Pages

Wednesday, 7 March 2012

KIZZA BESIGYE

Besigye, ambaye alikuwa wa pili katika familia ya watu 6, alianza masomo yake katika shule za msingi za Kinyasano na Mbarara. Alipoteza wazazi wake akiwa bado katika shule ya msingi. Alipata masomo yake ya sikondari katika shule za sekomdari za Kitante na Kiyezi, kisha akajiunga na chuo kikuu cha Makerere na akaweza kusomea udaktari.
Alihitimu masomo yake na kupata shahada ya udaktari karika mwaka wa 1980.
Baada ya kuwacha kazi kaika hospitali ya Aga Khan iliyoko Nairobi nchini kenya, alifanya mazoezi ya kigeshi mwaka wa 1980-1986 na kujiunga na kundi la jeshi la National Resistance Army.
Katika mwaka wa 1986, alichaguliwa kuwa waziri wa Mambo ya Ndani na aliyekuwa rais wa Uganda kwa wakati huo,ambaye bado ni rais wa Uganda kwa wakati huu, Yoweri Museveni. Kisha akachaguliwa kuwa waziri wa Nchi katika ofisi ya rais.
Katika mwaka wa 1991, akawa afisa mkuu wa kikosi cha kisasa katika Masaka na katika mwaka wa 1993, akawa Mkuu wa Vifaa na Uhandisi.
Katika mwaka wa 1998, Besigye alimwoa Winnie Byanyima, ambaye alikuwa mbunge wa Manispaa ya Mbarara na mwanamke mhandisi wa kwanza nchini Uganda, na wakajaliwa na mtoto wa kiume kwa jina Anselm Besigye.
Katika uchaguzi wa rais mwaka wa 2001, Besigye alikuwa miongoni mwa waliowania kiti cha urais na kwa bahati mbaya, hakufaulu katika huo uchaguzi na Museveni akaibuka kuwa mshindi na akachaguliwa kuwa rais wa Uganda.
Katika tarehe 23 mwezi Marchi mwaka 2001, Besigye alipinga matokeo ya huo uchaguzi katika Mahakama Kuu ya Uganda, akitoa mfano wa wizi mkubwa na ghasia za uchaguzi na Museveni lakini hakufaulu.
Besigye alikamatwa na kutiwa mbaloni na askari katika tarehe 30 mwezi Juni mwaka 2001, kwa kuhutumiwa kuwa na kosa la uhaini.
Alikimbilia ulaya katika mwezi wa Septemba ili kuokoa maisha yake yaliyokuwa hatarini.
Katika mwaka wa 2005 tarehe 26 mwezi Oktomba, Besigye alirudi nyumbani kutoka Afrika Kusini alikokuwa akiishi.
Katika uchaguzi mkuu uliofanyka mwaka wa 2006, Besigye kwa mara ya pili aliwania kiti cha rais na kutofanikiwa. Museveni alipata kura za asilimia 59 ilhali Besigye alipata kura za asilimia 37.
Besigye alipoteza kura kwa mara ya tatu katika uchaguzi wa 2011 ambao Yoweri Museveni bado aliibuka kuwa mshindi.
Katika tarehe 28 mwezi Aprili, Besigye alikamatwa na polisi baada ya kuanzisha maandamano dhidi ya bei ghali za chakula na mafuta.

















No comments:

Post a Comment