Pages

Tuesday, 27 March 2012

Vituko




Mama wa mtoto mmoja amempa mtoto wake adhabu ya mwaka kwa kumwambia atembee maili mbili akiwa ananyeshewa. Mtoto huyo wa miaka 12 alipewa adhabu hiyo kwa kunywa pombe ya Vodka.

Abdoulaye Wade





Alizaliwa Mai 29 1926 alikuwa rais wa tatu wa Senegali hadi tarehe 25 Marchi 2012 toka mwaka wa 2000.Yeye pia ni katibu mkuu wa chama cha Senegalese party(PDS) na ameongoza chama hicho tangu 1974.Alikuwa kiongozi wa upinzani kwa muda mrefu, na amewania urais mara nne,kuanzia mwaka 1978,kabla ya kuchaguliwa mwaka 2000.Alisomea sheria na kufunza Lycee Condorcet huko Ufaransa.
Wade ana udhamini wa udaktari katika Sheria na uchumi.Alikuwa pia mkuu wa Sheria na Uchumi wa Kitivo katika Chuo Kikuu cha Dakar nchini Senegali.

Amemuowa Viviane Wade. Mwana wao,Karim Wade alikuwa mkuu wa shirika la taifa la Kiislamu,na toka Mei 2009 alihudumu kama Waziri wa Nchi kwa ajili ya Ushirikiano wa Kimataifa,Mijini na Mikoa, Usafiri wa Unga na barabara.Bintiye Sindjely Wade, ni msaidizi maalum wa Rais ambaye alishirikikatika mikutano ya kampeni nyingi kimataifa.

Kufuatia uchaguzi wa 1988, alikamatwa kutokana na maandamano dhidi ya matokeo. Alipokea adhabu ya kusimamishwa kuwania kura.Hatimaye alikwenda Ufaransa, lakini alirudi mwaka 1990.
Aprili 1991, Wade akiwa na jamaa wengine wanne wa chama cha PDS walijiunga na serikali ya umoja wa kitaifa pamoja na chama tawala cha Socialist Party (PS); Wade akawa Waziri wa Nchi bila kupingwa Mnamo Oktoba 1992, yeye na mawaziri wengine wa chama cha PDS wakajiuzulu kwenye serikali kulingana na vile chama tawala cha PS kilivyokuwa kikiongoza serikali.
Uchaguzi wa Februari 1993 Wade alikuwa katika nafasi ya pili na asilimia 32% nyuma ya Diouf ambaye alishinda na asilimia 58%. Octoba mosi , Wade,mkewe na wanachama wa PDS wawili wabunge walikamatwa na kufungwa kutokana na kifo cha makamau wa rais wa baraza la katika. Waliwachiliwa huru baada ya uchunguzi lakini Februari 1994 Wade alikamatwa tena na wanachama wenzake kwa kutishia usalama wa serikali na nchi, waliachiliwa Julai 4 baada ya maandamano ya wafuasi wake.
.
Alijiunga na seikalikama waziri wa Nchi Machi 1995, lakini kama kawa alitoka tena na wafuasi wake wa chama chake cha PDS Machi 1998.Ingawa alichaguliwa kwa Bunge katika uchaguzi Februari 1998 wa bunge, alitangazakujiuzulu kwake kutoka Bunge mwishoni mwa mwezi Julai 1998, akisema kuwa kulikuwa na "manaibu wa kutosha wa kufanya kazi aliyokuwa akifanya.
Katika raundi ya kwanza ya Uchaguzi wa 2000 za urais zilizofanyika Februari 27 alikuwa wa pili tena akipata asilimia 31% za kura lakini kwa mara ya kwanza Diouf hakushinda raundi ya kwanza ya wingi wa kura, na raundi ya pili ikafanyika Machi 19 Wade akashinda na asilimia 58.49% Wade akawa rais Aprili Mosi 2000

Kura za 2007 zilifanywa na pia alishinda, kisha kura za hivi karibuni yaani jumapili mwaka huu zilifanywa lakini alikubali kushindwa.

Ukweli Barani



Nchi kumi masikini Duniani zatoka Afrika.

Monday, 26 March 2012

TABU LEY ROCHEREAU



Alizaliwa mwaka wa 1940, ni mwanamziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Yeye ni kiongozi wa Orchestre Afrisa International na kati ya washawishi wakubwa zaidi zaidi katika Sauti na utunzi wa nyimbo pamoja na uandishi wa nyimbo barani Afrika. Pamoja na mchezaji gitaa Dk.Nico Kasanda, walianzisha kundi la Soukous, aliufanya muziki wake ukakubaliwa ulimwenguni kote kwa kucheza muziki wa Kongo na ule wa Cuba, Caribbean na pia Amerika ya Kusini Rumba.

Tabu Ley alizaliwa katika mkoa wa Bandundu, kama Pascal Tabu. Mwaka wa 1954, akiwa na umri wa miaka 18 akiandika wimbo wake wa kwanza Bessama Muchacha ambao alirekodi na Joseph ''Grand Kalle'' kwenye bendi ya Kabasele ya Afrika Jazz. Tabu Ley aliimba wimbo wa Uhuru wa Afrika wa Independence Cha Cha uliotungwa na Grand Kalle wakati Kongo ilipata Uhuru wake mwaka 1960 na kumfanya kuwa maarufu zaidi. Alikaa kwenye bendi hiyo hadi 1963 wakati yeye na Dk. Nico Kasanda waliunda bendi yao Afrikan Fiesta. Miaka miwili baadaye walitawanyika na Tabu Ley kuunda bendi ya Afrikan Fiesta National ambayo ilijulikana pia kama Afrikan Fiesta Flash. Bendi hiyo ikawa yenye mafanikio na bendi iliyojistawi zaidi katika historia ya Afrika kwa kurekodi Afrikan Classic kama Afrika Mokili Mobimba na kupata mauzo zaidi ya nakala millioni moja mwaka 1970. Papa Wemba na Sam Mangwana.
Mwaka wa 1970 Tabu Ley pamoja na Franco walitengeneza bendi ya Orchestre Afrisa International walirekodi nyimbo kama ''Sorozo, ''Kaful Mayay'',''Aon Aon'' na Mose Konzo.

