David
Lekuta Rudisha alizaliwa Decemba 17 1988 ni mkimbiaji wa Kenya na ana
rekodi ya dunia katika mbio za mita 800 kwa muda wa 1:41.01. Rudisha
pia anashikilia rekodi nne za mbio kumi bora ulimwenguni.
Kazaliwa
katika Kovai Wilaya ya Transs Mara, alipata elimu yake katika shule
ya upili ya Mtakatifu Francis Kimuron huko Iten Wilaya ya Keiyo,
ambayo pia imekuza na kuwalea wakimbiaji kadhaa. Awali alikuwa
mkimbiaji wa mita 400 lakini kocha wake alimsababisha kujaribu mita
800.
Mwaka
wa 2006 akawa bingwa wa dunia katika kitengo cha junior cha umbali
huo.

Rudisha
sasa anashikilia rekodi ya dunia kwenye mbio mita 800 alivunja rekodi
ya hapo awali iliyokuwa imewekwa mwka wa 2007 kwenye mbio za ISTAF
IAAF World Challenge huko Berlin Agosti 22 2010 kwa muda wa 1:41.09.
Rekodi ya hapo awali ikishikiliwa na mzaliwa wa Kenya lakini hivi
sasa ni raiya wa Denmark Wilson Kipketer. Rudisha alivunja rekodi
hiyo kwa sekunde 0.02.
Novemba
2010 akiwa na umri wa miaka 21 alikuwa mkimbiaji mchanga duniani
kuwahi kushinda tuzo la mkimbiaji bora Duniani la IAAF, alishinda
pia mwanaspoti bora wa mwaka Kenya.
Rudisha
ni mwanachama wa kabila la wamaasai, babake Daniel Rudisha mkimbiaji
mstaafu aliyeshinda nishani ya fedha katika mbio za Olympiki mwaka
1968 katika mbio za rely za 4 x400 wakati mamake ni mstaafu wa mbio
za mita 400.
Amemuowa
Lizzy Naanyu na wana binti mmoja.
No comments:
Post a Comment