaka miwili baadaye. Talaka yao ilimaliza 19 Machi 1996, na makazi isiyojulikana nje ya mahakama. Jaribio la Winnie Mandela kupata makazi ya hadi dola milioni 5, nusu ya yale alidai ni thamani ya mume wake wa zamani, yalitupiliwa mbali na mahakama kwa kutoonekana mahakamani.

Machi 2009 tume ya Uchaguzi ilitoa uamuzi kuwa Winnie Mandela ambaye alichaguliwa kama mgombea wa ANC, anaweza kuwania Uchaguzi mkuu wa Aprili 2009, licha ya kuwa na kesi kotini na udanganyifu.
Jina lake Nomzamo linalomaanisha ''ajaribuye kitu'', alikutana na wakili na pia mwanaharakati Nelson Mandela 1957, Walioona 1958 na wana wasichana wawili. Juni 2010 alitibiwa kwa mshutuko wa moyo baada ya kusikia mjuku wake amefariki kwa ajali ya barabara usiku wa kufungua Kombe la Dunia. Ana ugonjwa wa Kisukari.
Licha ya vikwazo vya elimu kwa watu weusi wakati wa ubaguzi wa rangi,alipata shahada katika kazi za kijamii kutoka Jan Hofmeyer huko Johannesburg.
Bi. Mandela alijitokeza kama mpinzani kiongozi kwa wazungu wachache waliokuwa utawalani wa serikali katika miaka ya kifungu cha mumewe toka Agosti 1963 – Februari 1990, katika miaka hii alikuwa akikimbilia uhamishoni Brandfort isipokuwa ile tu siku aliyokubaliwa kumtembelea mumewe katika gereza la Roben Island.
Sifa yake iliharibika wakati akitoa hotuba yake Aprili 13 1986 wakati alitetea na kukubali watu kuchomwa wakiwa hai wakitumia gurudumu za gari ili kumaliza ubaguzi wa rangi. Fauka ya hayo hathi yake iliendelea kuharibika pale mlinzi wake, Jerry Musivuzi Richardson alisema eti Winnie aliamurisha utekaji nyara na mauaji.Desemba 29 1988 Richardson ambaye alikuwa kocha wa klabu ya mpira ya Mandela United ambayo ndiyo ndiyo ilikuwa kama ulinzi wa kibinafsi wa Bi. Mandela alisema kwamba ndiye aliyemuuwa kijana wa miaka 14 James Seipei ama Stompie Moeketsi miongoni mwa vijana wengine watatu.
Vituko
Mwanamke mmoja ampiga mmewe kisa na maana alipokuwa akienda kitandani wakati wa kulala Mme wake hakuenda kitandani naye bali alibaki aki facebook.
Thursday, 12 April 2012
Joyce Banda

Alikuwa pia mbunge na waziri wa jinsia, watoto na mambo ya Huduma za jamii. Kabla ya kushiriki katika siasa alikuwa mwanzilishi wa Joyce Banda Foundation, Mwanzilishi wa Chama cha Taifa cha Wafanyi biashara Wanawake (NABW), Viongozi Wanawake wachanga na mtandao wa mradi wa njaa. Alitajwa katika Forbes Magazine 2011 kama mwanamke wa tatu maarufu na mwenye nguvu zaidi katika Afrika.

Katika umri wa miaka 25 alikuwa tayari kashapata watoto watatu na alikuwa anaishi Nairobi Kenya. Yeye ni dada kwa Anjimile Oponyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Academy ya wasichana iliyoanzishwa na mwimbaji Madonna.
Ameolewa na Richard Banda,aliyekuwa Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Malawi.
Ana zawadi zaidi ya 10 kutoka nchini malawi na kimataifa.
Vituko
Mtoto mwenye umri wa miaka 15 ameokolewa na mwa wa jirani wao, baada ya kukimbizwa na kahaba mwanamke aliyekuwa anamdai. Mtoto huyo alikuwa anatoka dukani alipokuwa ametumwa na mamaye mwendo wa saa kumi na mbili jioni, hapo ndipo mwanamke huyo alipomuona na kuanza kumkimbiza, ndipo mbwa wa jirani alipomuona na kuanza kumkimbiza mwanamke huyo.
Ukweli Barani
Libreville, Gabon ndio nchi ya 5 Duniani ya gharama ya juu ama kubwa kuishi. Tokyo ndio ya kwanza.
Wednesday, 11 April 2012
Steven Kanumba

Steven Charles Kanumba alikuwa msanii wa maigizo na filamu kutoka nchini Tanzania. Katika historia ya tasnia ya filamu nchini Tanzania, Kanumba ndiye aliyekuwa msanii wa kwanza nchini kufanya kazi nje ya nchi na kuweza kuwavuta wageni kutoka nchi mbalimbali kuja kuigiza Tanzania. Hasa walikuwa Wanigeria kama vile Mercy Johnson, Emmanuel France, Nkiru Silvanus, Ramsey Nouah, na wengine wengi tu. Kanumba pia ameweza kuwaleta waongozaji filamu kadhaa was Kinigeria nchini.
Steven alizaliwa huko Shinyanga Januari 8 1984, alianza masomo yake katika shule ya msingi ya Bugoyi, na kuendela na masomo ya sekondari huko Mwadui na baadae kupata uhamisho katika shule moja jijini Dar es Salaam iitwayo Dar Christian Seminary. Alivyomaliza kidato cha nne akaendelea na masomo ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari ya Jitegemee ilioko huko huko Dar es salaam.
Kanumba
alieanza shughuli za kuigiza miaka mingi kwenye miaka ya "90".
Ila kufahamika zaidi alianza mwaka 2002
mara
tu baada ya kujiunga na kundi la sanaa ya maigizo maarufu kamaKaole
Sanaa Group.