Katika miaka ya 1980 Tabu Ley alikundua talanta mpya ya uimbaji na kucheza, M'bilia Bel ambaye alichangia kuikuza bendi hiyo yake. M'bilia akwa mwanamke wa kwanza barani Afrika kucheza na kuimba Soukous. M'bilia na Tabu Ley walioana na kujaliwa na mtoto mmoja.Mwaka wa 1988 Tabu Ley alileta Mwanamke mwingine wa kuimba anayejulikana kama Faya Tess, kisha mbilia Mbel alijitoa kwenye bendi hiyo na akaendelea kuwa maarufu.Baada ya kutoka M'bilia bendi hiyo na ile ya TPOK Jazz walianza kuwa na upinzani mkubwa zaidi mashabiki nao pia wakagawanya wengi wakikimbilia bendi ilyocheza mtindo mpya wa Soukous.

Mwaka wa 1985, serikali ya Kenya ilipiga marufuku muziki wa kigeni kuchezwa kwenye radio ya taifa, baada ya Tabu Ley kutunga wimbo wa ''Twende Nairobi''(Lets go Nairobi) ulioimbwa naye M'bilia Bel kwa sifa ya rais wa Kenya Daniel Moi, lakini marufuku hayo yalitupiliwa mbali.

Mwaka wa 1990 aliishi Kusini mwa California.akaanza kupeleka muziki wake kimataifa kwa kutunga nyimbo na kuimba kwa Kiingereza na kuoegeza mitindo tofauti kama vile Samba. Alipata maarufu zaidi alipotoa albamu zake kama Muzina, Exil Ley Afrika Worldwide na Babeti Soukous.

Mwaka wa 1996, Tabu Ley alishirikishwa katika albamu Gombo Salsa na kundi la kucheza salsa la Africandos.

Wakati rais Mobutu Sese Seko alipotolewa madarakani mwaka wa 1997 Tabu Ley alirudi Kinshasa na kuwa waziri katika baraza la mawaziri kwa serikali mpya ya rais Laurent Kabila. Kufuatia kifo cha Kabila Tabu Ley alijiunga na bunge maalum la mpito iliyoundwa na Joseph Kabila hadi pale ilipotupilwa mbali.

Novemba 2005 aliteuliwa Makamu Gavana katika maswala ya Kisiasa, Utawala na kijamii na kitamaduni, katika mji wa Kinshasa nafasi iliyopewa chama chake cha Kongo Rally for Democracy kwa mkubaliano wa amani 2002.



Alirudi Ubelgiji kwa kuugua stroke.  

Ukweli Barani Afrika

Mahali ambapo pana joto jingi dunia ni Al'Aziziyah nchini Libya

Vituko



Mwanamke mmoja wa nchi moja ametia fora kwa kuzaa watoto 18 ndani ya miaka 21 ya ndoa yake na mumewe. Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 40 na ushee alijifungua mtoto wake wa 18 jana.

Pamoja na kuwa na watoto 18 mwanamke huyo na mumewe bado hawajaridhika tu na idadi ya watoto walionao na walielezea mpango wao wa kuzaa mtoto wa 19, vyombo vya habari vimeripoti.

Wanandoa hao wana watoto 12 wa kiume na watoto sita wa kike. Mtoto wao wa mwisho ndiye huyo aliyezaliwa jana ikiwa ni wiki moja tu baada ya mtoto wao wa kwanza kusherehekea kutimiza miaka 21.

"Siwezi kusema jinsi ninavyojisikia kuwa na watoto wengi lakini kila mtoto amekuja na baraka zake" alisema mwanamke huyo.

Mwanamke huyo alisema kwamba kwa jinsi alivyoenda kujifungua mara nyingi kwenye hospitali ya Kaplan iliyoko kwenye mji wa Rehovot, manesi wote wa hospitali hiyo wamemzoea sana.

"Tumezoeana sana kiasi cha kwamba utadhani na mimi nafanya kazi hospitali hiyo" alisema mwanamke huyo. 

Friday, 23 March 2012

VITUKO

Mbwa mmoja amewashangaza waumini wa kanisa moja kwa kwenda kanisani na kuketi na kusikiliza neno.Mbwa huyo ambaye alifika mapema na kuketi katika kiti cha kwanza alionekana akifwatilia kila kitu kichokuwa kikitendeka kanisani.

Madilu System


Jean de Dieu Makiese aliyefahamika kama Madilu System , alikuwa muimbaji wa Soukous na muandishi wa nyimbo alizaliwa Léopoldville, Belgian Congo. Alikuwa wakati mmoja katika bendi ya TPOK Jazz,bendi iliyoongoza katika Miziki za Kufana za Afrika kwenye mika za 1960 na 1970.
Alizaliwa Mai 28 1952,na akiwa angali kijana mdogo 1969 Madilu aliimba na kundi la Orchestre Symba, Orchestre Bambula iliyo ongozwa na Papa Noel kisha alitengeneza bendi yake iliyoitwa Orchestre Bakuba Mayopi.
Baadaye alijiunga na Franco na akawa mwanamziki mashuhuri ulimwenguni, Franco ndiye aliyempa jina hilo la Madilu System, jina ambalo lilibaki hadi sasa. Wimbo wake wa kwanza na TPOK Jazz ni ''Mamou(Tu Vois)'' wimbo ambao ulivuma zaidi 1984. kisha ulifwatiwa na wimbo wake mwenyewe ''Pesa Position'' , kisha akatoa wimbo ''Mario'' Mwaka 1985 yeye na Franco walitoa wimbo''Reponse de Mario'' ambao unasemekana ndio wimbo mtamu zaidi kuwahi kuimbwa na wasanii hawa wawili pamoja.
Baada ya kifo cha Franco bendi ya TPOK Jazz aliwacha kurekodi muziki kwa mwaka mmoja. Baadaye bendi hiyo wakaja pamoja chini ya usimamazi wa Madilu System.
Aliaaza kuimba mwenyewe akahamia Pari mji mkuu wa Ufaransa kisha akaenda Geneva Switzerland.
Mwanzoni mwa Agosti 2007, Madilu alisafiri kwenda Kinshasa kupiga video ya nyimbo zake. Alizimia Ijumaa tarehe 10 2007 Agosti. Alipelekwa katika hospitali huko Kinshasa, ambapo aliagaa siku iliyofuatia asubuhi.


