![]() |
Dibaba |
Pia
anajulikana kama Tirunesh Dibaba Kenene alizaliwa Oktoba 1 1985 huko
Bekoji, Arsi Uhabeshini (Ethiopia). Ni mwanariadha wa masafa marefu.
Kwa sasa Ndiye bingwa wa Olompiki kwa mbio za mita 5000 na mita
10,000, amepewa jina la utani 'Baby Faced Destroyer'.
Alizaliwa
katika kijiji cha Bekoji, Dibaba ni mtoto wa 4 kwa watoto 6. Alianza
riadha akiwa na umri wa miaka 14, na alihamia mji mkuu wa Addis Ababa
mwaka 2000.
Dibaba
anatoka kwa familia ya wanariadha dada zake na ndugu zake pia wakiwa
kwenye nyanja hiyo ya riadha.
Dibaba
amepata mafanikio makubwa katika michuano ya dunia matukio ya riadha
ya 2003,2006 na 2007.
Aliweka
upya rekodi ya dunia katika mbio za mita 5000 kwa muda wa 14:11.15
katika mkutano wa Oslo Golden League mwaka 2008.

Wiki
moja baadaye akashinda mbio za mita 5000 Agosti 22 2008.
Dibaba
ameolewa kwa mshindi wa mbio za Olimpiki wa mwaka wa 2004 na 2008
Sileshi Sihine.
No comments:
Post a Comment