Steven
Kanumba alitangaza
hivi karibuni nia ya kuwa mgombea katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka
2015.
Aliaga dunia tarehe 7
Aprili,
2012)
na kuzikwa hapo jana ma mia ya waombolezaji wakiwemo watu mashuhuri
serikalini pamoja na Mama Salma Kikwetu walihudhuria na kumuaga.
VITUKO
Mwanamke
mmoja afungwa miaka 10 gerezani kwa kumpa mtoto wake pombe aina ya
vodka. Mtoto huyo mwenye umri wa miaka 5 alipatikana hajielewi na
babake.Alipomuuliza mamake pia alikuwa amelewa chakari.
UKWELI BARANI AFRIKA
Chura
wakubwa zaidi duniani wanapatikana nchini Cameroon na ni zaidi ya
futi moja.
Tuesday, 10 April 2012
Mohamed Amin

Mohamed ''Mo'' Amin alikuwa mpiga picha maarufu zaidi kutoka Kenya alithihirisha haya kwa picha na kanda zake za video alizopiga kuhusu njaa ya Ethiopia.Alizaliwa Agosti 29 1943, kwenye mtaa wa Eastleigh Nairobi na ari yake ya picha ilianza akiwa shuleni. Ndiye mwanzilishi wa kampuni ya Camerapix mwaka 1963 huko Dar es Salaam na kuihamisha kampuni hiyo hadi Nairobi.Katika miak ya 1970 akawa wapiga wa kutegemewa zaidi kuhusu habari za Afrika,akiripoti kuhusu vita na mapinduzi barani afrika na picha zake zilitumika pia na runinga na wanahabari wa magharibi
Ushawishi wake mkubwa ulikuja wakati picha zake pamoja Micheal Buerk mpiga picha mwenza ziliripotia Njaa ya Ethiopia zilipoleta hisia kimataifa na hatimaye kusaidiya na kusababisha matamasha ya Live Aid iliofanya wimbo ''We are the World'' wake wasanii wote ulimwenguni kutungwa.

Novemba 23 1996 aliabiri ndege aina ya Ethiopian Airlines Flight 961 na Brian Tetley mwenye umri wa miaka 61 kurudi Nairobi baada ya kazi ya kibiashara nchini Ethiopia ndege hiyo ilitekwa nyara na kumlazimisha rubani kuilekeza ndege hiyo mashariki mwa bara indi, alijaribu kupigana nao watekanyara hao lakini ndege hiyo ikaaisha mafuta kuanguka kwenye ufuo wa visiwa vya Comoros. Amin aliaga papo hapo akiwa na umri wa miaka 53 rafikiye pia aliaga.
VITUKO
Nusura
harusi ikatizwe wakati Bi Harusi alipokiri kwamba alikuwa na mpango
wa kando. Kulingana na walioshuhudia, mwanadada huyu alieleza kwamba
atampenda mumewe hata ingawa anao mpango wa kando...!
FACTS
Maeneo
kame kabisa duniani yanapatikana Afrika, nayo ni Al'Kufrah huko
Libya, Aswan na Luxor nchini Misri, Wadi Halfa nchini Sudan, Mwari
Point nchini Namibia na Aoelef nchini Algeria.
Thursday, 5 April 2012
Jakaya Kikwete
Jakaya Mrisho Kikwete alizaliwa Octoba 7 1950 ni mtoto wa sita kwa familia ya watoto 9, ni rais wa 4 na wa sasa wa jamhuri ya Tanzania.Alizaliwa huko Msoga, Bagamoyo Tanganyika ambayo sasa ni Tanzania. Alikuwa pia mwenyekiti wa Umoja wa Afrika toka Januari 31 2008 hadi Februari 2 2009.
Alifuzu na digri ya Uchumi mwaka wa 1975 na kuamua kufanya kazi ya mapato duni kwa chama kilichokuwa kikitawala cha TANU ambapo kikawa ccm, hii ilimpa nafasi kufanya kazi katika maeneo ya vijiji na wilayani.
Kisha slijiunga na Jeshi na kuanza mazoezi katika kambi ya taifa ya Ruvu mwaka 1972. Baada ya kumaliza mazoezi na masomo yake ya kijeshi alikuwa Luteni 1976. Katika kazi yake ya jeshi alipanda ngazi hadi Lieutenat – Colonel. Kuanzia mwaka 1984 hadi 1986, Kikwete alikuwa Mkuu wa Siasa Mwalimu na Commissar wa Siasa katika Chuo cha Kijeshi.
Aliondoka jeshi kama kanali Luteni-wakati vyama vingi vilianza kuingia Tanzania mwaka 1992 na kuamua kuwa mwanasiasa kamili.
Katika siasa za vyama , Kikwete alianza kungaa mwaka 1982 ,wakati alichaguliwa kwa kura nyingi kwa chama cha CCM kuwa mjumbe wa kamati kuu ya taifa sera ya juu na kuwa muamuzi wa chama hicho. Tangu achaguliwe amekuwa akichaguliwa kila baada ya miaka mitano.
Rais Ally Hassan Mwinyi alimteua kuwa mbunge na wakati huo huo, naibu wa Nishati na Madini Novemba 7 1988. Mwaka 1990alipandishwa cheo na kuwa Waziri kamili wa Nishati, Maji na Madini. Baadaye mwaka huo huo, alifanikiwa kugombea kiti cha ubunge katika jimbo la Bagamoyo anapotoka.
1994 akiwa miaka 44 alikuwa waziri wa Fedha nyanga kuwahi kuhudumu katika historia ya Tanzania. Kwenye hazina ya Tanzania aliasisi nidhamu katika usimamizi wa fedha za umma na uwajibikaji hadi leo,yeye hukumbukwa kwa kuanzisha mfumo wa bajeti ya fedha na kufufua miundo ya ukusanyaji wa mapato, mbinu ya taasisi, ikiwa ni pamoja na maandalizi kwa ajili ya malezi.

