
Mwigizaji katika sinema ya Lawrence of Arabia mwaka 1962,alizaliwa tarehe 10 mwezi Afril mwaka 1932 huko Alexandria nchini Misri.
Alipata elimu yake katika chuo cha Victoria huko Alexandria na kisha kusomea shahada ya hisabati na fizikia katika chuo kikuu cha Cairo.
Baada ya kuhitimu masomo yake, alijiunga na biashara ya familia.
Kabla ya kutoa filamu debut kwa lugha ya kiingereza, tayari alikuwa amenawiri nchini Misri na pia kimataifa.
Mwaka 1953, alikutana na muigizaji wa kike maarufu nchini Misri, Faten Hamama na hilo lilimlazimu kubadili dini na hapo ndipo alipojipatia jina Omar-al-Sharif.
Je wajua hata baada ya Sharif kubadili dini ili amuoe Faten Hamama walijaaliwa na mtoto mmoja na kutalakiana 1974.
Mwaka 2003 Augosti, alifungwa mwezi mmoja jela kwa kosa la kumpiga afisa wa polisi katika kilabu cha casino-Subburbar Paris mwezi Julai. Na kama haitoshi aliamuriwa kulipa faini ya shillingi 141,697.70 pesa za Kenya na kumlipa polisi elfu 28,339.54-pesa za Kenya.
No comments:
Post a Comment