UKWELI BARANI



Kuna nchi 54 barani Afrika. Chuo Kikuu cha zamani na cha kale zaidi ulimwenguni kinapatikana mjiini Timbuktu Mali. Katika karne ya 12 Mji huo ulikuwa na vyou vitatu. Zaidi ya wanafunzi 25,000 walisomea kwenye chuo kimoja.

Wednesday, 21 March 2012

VITUKO



Maharusi wamewashangaza jamaa na marafiki baada ya kuwaalika kwenye harusi ya na kupata hawana mavazi ya harusi la wamejichora mwilini kote kama nguo za harusi.

FRANCO LUAMBO LUANZO MAKIADI



Alizaliwa Julai 6 1938 alikuwa jamaa mashuhuru katika karne ya ishirini kwenye muziki wa Kongo, na muziki wa Afrika kwa ujumla. Yeye ni msanii anayejulikana ulimwengu kote kama Franco Luambo ama Franco. Anajulikana sana kwa ustadi wake wa Rumba, alipewa jina la utani 'Mchawi wa Guitar' kwa ajili ya kucheza kwake ala hiyo. Kama muasisi na mwanzilishi wa kundi la OK Jazz anahesabiwa pia kama mwanzilishi wa muziki na sauti ya Kongo.

Alizaliwa katika kijiji cha Sona Bata katika magharibi mwa Bas Zaire ambao sasa ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo siku za ukoloni ikiitwa (Kongo ya Ubelgiji). Alipokuwa bado mtoto wazazi wake walihamia mji mkuu wa Leopoldville (sasa Kinshasa). Babake Joseph Emongo, alikuwa mfanyikazi wa reli wakati mamake alikuwa akipika mikate na kuuza sokoni.Akiwa miaka saba alitengeneza gitaa ambayo alicheza ili kuwavutia wanunuzi katika duka ambalo mamake aliuzia.

Talanta yake ilimsisimua Paul Ebengo Dewayon ambaye alimfunza kucheza ala hiyo. Akiwa miaka 12 alijiunga na kundi la Paul na bendi yake. Miaka mitatu baadaye alitunga rekodi yake ya kwanza Bolingo na ngai na Beatrice (My Love for Beatrice)

Mwaka wa 1955 Franco aliunda bendi yake pamoja na Jean Serge Essous na kuitwa OK Bar huko Leopoldville. Mwaka uliofuatia jina la bendi hiyo likabadilishwa na kuwa OK Jazz kisha likaitwa TPOK Jazz kwa heshima ya mahali lililoazishwa. Basi bendi hiyo ikawa bendi kubwa zaidi kwa muziki wa kongo na likawa na waimbaji 30 kufikia 1980 toka waimbaji 6. Franco alidai kwamba bendi hiyo ilitoa albamu 150 kwa muda wa miak 30 ya bendi hiyo.

Mwaka wa 1958 Franco alitiwa mbaroni, lakini alikuwa ameshakuwa mwimbaji mashuhuri aliachiliwa kutokana na mashabiki wake waliomtaka atolewe jelani.

Franco ameonekana kuwa mfanyabiashara maarufu, na kutengeneza idadi ya makampuni ya kurekodi ya kudhibiti kazi yake mwenyewe na kulea vipaji vipya kama vile (Surboum OK Jazz, Epanza Makita, Boma Bango and Éditions Populaires). Katika miaka ya 1970 muziki wa kikongo ulienea katika Afrika, ukiongozwa na OK Jazz.

Mwaka wa 1980 Franco alitajwa na kupewa jina la ''Grand Master'' wa miziki wa Zaire na Serikali ya nchi hiyo. Jambo hili lilibadilisha mada za nyimbo zake kwa kasi katika kipindi hiki na kuanza kuimba nyimbo za kizalendo na kusifu mashabiki wake matajiri.

Franco alizuru Marekani kwa mara ya kwanza na ya mwisho mwaka wa 1983
Mwaka wa 1985 alitoa wimbo wake mkubwa zaidi Mario, ambao unamaanisha jamaa anayeishi kwa mpenzi wake mzee wa zamani.


Mwaka wa 1987 uvumi ulianza kwamba Franco anaugua sana.Wimbo aliotoa mwaka huo ulikuwa ''Attention Na SIDA''(jihadharini na UKIMWI) kuwaonya kuambukizwa ugonjwa huo,na hivyo kusababisha uvumi lakini bila kudhibitisha kwamba ana virusi vya HIV. Akaanza kutoa nguvu zake kutoka OK Jazz, bendi hiyo ikaanza kurudi chini. Kisha Franco akabadisha dini kutoka kwa Uislamu na kuwa Mkatoliki wa Kirumi. Oktoba 12 1989 aliaga dunia akiwa katika kilinikii ya Ubelgiji. Mwili wake ukasafirisha nyumbani Zaire ambapo jeneza lake lilikuwa limefungwa na bendera ya nchi hiyo polisi walisindikiza mwili wake kwa njia ya barabara na takriban milioni moja wakiomboleza. Serikali ilitangaza siku nne za maombolezo ya kitaifa huku redio zikicheza nyimbo zake tu bila nyimbo zingine. Alizikwa tarehe 17 Oktoba.

Tuesday, 20 March 2012

World Story Telling Day


Leo ni siku ya kusimulia hadithi Ulimwenguni.Katika siku hii watu husimuliana na husikiza hadithi kwa kila Lugha za Ulimwengu.Usiku na Mchana watu huadithiana na hupeana moyo na motisha ili kusoma kitu kuhusu mtu au kitu.

Ni siku ya kipekee Ulimwenguni ambayo watu hujifunza mengi kutokana na hadithi zao, kiini cha siku ya leo ni kuhusu Miti.