Utawala wake kama Rais umeshutumiwa kwa kiasi kikubwa cha hongo na kutoshughulikia maswala yanayo wakumba raia wa nchi hiyo.
Ametuhumiwa pia kwa kuchaguwa marafiki wake wa karibu kuwa mawaziri jambo ambalo linamfanya kutowarekebisha wanapoenda kinyume na maadili mema.
Alipokuwa mwenyekiti wa AU changamoto yake kubwa ilikuwa jinsi alivyo shughulikia ghasia zilizo ikumba nchi yetu mwaka 2008.
Amemuowa Mama Salma Kikwete na wana watoto 8.
Vituko
Mama
mwenye umri wa miaka 32 amekichoma chumba cha kulala cha bintiye
mwenye umri wa miaka 16, akidai kwamba basi la kumpeleka skuli
lilikuwa linamwacha. Kulingana na msichana huyo, mamake alibisha
mlango kabla ya kutengeneza shimo kwenye mlango na kisha kuwasha moto
kwa karatasi na kuingiza kwenye shimo hilo. Moto huo ulichoma kiti
chumbani humo.Mama huyo naye aliwaambia askari kwamba mtoto alikuwa
anawachwa na basi sasa alifanya hivyo ili msichana wake atoke
chumbani humo.
Ukweli Barani
Je
wajua, Watu kumi na nane kutoka Afrika wametuzwa na tuzo ya Nobel.
Nao wanatoka Algeria, Misri, Ghana, Kenya, Nigeria na Afrika Kusini.
Wednesday, 4 April 2012
Ukweli Barani
Mogadishu, Somalia ni mji wa 4 hatari zaidi dunia. Johannesburg, Afrika Kusini ni ya 10 hatari zaidi kuishi duniani.
Vituko
Ajuza
mmoja wa miaka 70 amemshangaza mtoto wake wa kiume na majirani wake
kwa kutongoza kichuna wa kijana wake, na kuvalia mavazi ya kisasa ya
kijana na kuongea kwa lugha ya Sheng akisema ''Yo Yo mresh si uko juu
manze utamanga nini kuku chipo ama''
Mzee huyo aliyekuwa amevalia Jeans na kusag na tishati kubwa alifaulu kumwingiza kidosho huyo kwenye box
MICHAEL KIJANA WAMALWA
Alikuwa mkuu wa wanafunzi na mjadili bora katika shule yake ya sekondari ya Strathmore. Aliibuka kuwa mwanafunzi mwandishi bora nchini na akawakilisha Kenya katika ushindani wa uandishi wa insha huko Uingereza.
Mwaka 1965, alipewa tuzo la masomo ya jamii na kusoma sheria katika Chuo cha Cambridge na kufuzu mwaka 1968.
Alirejea Kenya mwaka 1970 na kuwa mwalimu wa kusomesha elimu ya sheria katika Chuo Kikuu cha Nairobi.
Mwaka wa 1974, alihusika katika kampeini za uchaguzi na kufaulu katika uchaguzi wa 1979.
Alihusika tena katika kampeini za uchaguzi wa vyama na akachaguliwa kuwa mbunge wa wilaya ya Saboti pamoja na kuwa Makamu wa kwanza wa mwenyekiti wa chama chake.
Baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha Ford Kenya, Oginga Odinga, kuaga dunia, alifanywa kuwa mwenyekiti wa hicho chama mwaka wa 1994.
Wamalwa alihusika tena katika kampeini za uchaguzi wa 2002 na kufanikiwa kuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais, huku Mwai Kibaki akichaguliwa kuwa rais wa Kenya.
Katika mwaka wa 2002, baada ya rais wa Kenya, Mwai Kibaki, kuhusika katika ajali ya barabara na kupelekwa Ulaya ili apate matibabu bora, alimtembelea Mwai Kibaki hospitalini lakini kwa bahati mbaya akaugua figo.
Baada ya kupata nafuu kwa muda mfupi, alifunga pingu za maisha na Yvonne Nambia.
Miezi miwili baada ya harusi yake, akaugua tena na kupelekwa Ulaya katika hospitali ya Royal Free Hospital ambako aliaga dunia masaa ya asubuhi tarehe 23 mwezi Agosti mwaka wa 2003.
Tuesday, 3 April 2012
Vituko
Mwanamke
mmoja aliyekuwa akitafutwa sana kwa kumuuwa afisa mmoja amekamatwa
kichakani akiwa haja ndogo na kubwa.
Joseph Kabila
Joseph
Kabila Kabange
alizaliwa kama Hippolyte Kanambe Kazemberembe Kabange Mtwale
Juni
4
1971
ni rais
wa
nne wa Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo.
Aliingia
katika uraisi baada ya kifo cha babake Rais Laurent-Desiree
Kabila
aliyeuawa
na wanajeshi tar. 16
Januari
2001.
Wanasiasa wengine walimteua mwana kuwa raisi baada ya baba.Katika uchaguzi wa kitaifa wa 30 Julai 2006 alipata kura nyingi kuwa raisi lakini hakufikia nusu ya kura zote. Katika uchaguzi wa pili kati yake na Jean-Pierre Bemba alishinda akathebitishwa kuwa rais tar. 17 Novemba 2006. Joseph Kabila ni rais wa kwanza wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo aliyechaguliwa na wananchi wote katika uchaguzi huru.
Joseph Kabila alizaliwa mjini Hewa Bora mkoani wa Kivu Kusini katika mashariki ya Kongo. Babake alikuwa mwanasiasa na kiongozi wa kikundi cha wanamgambo waasi waliopinga serikali ya Mobutu Sese Seko.
