Pages

Wednesday, 14 March 2012

Charity Ngilu



Charity Ngilu Kaluki alizaliwa 1952, ni mwanasiasa kutoka Kenya. Alikuwa waziri wa Afya kutoka 2003 hadi 2007 na aliteuliwa waziri wa Maji Aprili 2008.

Alizaliwa kule mbooni wilayani Makueni 1952, alipata elimu yake kwenye shule ya upili ya Alliance High School, kisha alifanya kazi kama karani wa wa benki ya Central ya Kenya kabla ya kuanzisha biashara yake.

Katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi hapa nchini mwaka1992 aliwashangaza wengi kwa kupita kura za Kitui ya kati katika chama cha Democratic Paty.

Uchaguzi wa Desemba 1997 aliwania urais pamoja na Wangari Maathai wanawake wa kwanza kuwania urais nchini, wakati huo akiwa kwa chama cha Social Democratic Party na alimaliza wa tano.

Baadaye alijiunga na chama cha National Party of Kenya. Uchaguzi wa 2002 chama chake kilikuwa miongoni mwa vyama vilivyo tengeneza NARC muungano huo wa NARC ulishinda uchaguzi huo na Mwai Kibaki alimteuwa waziri wa Afya Januari 3 2003.

Julai 31 2007 Ngilu alimpeleka Ann Njogu mwandamaji hospitalini baada ya kupigwa na polisi, kisha alihutumiwa na kukashifiwa kwa madai ya kumtorosha Njogu polisini, alikamatwa na kufungwa Agosti 12 na kisha kutoka kwa thamani.

Oktoba 5,2007 ngilu alitangaza kujiunga na ODM na mwaniaji urais wa chama hicho Raila Odinga katika kura za 2007 na alimlinganisha Bw Odinga na Bw Nelson Mandela.

Bwanake Micheal Mwendwa Ngilu aliaga Julai mosi, 2006 Afrika Kusini na ana watoto watatu.

No comments:

Post a Comment