Ni
mwandishi, Nesi, Mwandishi wa habari, Mwanasiasa na Mwanadiplomasia
kutoka Kenya.
Alipozaliwa
alipewa jina la Grace Emily Akinyi katika sehemu wilayani Asembo,
katika mkoa wa Nyanza. Alisomea mafunzo yake ya nesi nchini Uganda na
Uingereza. Alifanya kazi kama mkunga, kama mwalimu, kama mwandishi wa
habari, kama mtangazaji wa huduma ya ng'ambo ya BBC, na katika cheo
cha usimamizi katika kampuni ya Air India Corporation ya Afrika
Mashariki. Mwaka wa 1984 akawa moja wa wanawake wachache kuhudumu
kama mbunge na mwanamke wa kipekee aliyehudumu ka naibu Waziri katika
Baraza la Mawaziri la Rais Daniel arap Moi.
Tangu
wakati huo ameshikilia nyadhifa mbalimbali za ubalozi kwani
amewakilisha nchi yake katika Umoja wa Mataifa na UNESCO. Alikuwa
mwanachama mwanzilishi wa shirika la Waandishi wa Kenya maarufu kwa
Kiingereza kama Writers' Association of Kenya.
Grace
Ogot aliyezaliwa 1934 alifunga ndoa na mwanahistoria Profesa Bethwell
Allan Ogot, kutoka sehemu ya Gem, mnamo mwaka wa 1959 na ni mama wa
watoto wanne.
Kitabu
chake cha kwanza kilikuwa Land Without Thunder kitabu cha hadithi
fupi. Riwaya yake ya kwanza ilikuwa The Promised Land.
Grace
Ogot anaweza kusemekana kuwa mmoja ya waandishi bora zaidi barani
Afrika. Mtindo wake wa uandishi
wake ni wa kuvutia sana hasa katika ubunifu wake wa wazi; yeye huweza
kuonyesha Utabibu wa mila na tamaduni ya Kiafrika, yanayofuata njia
mwafaka na ishara.
No comments:
Post a Comment