Joseph alihamia Dar es Salaam (Tanzania. Alisoma shule ya msingi na ya sekondari katika Dar es salaam na Mbeya na pia alisomea Chuo Kikuu cha Makerere na alisomea Uanajeshi. Octoba 1996 alikuwa Commanda wa kundi la "Kadogos" ambalo ni jeshi la watoto Inasemekana alitumia wakati ule jina la Hippolyte Kanambe Kazemberembe Kabange Mtwale kwa sababu za usalama.
Baada ya ushindi wa wapinzani dhidi ya Mobutu babake alikuwa rais na Joseph alipelekwa masomoni kwenye chuo cha kijeshi huko Uchina. Wakati wa kurudi alipewa cheo cha jenerali jeshini na mwaka 2000 alipandishwa cheo kuwa mkuu wa jeshi.
Alikuwa rais
Januari 26 2001 baada ya kifo cha babake Laurent-Desiree Kabila, na
kumfanya kuwa rais wa kwanza duniani aliyezaliwa katika miaka ya
1970s. Alikuwa rais mchanga Ulimwenguni hadi januari 2004.
Desemba 2002
alikubali mapatano ya amani kati ya serikali na waasi yaliyokuwa
msingi kwa ajili ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa na
maandalizi ya uchaguzi wa mwaka 2006.
juni 11 2004
mapinduzi ya kijeshi wakiongozwa naye Meja Eric Lenge walijaribu
kuchukuwa madaraka na kutangaza kwa radio ya taifa kwamba shughuli
zote za serikali zimesitishwa lakini walichindwa na askari wa Kabila.
Desemba 2005
kura ya maoni ya kupitisha katiba mpya ilifanyika na uchaguzi wa rais
ulifanyika Julai 30 2006 baada ya kusitishwa kwa tarehe ya hapo
awali. Kabila alishinda kwa asilimia 45% naye mpinzani wake na makamu
wa rais na mwaasi wa zamani Jean-Pierre Bemba alipata asilimia 20%,
Matokeo hayo yalikataliwa na kura zilirudiwa kati ya Kabila na Bemba
Oktoba 29.Novemba 15,tume ya uchaguzi ilitangaza matokeo rasmi na
Kabila kutangazwa kuwa mshindi na asilimia 58.05% za kura. Matokeo
hayo yalithibitishwa na Mahakama Kuu Novemba 27 2006 na kabila
kuapishwa Desemba 6 2006 kama rais.
Desemba 2011
Kabila alichaguliwa kwa kipindi cha pili kama rais. Baada ya matokeo
kutangazwa tarehe 9 Desemba, kulikuwa na vurugu katika machafuko huko
Kinshasa na Mbuji-Mayi ambapo ndiyo iliyo kuwa ngome kuu ya mpinzani
wa Kabila Etienne Tshisekedi
Juni Mosi baada
ya uvumi mbalimbali kutolewa na maafisa wa nyadhifa za juu serikalini
kuhusu ndoa yake,mkuu wa Kaya ya rais, Balozi Theodore Mugalu
alitangaza rasmi harusi ya rais na Olive Lembe di Sita.Harusi hiyo
ilitendeka Juni 17 2006 wana msichana aliyepewa jina Sifa, jina la
mamake Kabila
Monday, 2 April 2012
MARY ONYANGO
i)Alikuwa makamu mwenyakiti wa tume la shikamano na ushirikiano wa kitaifa.
ii)Alihitimu masomo yke katika Chuo Kikuu cha Nairobi na kupokea shahada ya Biashara. Pia alipokea shahada ya Mambo ya Kifedha kutoka Chuo cha Maastricht nchini Ketherlands
iii)Baada ya kuugua saratani ya matiti, aliungana na marehemu bi. Julia Mulaha ambaye pia laikuwa augua saratani, na kuanzisha programu ya kuwasaidia wanawke wanaougua saratani ya matiti nchini Kenya mwaka 1999.
iv)Akiwa bado katika chuo kikuu, alikuwa muigizaji katika tamthilia mbalimbali kama vile miaha.
iv)Akiwa bado katika chuo kikuu, alikuwa muigizaji katika tamthilia mbalimbali kama vile miaha.
KWAME NKRUMAH
Kwame Nkrumah alizaliwa mwaka 1909 katika eneo la Nkroful nchini Gold Coast.
Alimaliza masomo yake ya msingi katiika shule ya Achimota iliyoko Accra mwaka 1930, kisha akasomea katika shule ya katoliki ya Roman Catholic Seminary, ambako baadaye alianza kufunza shule moja ya kikatoliki iliyoko Axim.
Katika mwaka 1935, alienda kuendeleza masomo yake katika Chuo Kikuu cha Pennsylvania na kuhitimu masomo yake mwaka 1942.
Kwame alirudi Ghana na kufanywa kuwa katibu mkuu wa chama cha 'United Cold Coast Convention'. Mzozo uliibuka mwaka 1948 tarehe 28 mwezi Februari nchini Chana ambao ulimsababisha kutiwa mbaroni kwani, ilishukiwa kuwa chana cha UGCC ndicho kilichoanzisha mzozo huo.
Baada ya kuwekwa huru, alifanywa kuwa kiongozi wa Chama cha Vijana mwaka 1948.
Katiba ilirekebishwa katika mwaka 1952 mwezi Marchi tarehe 10 na Nkrumah akafanywa kuwa waziri mkuu wa kwanza nchini Ghana.
Katika mwaka 1966 mwezi Februari, akiwa bado akizuru nchini Vietnam na China, serikali ya Ghana ikapinduliwa katika mapinduzi ya kijeshi yaliyoanzishwa na Emmanuel Kwasi Kotaka na Baraza la National Liberation Council.
Nkrumah hakurudi Ghana na kuishi uhamishoni nchini Guinea, kama mgeni wa rais wa Guinea, Ahmed Sekou Toure.
Katika mwaka 1972 mwezi Aprili, Nkruma aliugua saratani ya ngozi na kuaga dunia akiwa na umri wa miaka 62.