Babatunde Olatunji


Alizaliwa Aprili 7, 1927, alikuwa mpiga ngoma, mwanaharakati wa kijamii na msanii wa kurekodi mziki.

Olatunji alizaliwa katika kijiji cha Ajido, mji mdogo karibu na Badagry kusini magharibi mwa Nigeria. Alipata udhamini na kwenda kusomea huko Atlanta mwaka wa 1950.
Ameshinda zawadi nyingi sana katika kazi yake ya muziki.
Alitunga mziki uliotumiwa katika filamu ya Hollywood ya Raisin in the Sun.


Olatunji aliaga dunia mwaka wa 2003 Aprili 6.

VITUKO



Mwanamke mmoja wa miaka 35 ameshtakiwa kwa kuiba chupa mbili za pombe kwenye bar moja. Mwanamke huyo alipatikana akiweka chupa hizo kwenye kwapa zake na chupa ingine alitaka kuweka katikati ya matiti yake.

Monday, 19 March 2012

BAABA MAAL


Alizaliwa Novemba 12 1953 ni mwanamziki kutoka Senegali na mchezaji Guitarist,alizaliwa huko Podor kwenye mto wa Senegali.Licha ya kucheza Guitar yeye pia anawezacheza ala zingine.Ametoa Albamu nyingi sana. Julai mwaka 2003 alifanywa mjumbe wa vijana wa UNDP.

Baaba Maal alitarajiwa kufuata babake na kuwa mvuvi. Hata hivyo, chini ya ushawishi wa maisha yake Mansour Seck rafikiye, Baaba alijitoa mwenyewe kwa kujifunza muziki kutoka kwa mama yake na Mkuu wa shule aliyosomea. Aliendelea kusoma muziki kwenye chuo kikuu katika Dakar kabla ya kuondoka kwa ajili ya masomo ya shahada ya uzamili kwa udhamini katika Beaux-Sanaa mjini Paris.Anajulikana sana barani Afrika na Ulimwenguni kote, huenda akawa mwanamziki maarufu huko Senagali baada ya Youssou N'Dour.

VITUKO



Mama wa mtoto mmoja amempa mtoto wake adhabu ya kusimama kwa barabara na alama zake za mtihani zikiwa zimeandikwa kwenye ubao mkubwa mtoto huyo akiwa ameubeba ili watu waone. Kijana huyo alienda nyumbani na alama mbaya. Babake alimuona mtoto wake akienda barabarani na ubao uliokuwa na maadishi '' Nataka kuwa mtoto mkorofi wa darasa''
Na upande mwingine maadishi yalisoma nipo darasa la nane na nimepata alama ya E kila somo.
Akiwaabia wanahabari wa runinga fulani mtoto huyo alisema nimepata alama ya E kwa darasa langu na kama adhabu napaswa kuwa hapa hadi saa saba.

Thursday, 15 March 2012

UKWELI BARANI





Inajulikana kama reli ndefu ulimwenguni na ni ya Mauritania na ina urefu wa Maili 1.8 yani kilomita 3 na safari hiyo huchukuwa masa 12.

VITUKO




Abiria na wananchi waliozidi elfu 50 wake kwa waume wa nchi fulani hapa Afrika walinunua baskeli kila mmoja na kuendesha baskeli zao wakiwa uchi wa mnyama kisa na maana ni kuwa waendeshaji magari wamekuwa hawajali na ajali za barabara zilizidi. Waendeshaji baskeli hao walijiandika kwenye mwili wao wakisema huu ni mwili wangu.

GRACE OGOT



Ni mwandishi, Nesi, Mwandishi wa habari, Mwanasiasa na Mwanadiplomasia kutoka Kenya.
Alipozaliwa alipewa jina la Grace Emily Akinyi katika sehemu wilayani Asembo, katika mkoa wa Nyanza. Alisomea mafunzo yake ya nesi nchini Uganda na Uingereza. Alifanya kazi kama mkunga, kama mwalimu, kama mwandishi wa habari, kama mtangazaji wa huduma ya ng'ambo ya BBC, na katika cheo cha usimamizi katika kampuni ya Air India Corporation ya Afrika Mashariki. Mwaka wa 1984 akawa moja wa wanawake wachache kuhudumu kama mbunge na mwanamke wa kipekee aliyehudumu ka naibu Waziri katika Baraza la Mawaziri la Rais Daniel arap Moi.

Tangu wakati huo ameshikilia nyadhifa mbalimbali za ubalozi kwani amewakilisha nchi yake katika Umoja wa Mataifa na UNESCO. Alikuwa mwanachama mwanzilishi wa shirika la Waandishi wa Kenya maarufu kwa Kiingereza kama Writers' Association of Kenya.

Grace Ogot aliyezaliwa 1934 alifunga ndoa na mwanahistoria Profesa Bethwell Allan Ogot, kutoka sehemu ya Gem, mnamo mwaka wa 1959 na ni mama wa watoto wanne.
Kitabu chake cha kwanza kilikuwa Land Without Thunder kitabu cha hadithi fupi. Riwaya yake ya kwanza ilikuwa The Promised Land.

Grace Ogot anaweza kusemekana kuwa mmoja ya waandishi bora zaidi barani Afrika. Mtindo wake wa uandishi wake ni wa kuvutia sana hasa katika ubunifu wake wa wazi; yeye huweza kuonyesha Utabibu wa mila na tamaduni ya Kiafrika, yanayofuata njia mwafaka na ishara.

Wednesday, 14 March 2012

Charity Ngilu



Charity Ngilu Kaluki alizaliwa 1952, ni mwanasiasa kutoka Kenya. Alikuwa waziri wa Afya kutoka 2003 hadi 2007 na aliteuliwa waziri wa Maji Aprili 2008.

Alizaliwa kule mbooni wilayani Makueni 1952, alipata elimu yake kwenye shule ya upili ya Alliance High School, kisha alifanya kazi kama karani wa wa benki ya Central ya Kenya kabla ya kuanzisha biashara yake.

Katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi hapa nchini mwaka1992 aliwashangaza wengi kwa kupita kura za Kitui ya kati katika chama cha Democratic Paty.

