Pages

Thursday, 8 March 2012

TEKLA LORUPE CHEPKITE



Alizaliwa Mei 9 1973 katika Kutomwony Kenya, ni mkimbiaji wa mbio za masafa marefu na msemaji wa kimataifa kwa ajili ya amani, haki za wanawake na elimu.
Lorupe anashikilia rekodi ya dunia kwa kilomita 20,25 na 30 na hapo awali alishikilia rekodi ya marathon duniani. Ni bingwa wa wa marathon duniani na alikuwa mwanamke mwafrika wa kwanza kushinda mbio za marathon za New York ambazo ameshinda mara mbili.Ameshinda marathon katika miji kama London, Boston, Hong Kong, Berlin, Rome na nchi nyingine nyingi.

Utotoni mwake alikuwa akienda shambani, akichunga ngombe na kuwaangalia baadhi ya ndugu na dada zake. Ana Ndugu na Dada 24, alianza shule akiwa na umri wa miaka 6 na alikuwa akikimbia kilomita 10 kwenda na kurudi shuleni. Alijua ana kipaji cha ukimbiaji akiwa shuleni akishiriki katika mbio za mita 800 na 1500 na wanafunzi amboa wengine walikuwa wakimshinda kwa umri.

Kutokana na hayo alianza ukimbiaji lakini bila usaidizi wa mtu yeyote, Mwaka 1994 na 1998 alishinda mbio za Goodwill zaidi ya mita 10,00 bila viatu. Kwa umbali huo huo alishinda medali ya shaba katika mashindano ya Dunia ya IAAF mwaka 1995 na 1998.

Mwaka wa 2006 alitajwa na katibu wa umoja wa mataifa wakati ule Koffi Annan kama balozi wa michezo wa umoja wa mataifa pamoja na Roger Federer bingwa wa Tennis kutoka Uswisi.

No comments:

Post a Comment