Pages

Friday, 23 March 2012

Madilu System


Jean de Dieu Makiese aliyefahamika kama Madilu System , alikuwa muimbaji wa Soukous na muandishi wa nyimbo alizaliwa Léopoldville, Belgian Congo. Alikuwa wakati mmoja katika bendi ya TPOK Jazz,bendi iliyoongoza katika Miziki za Kufana za Afrika kwenye mika za 1960 na 1970.
Alizaliwa Mai 28 1952,na akiwa angali kijana mdogo 1969 Madilu aliimba na kundi la Orchestre Symba, Orchestre Bambula iliyo ongozwa na Papa Noel kisha alitengeneza bendi yake iliyoitwa Orchestre Bakuba Mayopi.
Baadaye alijiunga na Franco na akawa mwanamziki mashuhuri ulimwenguni, Franco ndiye aliyempa jina hilo la Madilu System, jina ambalo lilibaki hadi sasa. Wimbo wake wa kwanza na TPOK Jazz ni ''Mamou(Tu Vois)'' wimbo ambao ulivuma zaidi 1984. kisha ulifwatiwa na wimbo wake mwenyewe ''Pesa Position'' , kisha akatoa wimbo ''Mario'' Mwaka 1985 yeye na Franco walitoa wimbo''Reponse de Mario'' ambao unasemekana ndio wimbo mtamu zaidi kuwahi kuimbwa na wasanii hawa wawili pamoja.
Baada ya kifo cha Franco bendi ya TPOK Jazz aliwacha kurekodi muziki kwa mwaka mmoja. Baadaye bendi hiyo wakaja pamoja chini ya usimamazi wa Madilu System.
Aliaaza kuimba mwenyewe akahamia Pari mji mkuu wa Ufaransa kisha akaenda Geneva Switzerland.
Mwanzoni mwa Agosti 2007, Madilu alisafiri kwenda Kinshasa kupiga video ya nyimbo zake. Alizimia Ijumaa tarehe 10 2007 Agosti. Alipelekwa katika hospitali huko Kinshasa, ambapo aliagaa siku iliyofuatia asubuhi.


No comments:

Post a Comment