Alizaliwa mwaka wa 1940, ni mwanamziki
kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Yeye ni kiongozi wa
Orchestre Afrisa International na kati ya washawishi wakubwa zaidi
zaidi katika Sauti na utunzi wa nyimbo pamoja na uandishi wa nyimbo
barani Afrika. Pamoja na mchezaji gitaa Dk.Nico Kasanda, walianzisha
kundi la Soukous, aliufanya muziki wake ukakubaliwa ulimwenguni kote
kwa kucheza muziki wa Kongo na ule wa Cuba, Caribbean na pia Amerika
ya Kusini Rumba.
Tabu Ley alizaliwa katika mkoa wa
Bandundu, kama Pascal Tabu. Mwaka wa 1954, akiwa na umri wa miaka 18
akiandika wimbo wake wa kwanza Bessama Muchacha ambao alirekodi na
Joseph ''Grand Kalle'' kwenye bendi ya Kabasele ya Afrika Jazz. Tabu
Ley aliimba wimbo wa Uhuru wa Afrika wa Independence Cha Cha
uliotungwa na Grand Kalle wakati Kongo ilipata Uhuru wake mwaka 1960
na kumfanya kuwa maarufu zaidi. Alikaa kwenye bendi hiyo hadi 1963
wakati yeye na Dk. Nico Kasanda waliunda bendi yao Afrikan Fiesta.
Miaka miwili baadaye walitawanyika na Tabu Ley kuunda bendi ya
Afrikan Fiesta National ambayo ilijulikana pia kama Afrikan Fiesta
Flash. Bendi hiyo ikawa yenye mafanikio na bendi iliyojistawi zaidi
katika historia ya Afrika kwa kurekodi Afrikan Classic kama Afrika
Mokili Mobimba na kupata mauzo zaidi ya nakala millioni moja mwaka
1970. Papa Wemba na Sam Mangwana.
Mwaka wa 1970 Tabu Ley pamoja na Franco
walitengeneza bendi ya Orchestre Afrisa International walirekodi
nyimbo kama ''Sorozo, ''Kaful Mayay'',''Aon Aon'' na Mose Konzo.
Katika miaka ya 1980 Tabu Ley alikundua
talanta mpya ya uimbaji na kucheza, M'bilia Bel ambaye alichangia
kuikuza bendi hiyo yake. M'bilia akwa mwanamke wa kwanza barani
Afrika kucheza na kuimba Soukous. M'bilia na Tabu Ley walioana na
kujaliwa na mtoto mmoja.Mwaka wa 1988 Tabu Ley alileta Mwanamke
mwingine wa kuimba anayejulikana kama Faya Tess, kisha mbilia Mbel
alijitoa kwenye bendi hiyo na akaendelea kuwa maarufu.Baada ya kutoka
M'bilia bendi hiyo na ile ya TPOK Jazz walianza kuwa na upinzani
mkubwa zaidi mashabiki nao pia wakagawanya wengi wakikimbilia bendi
ilyocheza mtindo mpya wa Soukous.
Mwaka wa 1985, serikali ya Kenya
ilipiga marufuku muziki wa kigeni kuchezwa kwenye radio ya taifa,
baada ya Tabu Ley kutunga wimbo wa ''Twende Nairobi''(Lets go
Nairobi) ulioimbwa naye M'bilia Bel kwa sifa ya rais wa Kenya Daniel
Moi, lakini marufuku hayo yalitupiliwa mbali.
Mwaka wa 1990 aliishi Kusini mwa
California.akaanza kupeleka muziki wake kimataifa kwa kutunga nyimbo
na kuimba kwa Kiingereza na kuoegeza mitindo tofauti kama vile Samba.
Alipata maarufu zaidi alipotoa albamu zake kama Muzina, Exil Ley
Afrika Worldwide na Babeti Soukous.
Mwaka wa 1996, Tabu Ley alishirikishwa
katika albamu Gombo Salsa na kundi la kucheza salsa la Africandos.
Wakati rais Mobutu Sese Seko
alipotolewa madarakani mwaka wa 1997 Tabu Ley alirudi Kinshasa na
kuwa waziri katika baraza la mawaziri kwa serikali mpya ya rais
Laurent Kabila. Kufuatia kifo cha Kabila Tabu Ley alijiunga na bunge
maalum la mpito iliyoundwa na Joseph Kabila hadi pale ilipotupilwa
mbali.
Novemba 2005 aliteuliwa Makamu Gavana
katika maswala ya Kisiasa, Utawala na kijamii na kitamaduni, katika
mji wa Kinshasa nafasi iliyopewa chama chake cha Kongo Rally for
Democracy kwa mkubaliano wa amani 2002.
Alirudi Ubelgiji kwa kuugua stroke.

No comments:
Post a Comment