Alimaliza masomo yake ya msingi katiika shule ya Achimota iliyoko Accra mwaka 1930, kisha akasomea katika shule ya katoliki ya Roman Catholic Seminary, ambako baadaye alianza kufunza shule moja ya kikatoliki iliyoko Axim.
Katika mwaka 1935, alienda kuendeleza masomo yake katika Chuo Kikuu cha Pennsylvania na kuhitimu masomo yake mwaka 1942.
Kwame alirudi Ghana na kufanywa kuwa katibu mkuu wa chama cha 'United Cold Coast Convention'. Mzozo uliibuka mwaka 1948 tarehe 28 mwezi Februari nchini Chana ambao ulimsababisha kutiwa mbaroni kwani, ilishukiwa kuwa chana cha UGCC ndicho kilichoanzisha mzozo huo.
Baada ya kuwekwa huru, alifanywa kuwa kiongozi wa Chama cha Vijana mwaka 1948.
Katiba ilirekebishwa katika mwaka 1952 mwezi Marchi tarehe 10 na Nkrumah akafanywa kuwa waziri mkuu wa kwanza nchini Ghana.
Katika mwaka 1966 mwezi Februari, akiwa bado akizuru nchini Vietnam na China, serikali ya Ghana ikapinduliwa katika mapinduzi ya kijeshi yaliyoanzishwa na Emmanuel Kwasi Kotaka na Baraza la National Liberation Council.
Nkrumah hakurudi Ghana na kuishi uhamishoni nchini Guinea, kama mgeni wa rais wa Guinea, Ahmed Sekou Toure.
Katika mwaka 1972 mwezi Aprili, Nkruma aliugua saratani ya ngozi na kuaga dunia akiwa na umri wa miaka 62.
Tuesday, 27 March 2012
Vituko
Mama wa mtoto mmoja amempa mtoto wake adhabu ya mwaka kwa kumwambia atembee maili mbili akiwa ananyeshewa. Mtoto huyo wa miaka 12 alipewa adhabu hiyo kwa kunywa pombe ya Vodka.
Abdoulaye Wade
Alizaliwa
Mai 29 1926 alikuwa rais wa tatu wa Senegali hadi tarehe 25 Marchi
2012 toka mwaka wa 2000.Yeye pia ni katibu mkuu wa chama cha
Senegalese party(PDS) na ameongoza chama hicho tangu 1974.Alikuwa
kiongozi wa upinzani kwa muda mrefu, na amewania urais mara
nne,kuanzia mwaka 1978,kabla ya kuchaguliwa mwaka 2000.Alisomea
sheria na kufunza Lycee Condorcet huko Ufaransa.
Wade
ana udhamini wa udaktari katika Sheria na uchumi.Alikuwa pia mkuu wa
Sheria na Uchumi wa Kitivo katika Chuo Kikuu cha Dakar nchini
Senegali.
Amemuowa
Viviane Wade. Mwana wao,Karim Wade alikuwa mkuu wa shirika la taifa
la Kiislamu,na toka Mei 2009 alihudumu kama Waziri wa Nchi kwa ajili
ya Ushirikiano wa Kimataifa,Mijini na Mikoa, Usafiri wa Unga na
barabara.Bintiye Sindjely Wade, ni msaidizi maalum wa Rais ambaye
alishirikikatika mikutano ya kampeni nyingi kimataifa.
Kufuatia
uchaguzi wa 1988, alikamatwa kutokana na maandamano dhidi ya matokeo.
Alipokea adhabu ya kusimamishwa kuwania kura.Hatimaye alikwenda
Ufaransa, lakini alirudi mwaka 1990.
Aprili
1991, Wade akiwa na jamaa wengine wanne wa chama cha PDS walijiunga
na serikali
ya umoja wa kitaifa pamoja na chama tawala cha Socialist Party (PS);
Wade akawa Waziri wa Nchi bila kupingwa Mnamo Oktoba 1992, yeye na
mawaziri wengine wa chama cha PDS wakajiuzulu kwenye serikali
kulingana na vile chama tawala cha PS kilivyokuwa kikiongoza
serikali.
Uchaguzi
wa Februari 1993 Wade alikuwa katika nafasi ya pili na asilimia 32%
nyuma ya Diouf ambaye alishinda na asilimia 58%. Octoba mosi ,
Wade,mkewe na wanachama wa PDS wawili wabunge walikamatwa na kufungwa
kutokana na kifo cha makamau wa rais wa baraza la katika.
Waliwachiliwa huru baada ya uchunguzi lakini Februari 1994 Wade
alikamatwa tena na wanachama wenzake kwa kutishia usalama wa serikali
na nchi, waliachiliwa Julai 4 baada ya maandamano ya wafuasi wake.
.
Alijiunga
na seikalikama waziri wa Nchi Machi 1995, lakini kama kawa alitoka
tena na wafuasi wake wa chama chake cha PDS Machi 1998.Ingawa
alichaguliwa kwa Bunge katika uchaguzi Februari 1998 wa bunge,
alitangazakujiuzulu kwake kutoka Bunge mwishoni mwa mwezi Julai 1998,
akisema kuwa kulikuwa na "manaibu wa
kutosha wa kufanya kazi aliyokuwa akifanya.