Uchaguzi wa Desemba 1997 aliwania urais pamoja na Wangari Maathai wanawake wa kwanza kuwania urais nchini, wakati huo akiwa kwa chama cha Social Democratic Party na alimaliza wa tano.

Baadaye alijiunga na chama cha National Party of Kenya. Uchaguzi wa 2002 chama chake kilikuwa miongoni mwa vyama vilivyo tengeneza NARC muungano huo wa NARC ulishinda uchaguzi huo na Mwai Kibaki alimteuwa waziri wa Afya Januari 3 2003.

Julai 31 2007 Ngilu alimpeleka Ann Njogu mwandamaji hospitalini baada ya kupigwa na polisi, kisha alihutumiwa na kukashifiwa kwa madai ya kumtorosha Njogu polisini, alikamatwa na kufungwa Agosti 12 na kisha kutoka kwa thamani.

Oktoba 5,2007 ngilu alitangaza kujiunga na ODM na mwaniaji urais wa chama hicho Raila Odinga katika kura za 2007 na alimlinganisha Bw Odinga na Bw Nelson Mandela.

Bwanake Micheal Mwendwa Ngilu aliaga Julai mosi, 2006 Afrika Kusini na ana watoto watatu.

VITUKO



Mtoto wa miaka 8 amewashangaza waziziwe na majirani kwa kuvuta sigara. Babake msichana huyo anasema aliaza kuvuta sigara akiwa na umri wa miaka 4, na sasa yeye huvuta hadi packeti 2 kila siku na asipovuta sigara huanza kulia.

UKWELI BARANI.



Wanyama wanne wa porini ambao wana mbio zaidi wanapatikana barini afrika, Miongoni ni Duma, Simba,WildBeest, na Thomson's gazelle. Wanyama hawa wote wana mbio zaidi ya maili 50 kwa lisali moja, na Duma akiweza kufikisha maili 70 kwa lisali.

Tuesday, 13 March 2012

Martha Karua.



Martha Wangari Karua alizaliwa 22 Septemba 1957, ni mwanasiasa kutoka Kenya na pia ni mbunge wa Gichugu na wakili wa mahakama kuu ya Kenya. Alikuwa waziri wa Sheria lakini alijiuzuli mnamo Aprili 2009.



Karua alizaliwa katika Wilaya ya Kirinyaga, Mkoa wa Kati wa Kenya, yeye ni wa pili katika familia ya watoto nane, wasichana wanne na wavulana wanne. Alisomea sheria katika Chuo Kikuu cha Nairobi 1977-1980. Kati ya mwaka 1980 na 1981 alijiunga na shule ya sheria Kenya School of Law, baada ya hapo alijiunga na utumishi wa umma na kufanya kazi na kufanya kazi kama hakimu kutoka 1981 – 1987. Kutoka 1987 – 2002 alifanya kazi katika mazoezi binafsi kama mtetezi.

Alifanya kazi katika mahakama ya hakimu wilayani na kupanda ngazi hadi Hakimu mkazi Mwandamizi hadi alipotoka 1987. Katika kipindi hiki, alikuwa alikuwa msimamizi wa mahakama za sheria Makadara 1984 – 1985 na Mahakama za Kibera 1986 – 1987.

Yeye alichangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya sheria ya familia na hasa ugawaji wa mali ya ndoa pamoja na sheria ya kikatiba na utawala.

Kutoka mwaka wa 1990 – 2002 alikuwa mwanachama wa harakati za upinzani wa kisiasa ambao walipigania demokrasia ya vyama vingi nchini Kenya katika miaka ya 1990 wakati Kenya ilikuwa chini ya utawala wa Daniel Moi.
Alikuwa mmoja wa waliotengeneza chama cha NARC kilichoshinda kura za 2003 na kumaliza miongo minee ya utawala wa KANU.
Alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa NARC Novemba 15 2008.
Alikuwa waziri wa kwanza kujiuzulu kwa hiyari yake tangu 2003.

UKWELI BARANI



Karibia asilimia 90 za kasi za Malaria duniani kote hutokea Afrika, na watoto 3,000 kutoka Afrika hufariki kila siku kutokana na mathara yake.

VITUKO


Mwanamme mmoja alijipangia kifo chake alipopigwa na risasi karibu na kaburi lake alilojichimbia. Imebaki haijulikani kama alipanga ama ilikuwa kwa bahati mbaya.

Friday, 9 March 2012

TIRUNESH DIBABA



Dibaba

Pia anajulikana kama Tirunesh Dibaba Kenene alizaliwa Oktoba 1 1985 huko Bekoji, Arsi Uhabeshini (Ethiopia). Ni mwanariadha wa masafa marefu. Kwa sasa Ndiye bingwa wa Olompiki kwa mbio za mita 5000 na mita 10,000, amepewa jina la utani 'Baby Faced Destroyer'.

Alizaliwa katika kijiji cha Bekoji, Dibaba ni mtoto wa 4 kwa watoto 6. Alianza riadha akiwa na umri wa miaka 14, na alihamia mji mkuu wa Addis Ababa mwaka 2000.

Dibaba anatoka kwa familia ya wanariadha dada zake na ndugu zake pia wakiwa kwenye nyanja hiyo ya riadha.
Dibaba amepata mafanikio makubwa katika michuano ya dunia matukio ya riadha ya 2003,2006 na 2007.
Aliweka upya rekodi ya dunia katika mbio za mita 5000 kwa muda wa 14:11.15 katika mkutano wa Oslo Golden League mwaka 2008.
Alishinda dhahabu kwa mbio za mita 10,000 katika michezo ya Olimpiki huko Beijing Agosti 2008, na kuweka rekodi mpya ya Olimpiki kwa muda wa 29:54.66 rekodi ya hapo awali ikishikiliwa na binamuye Deratu Tulu kwa muda wa 30:17.49 katika michezo ya Summer Olimpik huko Sydney 2000.

Wiki moja baadaye akashinda mbio za mita 5000 Agosti 22 2008.
Dibaba ameolewa kwa mshindi wa mbio za Olimpiki wa mwaka wa 2004 na 2008 Sileshi Sihine.

