Pages

Wednesday, 21 March 2012

FRANCO LUAMBO LUANZO MAKIADI



Alizaliwa Julai 6 1938 alikuwa jamaa mashuhuru katika karne ya ishirini kwenye muziki wa Kongo, na muziki wa Afrika kwa ujumla. Yeye ni msanii anayejulikana ulimwengu kote kama Franco Luambo ama Franco. Anajulikana sana kwa ustadi wake wa Rumba, alipewa jina la utani 'Mchawi wa Guitar' kwa ajili ya kucheza kwake ala hiyo. Kama muasisi na mwanzilishi wa kundi la OK Jazz anahesabiwa pia kama mwanzilishi wa muziki na sauti ya Kongo.

Alizaliwa katika kijiji cha Sona Bata katika magharibi mwa Bas Zaire ambao sasa ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo siku za ukoloni ikiitwa (Kongo ya Ubelgiji). Alipokuwa bado mtoto wazazi wake walihamia mji mkuu wa Leopoldville (sasa Kinshasa). Babake Joseph Emongo, alikuwa mfanyikazi wa reli wakati mamake alikuwa akipika mikate na kuuza sokoni.Akiwa miaka saba alitengeneza gitaa ambayo alicheza ili kuwavutia wanunuzi katika duka ambalo mamake aliuzia.

Talanta yake ilimsisimua Paul Ebengo Dewayon ambaye alimfunza kucheza ala hiyo. Akiwa miaka 12 alijiunga na kundi la Paul na bendi yake. Miaka mitatu baadaye alitunga rekodi yake ya kwanza Bolingo na ngai na Beatrice (My Love for Beatrice)

Mwaka wa 1955 Franco aliunda bendi yake pamoja na Jean Serge Essous na kuitwa OK Bar huko Leopoldville. Mwaka uliofuatia jina la bendi hiyo likabadilishwa na kuwa OK Jazz kisha likaitwa TPOK Jazz kwa heshima ya mahali lililoazishwa. Basi bendi hiyo ikawa bendi kubwa zaidi kwa muziki wa kongo na likawa na waimbaji 30 kufikia 1980 toka waimbaji 6. Franco alidai kwamba bendi hiyo ilitoa albamu 150 kwa muda wa miak 30 ya bendi hiyo.

Mwaka wa 1958 Franco alitiwa mbaroni, lakini alikuwa ameshakuwa mwimbaji mashuhuri aliachiliwa kutokana na mashabiki wake waliomtaka atolewe jelani.

Franco ameonekana kuwa mfanyabiashara maarufu, na kutengeneza idadi ya makampuni ya kurekodi ya kudhibiti kazi yake mwenyewe na kulea vipaji vipya kama vile (Surboum OK Jazz, Epanza Makita, Boma Bango and Éditions Populaires). Katika miaka ya 1970 muziki wa kikongo ulienea katika Afrika, ukiongozwa na OK Jazz.

Mwaka wa 1980 Franco alitajwa na kupewa jina la ''Grand Master'' wa miziki wa Zaire na Serikali ya nchi hiyo. Jambo hili lilibadilisha mada za nyimbo zake kwa kasi katika kipindi hiki na kuanza kuimba nyimbo za kizalendo na kusifu mashabiki wake matajiri.

Franco alizuru Marekani kwa mara ya kwanza na ya mwisho mwaka wa 1983
Mwaka wa 1985 alitoa wimbo wake mkubwa zaidi Mario, ambao unamaanisha jamaa anayeishi kwa mpenzi wake mzee wa zamani.


Mwaka wa 1987 uvumi ulianza kwamba Franco anaugua sana.Wimbo aliotoa mwaka huo ulikuwa ''Attention Na SIDA''(jihadharini na UKIMWI) kuwaonya kuambukizwa ugonjwa huo,na hivyo kusababisha uvumi lakini bila kudhibitisha kwamba ana virusi vya HIV. Akaanza kutoa nguvu zake kutoka OK Jazz, bendi hiyo ikaanza kurudi chini. Kisha Franco akabadisha dini kutoka kwa Uislamu na kuwa Mkatoliki wa Kirumi. Oktoba 12 1989 aliaga dunia akiwa katika kilinikii ya Ubelgiji. Mwili wake ukasafirisha nyumbani Zaire ambapo jeneza lake lilikuwa limefungwa na bendera ya nchi hiyo polisi walisindikiza mwili wake kwa njia ya barabara na takriban milioni moja wakiomboleza. Serikali ilitangaza siku nne za maombolezo ya kitaifa huku redio zikicheza nyimbo zake tu bila nyimbo zingine. Alizikwa tarehe 17 Oktoba.

No comments:

Post a Comment