Kura za 2007 zilifanywa na pia alishinda, kisha kura za hivi karibuni yaani jumapili mwaka huu zilifanywa lakini alikubali kushindwa.
Monday, 26 March 2012
TABU LEY ROCHEREAU
Alizaliwa mwaka wa 1940, ni mwanamziki
kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Yeye ni kiongozi wa
Orchestre Afrisa International na kati ya washawishi wakubwa zaidi
zaidi katika Sauti na utunzi wa nyimbo pamoja na uandishi wa nyimbo
barani Afrika. Pamoja na mchezaji gitaa Dk.Nico Kasanda, walianzisha
kundi la Soukous, aliufanya muziki wake ukakubaliwa ulimwenguni kote
kwa kucheza muziki wa Kongo na ule wa Cuba, Caribbean na pia Amerika
ya Kusini Rumba.

Mwaka wa 1970 Tabu Ley pamoja na Franco
walitengeneza bendi ya Orchestre Afrisa International walirekodi
nyimbo kama ''Sorozo, ''Kaful Mayay'',''Aon Aon'' na Mose Konzo.

Mwaka wa 1985, serikali ya Kenya
ilipiga marufuku muziki wa kigeni kuchezwa kwenye radio ya taifa,
baada ya Tabu Ley kutunga wimbo wa ''Twende Nairobi''(Lets go
Nairobi) ulioimbwa naye M'bilia Bel kwa sifa ya rais wa Kenya Daniel
Moi, lakini marufuku hayo yalitupiliwa mbali.
Mwaka wa 1990 aliishi Kusini mwa
California.akaanza kupeleka muziki wake kimataifa kwa kutunga nyimbo
na kuimba kwa Kiingereza na kuoegeza mitindo tofauti kama vile Samba.
Alipata maarufu zaidi alipotoa albamu zake kama Muzina, Exil Ley
Afrika Worldwide na Babeti Soukous.
Mwaka wa 1996, Tabu Ley alishirikishwa
katika albamu Gombo Salsa na kundi la kucheza salsa la Africandos.
Wakati rais Mobutu Sese Seko
alipotolewa madarakani mwaka wa 1997 Tabu Ley alirudi Kinshasa na
kuwa waziri katika baraza la mawaziri kwa serikali mpya ya rais
Laurent Kabila. Kufuatia kifo cha Kabila Tabu Ley alijiunga na bunge
maalum la mpito iliyoundwa na Joseph Kabila hadi pale ilipotupilwa
mbali.
Novemba 2005 aliteuliwa Makamu Gavana
katika maswala ya Kisiasa, Utawala na kijamii na kitamaduni, katika
mji wa Kinshasa nafasi iliyopewa chama chake cha Kongo Rally for
Democracy kwa mkubaliano wa amani 2002.
Alirudi Ubelgiji kwa kuugua stroke.
Vituko
Mwanamke
mmoja wa nchi moja ametia fora kwa kuzaa watoto 18 ndani ya miaka
21 ya ndoa yake na mumewe. Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 40 na
ushee alijifungua mtoto wake wa 18 jana.
Pamoja na kuwa na watoto 18 mwanamke huyo na mumewe bado hawajaridhika tu na idadi ya watoto walionao na walielezea mpango wao wa kuzaa mtoto wa 19, vyombo vya habari vimeripoti.
Wanandoa hao wana watoto 12 wa kiume na watoto sita wa kike. Mtoto wao wa mwisho ndiye huyo aliyezaliwa jana ikiwa ni wiki moja tu baada ya mtoto wao wa kwanza kusherehekea kutimiza miaka 21.
"Siwezi kusema jinsi ninavyojisikia kuwa na watoto wengi lakini kila mtoto amekuja na baraka zake" alisema mwanamke huyo.
Mwanamke huyo alisema kwamba kwa jinsi alivyoenda kujifungua mara nyingi kwenye hospitali ya Kaplan iliyoko kwenye mji wa Rehovot, manesi wote wa hospitali hiyo wamemzoea sana.
"Tumezoeana sana kiasi cha kwamba utadhani na mimi nafanya kazi hospitali hiyo" alisema mwanamke huyo.
Pamoja na kuwa na watoto 18 mwanamke huyo na mumewe bado hawajaridhika tu na idadi ya watoto walionao na walielezea mpango wao wa kuzaa mtoto wa 19, vyombo vya habari vimeripoti.
Wanandoa hao wana watoto 12 wa kiume na watoto sita wa kike. Mtoto wao wa mwisho ndiye huyo aliyezaliwa jana ikiwa ni wiki moja tu baada ya mtoto wao wa kwanza kusherehekea kutimiza miaka 21.
"Siwezi kusema jinsi ninavyojisikia kuwa na watoto wengi lakini kila mtoto amekuja na baraka zake" alisema mwanamke huyo.
Mwanamke huyo alisema kwamba kwa jinsi alivyoenda kujifungua mara nyingi kwenye hospitali ya Kaplan iliyoko kwenye mji wa Rehovot, manesi wote wa hospitali hiyo wamemzoea sana.
"Tumezoeana sana kiasi cha kwamba utadhani na mimi nafanya kazi hospitali hiyo" alisema mwanamke huyo.
Friday, 23 March 2012
VITUKO
Mbwa mmoja amewashangaza waumini wa kanisa moja kwa kwenda kanisani na kuketi na kusikiliza neno.Mbwa huyo ambaye alifika mapema na kuketi katika kiti cha kwanza alionekana akifwatilia kila kitu kichokuwa kikitendeka kanisani.
Madilu System