VITUKO



Polisi mmoja ameshtakiwa kwa madai ya kula mlungula miaka miwili baada ya kifo chake.
Polisi huyo aliyeaga ameshtakiwa kwa kukubali rushwa ya shillingi elfu 100,000 kutoka kwa binamu wa jambazi sugu wa mtaa huo ambaye alikuwa anasakwa sana..
Aliaga kwa mshtuko wa moyo miaka miwili kabla ya kesi hiyo.
Jaji wa kesi hiyo aliambia koti kwamba watu waliofariki hawawezi toa ushuhuda.lakini atiwe pingu akiwa kwenye kaburi lake.

UKWELI BARANI



Zaidi ya watu milioni 17 katika Afrika kusini mwa Sahara wamefariki kutokana na UKIMWI, na wataalamu wanakadiria kuwa angalau zaidi ya watu milioni 25 wana UKIMWI kutoka Afrika.

Thursday, 8 March 2012

BENJAMIN MKAPA

Mkapa alizaliwa mwaka wa 1938 huko Ndanda Tnzania kusini. Alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda mwaka 1962 na shahada ya Kiingereza. Pia alihudhuria Chuo Kikuu cha Columbia mwaka 1963 na akatuzwa shahada yake katika masuala ya kimataifa.
Alikuwa ni afisa wa utawala wa Dodoma na waziri wa Teknolojia ya Sayansi na Elimu ya juu.
Tangu mwaka 1977 hadi 1990 alikuwa ni Waziri wa mambo ya kigeni.
Katika mwaka wa 1995, Mkapa alichaguliwa kuwa rais wa Tamzania kwa kufuatilia misingi ya kampeni maarufu ya kupambana na rushwa na kuwa mfuasi mwamini wa aliyekuwa rais wa Tanzania Julius Nyerere.
Mkapa alitoa juhudi za kupambana na rushwa na kuumba jukwaa la wazi la Rushwa la Tume ya Rais.
Akiwa bado rais, Mkapa alibinafsisha mashirika ya serikali na akaweka sera za soko huru,
Wafuasi wake walisema kuwa kuvutia uwekezaji wa kigeni ungesaidia kukuza uchumi.
Sera zake zilipata msaada wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani na kusababisha kufutwa kwa baadhi ya madeni ya kigeni ya Tanzania.
Uongozi wake kama rais wa Tanzania ulifika kikomo mwezi Desemba mwaka 2005.

VITUKO


Huku wanawake wakisherehekea siku yao Duniani mwanamke mmoja Nchini Zimbabwe amewashangaza watu kwa kutaka kufunga ndoa na kumuowa mwanawe mwenye umri wa miaka 24.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 42 alisema kwamba wakati bwanake aliaga miaka 6 iliyopita hakuna mtu yeyote alimsaidia kumsomesha mwanawe na sasa hataki msichana yeyote kumkaribia mwanawe eti kwa sababu ana kazi. Kuongeza maji kwenye Unga mwanamke huyo amesema tayari ni mja mzito na miezi sita na mwanawe.
Mwanamke huyo alisema ndugu za marehemu bwanake walionyesha hari ya kumrithi lakini yeye hataki anataka mwanawe, basi mwanawe pia amekubali atamuowa mamake.

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI






Nchi zingine kama Uchina, Russia, Vietnam na Bulgaria siku ya leo ni sikuku ya kitaifa.
Siku hii wanawake wanaadhimisha miaka 101 tangu siku hii izinduliwe.

Kiini cha siku hii ni 'Connecting Girls, Inspiring Future' Yaani KUUNGANISHA WASICHANA KUHIMIZA HATIMA

BAADHI TU YA WANAWAKE WALIOFUZU KWA NYANJA MBALIMBALI

Luisa Diogo ni Waziri Mkuu wa nchi ya Mozambique .

Ellen Sirleaf-Johnson ndiye rais wa kwanza mwanamke barani Afrika wa nchi ya Liberia.
Sylvie Kinigi ndiye mwanamke wa kwanza kuwa Waziri Mkuu barani Afrika wa nchi ya Burund.
Wanawake wanashikilia asilimia 18% za nyadhifa za ubunge Ulimwenguni,
Marekani ipo katika nafasi ya 68 kwa mataifa 134 ulimwenguni kwa asilimia 16.8% ya wanawake ambao wapo bungeni.
Oktoba 2003 nchi ya Rwanda ndio nchi iliyo karibia idadi ya wanawake kwa wanaume bungeni.
Kwa Serikali 189 Duniani kuna wanawake 13 ambao wanashikilia nyadhifa za juu sana.ambao ni
  • Angela Merkel, Chancellor of Germany
  • Cristina Fernández de Kirchner, President of Argentina
  • Ellen Johnson-Sirleaf, President of Liberia
  • Gloria Macapagal-Arroyo, President of the Philippines
  • Helen Clark, Prime Minister of New Zealand
  • Luisa Diogo, Prime Minister of Mozambique
  • Mary McAleese, President of Ireland
  • Micheline Calmy-Rey, President of the Swiss Confederation
  • Michelle Bachelet, President of Chile
  • Pratibha Patil, President of India
  • Tarja Halonen, President of Finland
  • Yulia Tymoshenko, Prime Minister of Ukraine
  • Zinaida Greceanîi, Prime Minister of Moldova
    FACTS ABOUT WOMEN
    Kwa watu milioni 876 ya waliosoma kwa nchi zilizostawi duniani thulithi mbili ni wanawake.
    Wanawake hukuza ama huzalisha nusu ya chakula duniani lakini wana asilimia moja tu ya shamba.
    Katika nchi ya Saudi Arabia mwanake anaweza kupa talaka mme wake iwapo hatampa chai.
    Mwanamke aliye stawi ana viatu 20, ambavyo viatu 11 kwa hivyo hatawahi vivaa.
    Wanawake huongea mara tatu zaidi ya wanaume, Uchunguzi umeonchesha kwamba wanawake takriban maneno 20,000 kwa siku, na wanaume maneno 7,000
    Wanawake huchukua takriban miaka 2 ya maisha yao wakijiangalia kwenye kioo, na wao husema kwamba Tv sio nzuri kama ilivyokuwa hapo zamani
     HISTORY
    Siku ya Wanawake Duniani ni siku ya kimataifa inayosherehekea mafanikio ya kiuchumi, kisiasa na kijamii ya wanawake kutoka vizazi vilivyopita, vya sasa na vya baadaye.

    Mashirika, serikali na mashirika ya wanawake kote duniani huchagua mandhari tofauti kila mwaka kwa kutafakari masuala ya jinsia ya kimataifa na serikali za mitaa.

    Siku hii ilianza kusherehekewa katika miaka ya 1910.

    Siku hii ya wanawake ilisherehekewa Machi 19 ,1911 huko Ujerumani, Australia, Denmark na nchi zingine za ulaya. Wanawake wa nchi zii walisherehekea siku hii kwa sababu ya wanawake kunyimwa haki za kupiga kura na mfalame wa nchi ya Prussian.

    Kiini cha kutenga siku hii ilikuwa ni
    kuwapa uhuru wa kupiga kua
    Uhuru wa kutoa maoni yao
    Uhuru wa kufanya kazi kwa ofisi za uma
    Uhuru wa kwenda shule miongoni maswala mengi.
    Tunaposherehekea siku 101 ya wanawake Shirika la wanawake la Kenya FIDA wamesema wanachukuwa fursa hii kuangalia mafanikio wanawake wamepata.
     

TEKLA LORUPE CHEPKITE



Alizaliwa Mei 9 1973 katika Kutomwony Kenya, ni mkimbiaji wa mbio za masafa marefu na msemaji wa kimataifa kwa ajili ya amani, haki za wanawake na elimu.
Lorupe anashikilia rekodi ya dunia kwa kilomita 20,25 na 30 na hapo awali alishikilia rekodi ya marathon duniani. Ni bingwa wa wa marathon duniani na alikuwa mwanamke mwafrika wa kwanza kushinda mbio za marathon za New York ambazo ameshinda mara mbili.Ameshinda marathon katika miji kama London, Boston, Hong Kong, Berlin, Rome na nchi nyingine nyingi.

Utotoni mwake alikuwa akienda shambani, akichunga ngombe na kuwaangalia baadhi ya ndugu na dada zake. Ana Ndugu na Dada 24, alianza shule akiwa na umri wa miaka 6 na alikuwa akikimbia kilomita 10 kwenda na kurudi shuleni. Alijua ana kipaji cha ukimbiaji akiwa shuleni akishiriki katika mbio za mita 800 na 1500 na wanafunzi amboa wengine walikuwa wakimshinda kwa umri.

Kutokana na hayo alianza ukimbiaji lakini bila usaidizi wa mtu yeyote, Mwaka 1994 na 1998 alishinda mbio za Goodwill zaidi ya mita 10,00 bila viatu. Kwa umbali huo huo alishinda medali ya shaba katika mashindano ya Dunia ya IAAF mwaka 1995 na 1998.

Mwaka wa 2006 alitajwa na katibu wa umoja wa mataifa wakati ule Koffi Annan kama balozi wa michezo wa umoja wa mataifa pamoja na Roger Federer bingwa wa Tennis kutoka Uswisi.

UKWELI KUHUSU WANAWAKE

Mwanamke huhitaji kulia na hawezi kufanya hivyo kama hakuna wa kumsikia na kumtuliza.

Mwnawamke hutishika sana na swala la uzito wake kimwili.Kila wakati lazima ajiangalie ameongeza au amepunguza.

Mwanamke hupenda kutengeneza nywele zake vilivyo kabla kulala.

Wanawake hupenda kupiga ngumzo ingawaje wanachozungumzia kinaweza kuwa hakina maana yeyote.

Wanawake daima huuliza maswali yasiyokuwa na majibu sahihi kwa jitihada za kumfanya mtu kupata hisia za hatia moyoni mwake.

Mwanamke ni mtu ambaye anapenda kufanya shopping ama vitu ukipenda hususan rejareja.

Mwanamke ni mtu anaye chukia mende (KOMBAMWIKO) .

Mwanamke ni mtu asiyeweza kukosa kujibu simu.

Wednesday, 7 March 2012

UKWELI BARANI



Ishara ama alama za samaki hutumika kama njia za kuwafukuza pepo ama mashetani huko Tunisia. Majumba mapya yana mifupa ya samaki ama mkia wa samaki yanapojengwa, na magari pia yana michoro ya samaki ili kuwapa usalama wanaosafiri.

VITUKO



Msichana mwenye umri wa mika 12 amechaguliwa kwenye bodi ya halmashauri ya shule anayosomea.

David Rudisha



David Lekuta Rudisha alizaliwa Decemba 17 1988 ni mkimbiaji wa Kenya na ana rekodi ya dunia katika mbio za mita 800 kwa muda wa 1:41.01. Rudisha pia anashikilia rekodi nne za mbio kumi bora ulimwenguni.
Kazaliwa katika Kovai Wilaya ya Transs Mara, alipata elimu yake katika shule ya upili ya Mtakatifu Francis Kimuron huko Iten Wilaya ya Keiyo, ambayo pia imekuza na kuwalea wakimbiaji kadhaa. Awali alikuwa mkimbiaji wa mita 400 lakini kocha wake alimsababisha kujaribu mita 800.
Mwaka wa 2006 akawa bingwa wa dunia katika kitengo cha junior cha umbali huo.

Rudisha alishiriki katika mbio za 2009 World friidrott, na kufikia mita 800 nusu fainali. Septemba 2009, Rudisha alishinda mbio za IAAF Grand Prix huko Italia na kuweka rekodi mpya ya Afrika kwa muda wa 1:42.01. na kuvunjilia mbali rekodi ya miaka 25 ya muda wa 1:42.28 iliyowekwa na Sammy Koskei.Juhudi zake zikamweka katika nafasi ya nne katika orodha ya muda wote. Katika mbio za IAAF Diamond League mwaka wa 2010 alishinda na kutupilia mbali rekodi ya hapo awali iliyokuwa imeshikiliwa na Sebastian Coe kwa miaka 31 kwa muda wa 1:42.04 na kumweka katika orodha nyingine ya watu kumi bora katika mbio za mita 800. Tarehe 10 July 2010, Rudisha alishiriki katika KBC Night of Athletics huko Ubelgiji katika mbio za mita 800 na kuweka rekodi nyingine mpya ya 1:41.51 na kumweka nambari mbili duniani kwenye mbio hizo.