Jean de Dieu Makiese aliyefahamika kama Madilu System , alikuwa muimbaji wa Soukous na muandishi wa nyimbo alizaliwa Léopoldville, Belgian Congo. Alikuwa wakati mmoja katika bendi ya TPOK Jazz,bendi iliyoongoza katika Miziki za Kufana za Afrika kwenye mika za 1960 na 1970.
Alizaliwa Mai 28 1952,na akiwa angali kijana mdogo
1969 Madilu aliimba na kundi la Orchestre Symba, Orchestre Bambula
iliyo ongozwa na Papa Noel kisha alitengeneza bendi yake iliyoitwa
Orchestre Bakuba Mayopi.
Baadaye alijiunga na Franco na akawa mwanamziki
mashuhuri ulimwenguni, Franco ndiye aliyempa jina hilo la Madilu
System, jina ambalo lilibaki hadi sasa. Wimbo wake wa kwanza na TPOK
Jazz ni ''Mamou(Tu Vois)'' wimbo ambao ulivuma zaidi 1984. kisha
ulifwatiwa na wimbo wake mwenyewe ''Pesa Position'' , kisha akatoa
wimbo ''Mario'' Mwaka 1985 yeye na Franco walitoa wimbo''Reponse de
Mario'' ambao unasemekana ndio wimbo mtamu zaidi kuwahi kuimbwa na
wasanii hawa wawili pamoja.
Baada ya kifo cha Franco bendi ya TPOK Jazz aliwacha
kurekodi muziki kwa mwaka mmoja. Baadaye bendi hiyo wakaja pamoja
chini ya usimamazi wa Madilu System.
Aliaaza kuimba mwenyewe akahamia Pari mji mkuu wa
Ufaransa kisha akaenda Geneva Switzerland.

UKWELI BARANI
Kuna nchi 54 barani Afrika. Chuo Kikuu cha zamani na
cha kale zaidi ulimwenguni kinapatikana mjiini Timbuktu Mali. Katika
karne ya 12 Mji huo ulikuwa na vyou vitatu. Zaidi ya wanafunzi 25,000
walisomea kwenye chuo kimoja.
Wednesday, 21 March 2012
VITUKO
Maharusi wamewashangaza jamaa na marafiki baada ya kuwaalika kwenye harusi ya na kupata hawana mavazi ya harusi la wamejichora mwilini kote kama nguo za harusi.
FRANCO LUAMBO LUANZO MAKIADI
Alizaliwa Julai 6 1938 alikuwa jamaa mashuhuru katika karne ya ishirini kwenye muziki wa Kongo, na muziki wa Afrika kwa ujumla. Yeye ni msanii anayejulikana ulimwengu kote kama Franco Luambo ama Franco. Anajulikana sana kwa ustadi wake wa Rumba, alipewa jina la utani 'Mchawi wa Guitar' kwa ajili ya kucheza kwake ala hiyo. Kama muasisi na mwanzilishi wa kundi la OK Jazz anahesabiwa pia kama mwanzilishi wa muziki na sauti ya Kongo.
Alizaliwa katika kijiji cha Sona Bata katika magharibi mwa Bas Zaire ambao sasa ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo siku za ukoloni ikiitwa (Kongo ya Ubelgiji). Alipokuwa bado mtoto wazazi wake walihamia mji mkuu wa Leopoldville (sasa Kinshasa). Babake Joseph Emongo, alikuwa mfanyikazi wa reli wakati mamake alikuwa akipika mikate na kuuza sokoni.Akiwa miaka saba alitengeneza gitaa ambayo alicheza ili kuwavutia wanunuzi katika duka ambalo mamake aliuzia.
Talanta yake ilimsisimua Paul Ebengo Dewayon ambaye alimfunza kucheza ala hiyo. Akiwa miaka 12 alijiunga na kundi la Paul na bendi yake. Miaka mitatu baadaye alitunga rekodi yake ya kwanza Bolingo na ngai na Beatrice (My Love for Beatrice)
Mwaka wa 1955 Franco aliunda bendi yake pamoja na Jean Serge Essous na kuitwa OK Bar huko Leopoldville. Mwaka uliofuatia jina la bendi hiyo likabadilishwa na kuwa OK Jazz kisha likaitwa TPOK Jazz kwa heshima ya mahali lililoazishwa. Basi bendi hiyo ikawa bendi kubwa zaidi kwa muziki wa kongo na likawa na waimbaji 30 kufikia 1980 toka waimbaji 6. Franco alidai kwamba bendi hiyo ilitoa albamu 150 kwa muda wa miak 30 ya bendi hiyo.
Mwaka wa 1958 Franco alitiwa mbaroni, lakini alikuwa ameshakuwa mwimbaji mashuhuri aliachiliwa kutokana na mashabiki wake waliomtaka atolewe jelani.
Franco ameonekana kuwa mfanyabiashara maarufu, na kutengeneza idadi ya makampuni ya kurekodi ya kudhibiti kazi yake mwenyewe na kulea vipaji vipya kama vile (Surboum OK Jazz, Epanza Makita, Boma Bango and Éditions Populaires). Katika miaka ya 1970 muziki wa kikongo ulienea katika Afrika, ukiongozwa na OK Jazz.
Mwaka wa 1980 Franco alitajwa na kupewa jina la ''Grand Master'' wa miziki wa Zaire na Serikali ya nchi hiyo. Jambo hili lilibadilisha mada za nyimbo zake kwa kasi katika kipindi hiki na kuanza kuimba nyimbo za kizalendo na kusifu mashabiki wake matajiri.
Franco alizuru Marekani kwa mara ya kwanza na ya mwisho mwaka wa 1983
Mwaka wa 1985 alitoa wimbo wake mkubwa zaidi Mario, ambao unamaanisha jamaa anayeishi kwa mpenzi wake mzee wa zamani.