Rudisha sasa anashikilia rekodi ya dunia kwenye mbio mita 800 alivunja rekodi ya hapo awali iliyokuwa imewekwa mwka wa 2007 kwenye mbio za ISTAF IAAF World Challenge huko Berlin Agosti 22 2010 kwa muda wa 1:41.09. Rekodi ya hapo awali ikishikiliwa na mzaliwa wa Kenya lakini hivi sasa ni raiya wa Denmark Wilson Kipketer. Rudisha alivunja rekodi hiyo kwa sekunde 0.02.
Novemba 2010 akiwa na umri wa miaka 21 alikuwa mkimbiaji mchanga duniani kuwahi kushinda tuzo la mkimbiaji bora Duniani la IAAF, alishinda pia mwanaspoti bora wa mwaka Kenya.
Rudisha ni mwanachama wa kabila la wamaasai, babake Daniel Rudisha mkimbiaji mstaafu aliyeshinda nishani ya fedha katika mbio za Olympiki mwaka 1968 katika mbio za rely za 4 x400 wakati mamake ni mstaafu wa mbio za mita 400.

Amemuowa Lizzy Naanyu na wana binti mmoja.

KIZZA BESIGYE

Besigye, ambaye alikuwa wa pili katika familia ya watu 6, alianza masomo yake katika shule za msingi za Kinyasano na Mbarara. Alipoteza wazazi wake akiwa bado katika shule ya msingi. Alipata masomo yake ya sikondari katika shule za sekomdari za Kitante na Kiyezi, kisha akajiunga na chuo kikuu cha Makerere na akaweza kusomea udaktari.
Alihitimu masomo yake na kupata shahada ya udaktari karika mwaka wa 1980.
Baada ya kuwacha kazi kaika hospitali ya Aga Khan iliyoko Nairobi nchini kenya, alifanya mazoezi ya kigeshi mwaka wa 1980-1986 na kujiunga na kundi la jeshi la National Resistance Army.
Katika mwaka wa 1986, alichaguliwa kuwa waziri wa Mambo ya Ndani na aliyekuwa rais wa Uganda kwa wakati huo,ambaye bado ni rais wa Uganda kwa wakati huu, Yoweri Museveni. Kisha akachaguliwa kuwa waziri wa Nchi katika ofisi ya rais.
Katika mwaka wa 1991, akawa afisa mkuu wa kikosi cha kisasa katika Masaka na katika mwaka wa 1993, akawa Mkuu wa Vifaa na Uhandisi.
Katika mwaka wa 1998, Besigye alimwoa Winnie Byanyima, ambaye alikuwa mbunge wa Manispaa ya Mbarara na mwanamke mhandisi wa kwanza nchini Uganda, na wakajaliwa na mtoto wa kiume kwa jina Anselm Besigye.
Katika uchaguzi wa rais mwaka wa 2001, Besigye alikuwa miongoni mwa waliowania kiti cha urais na kwa bahati mbaya, hakufaulu katika huo uchaguzi na Museveni akaibuka kuwa mshindi na akachaguliwa kuwa rais wa Uganda.
Katika tarehe 23 mwezi Marchi mwaka 2001, Besigye alipinga matokeo ya huo uchaguzi katika Mahakama Kuu ya Uganda, akitoa mfano wa wizi mkubwa na ghasia za uchaguzi na Museveni lakini hakufaulu.
Besigye alikamatwa na kutiwa mbaloni na askari katika tarehe 30 mwezi Juni mwaka 2001, kwa kuhutumiwa kuwa na kosa la uhaini.
Alikimbilia ulaya katika mwezi wa Septemba ili kuokoa maisha yake yaliyokuwa hatarini.
Katika mwaka wa 2005 tarehe 26 mwezi Oktomba, Besigye alirudi nyumbani kutoka Afrika Kusini alikokuwa akiishi.
Katika uchaguzi mkuu uliofanyka mwaka wa 2006, Besigye kwa mara ya pili aliwania kiti cha rais na kutofanikiwa. Museveni alipata kura za asilimia 59 ilhali Besigye alipata kura za asilimia 37.
Besigye alipoteza kura kwa mara ya tatu katika uchaguzi wa 2011 ambao Yoweri Museveni bado aliibuka kuwa mshindi.
Katika tarehe 28 mwezi Aprili, Besigye alikamatwa na polisi baada ya kuanzisha maandamano dhidi ya bei ghali za chakula na mafuta.

















Tuesday, 6 March 2012

MICHAEL DEMITRI SHALHOUB



Mwigizaji katika sinema ya Lawrence of Arabia mwaka 1962,alizaliwa tarehe 10 mwezi Afril mwaka 1932 huko Alexandria nchini Misri.
Alipata elimu yake katika chuo cha Victoria huko Alexandria na kisha kusomea shahada ya hisabati na fizikia katika chuo kikuu cha Cairo.
Baada ya kuhitimu masomo yake, alijiunga na biashara ya familia.
Kabla ya kutoa filamu debut kwa lugha ya kiingereza, tayari alikuwa amenawiri nchini Misri na pia kimataifa.
Mwaka 1953, alikutana na muigizaji wa kike maarufu nchini Misri, Faten Hamama na hilo lilimlazimu kubadili dini na hapo ndipo alipojipatia jina Omar-al-Sharif.
Je wajua hata baada ya Sharif kubadili dini ili amuoe Faten Hamama walijaaliwa na mtoto mmoja na kutalakiana 1974.
Mwaka 2003 Augosti, alifungwa mwezi mmoja jela kwa kosa la kumpiga afisa wa polisi katika kilabu cha casino-Subburbar Paris mwezi Julai. Na kama haitoshi aliamuriwa kulipa faini ya shillingi 141,697.70 pesa za Kenya na kumlipa polisi elfu 28,339.54-pesa za Kenya.