Tuesday, 20 March 2012
World Story Telling Day
Leo ni siku ya kusimulia hadithi Ulimwenguni.Katika siku hii watu husimuliana na husikiza hadithi kwa kila Lugha za Ulimwengu.Usiku na Mchana watu huadithiana na hupeana moyo na motisha ili kusoma kitu kuhusu mtu au kitu.
Ni siku ya kipekee Ulimwenguni ambayo watu hujifunza mengi kutokana na hadithi zao, kiini cha siku ya leo ni kuhusu Miti.
Babatunde Olatunji
Alizaliwa Aprili 7, 1927, alikuwa mpiga ngoma, mwanaharakati wa kijamii na msanii wa kurekodi mziki.
Olatunji alizaliwa katika kijiji cha Ajido, mji mdogo karibu na Badagry kusini magharibi mwa Nigeria. Alipata udhamini na kwenda kusomea huko Atlanta mwaka wa 1950.
Ameshinda zawadi nyingi sana katika kazi yake ya muziki.
Alitunga mziki uliotumiwa katika filamu ya Hollywood ya Raisin in the Sun.
VITUKO
Mwanamke mmoja wa miaka 35 ameshtakiwa kwa kuiba chupa mbili za pombe kwenye bar moja. Mwanamke huyo alipatikana akiweka chupa hizo kwenye kwapa zake na chupa ingine alitaka kuweka katikati ya matiti yake.
Monday, 19 March 2012
BAABA MAAL

Baaba
Maal alitarajiwa kufuata babake na kuwa mvuvi. Hata hivyo, chini ya
ushawishi wa maisha yake Mansour Seck rafikiye, Baaba alijitoa
mwenyewe kwa kujifunza muziki kutoka kwa mama yake na Mkuu wa shule
aliyosomea. Aliendelea kusoma muziki kwenye chuo kikuu katika Dakar
kabla ya kuondoka kwa ajili ya masomo ya shahada ya uzamili kwa
udhamini katika Beaux-Sanaa mjini Paris.Anajulikana sana barani
Afrika na Ulimwenguni kote, huenda akawa mwanamziki maarufu huko
Senagali baada ya Youssou N'Dour.
VITUKO
Mama wa mtoto mmoja amempa
mtoto wake adhabu ya kusimama kwa barabara na alama zake za mtihani
zikiwa zimeandikwa kwenye ubao mkubwa mtoto huyo akiwa ameubeba ili
watu waone. Kijana huyo alienda nyumbani na alama mbaya. Babake
alimuona mtoto wake akienda barabarani na ubao uliokuwa na maadishi
'' Nataka kuwa mtoto mkorofi wa darasa''
Na upande mwingine maadishi
yalisoma nipo darasa la nane na nimepata alama ya E kila somo.
Akiwaabia wanahabari wa
runinga fulani mtoto huyo alisema nimepata alama ya E kwa darasa
langu na kama adhabu napaswa kuwa hapa hadi saa saba.
Thursday, 15 March 2012
UKWELI BARANI
Inajulikana
kama reli ndefu ulimwenguni na ni ya Mauritania na ina urefu wa Maili
1.8 yani kilomita 3 na safari hiyo huchukuwa masa 12.
VITUKO
Abiria na wananchi waliozidi elfu 50 wake kwa waume wa nchi fulani hapa Afrika walinunua baskeli kila mmoja na kuendesha baskeli zao wakiwa uchi wa mnyama kisa na maana ni kuwa waendeshaji magari wamekuwa hawajali na ajali za barabara zilizidi. Waendeshaji baskeli hao walijiandika kwenye mwili wao wakisema huu ni mwili wangu.
Subscribe to:
Posts (Atom)