Pages

Tuesday, 13 March 2012

Martha Karua.



Martha Wangari Karua alizaliwa 22 Septemba 1957, ni mwanasiasa kutoka Kenya na pia ni mbunge wa Gichugu na wakili wa mahakama kuu ya Kenya. Alikuwa waziri wa Sheria lakini alijiuzuli mnamo Aprili 2009.



Karua alizaliwa katika Wilaya ya Kirinyaga, Mkoa wa Kati wa Kenya, yeye ni wa pili katika familia ya watoto nane, wasichana wanne na wavulana wanne. Alisomea sheria katika Chuo Kikuu cha Nairobi 1977-1980. Kati ya mwaka 1980 na 1981 alijiunga na shule ya sheria Kenya School of Law, baada ya hapo alijiunga na utumishi wa umma na kufanya kazi na kufanya kazi kama hakimu kutoka 1981 – 1987. Kutoka 1987 – 2002 alifanya kazi katika mazoezi binafsi kama mtetezi.

Alifanya kazi katika mahakama ya hakimu wilayani na kupanda ngazi hadi Hakimu mkazi Mwandamizi hadi alipotoka 1987. Katika kipindi hiki, alikuwa alikuwa msimamizi wa mahakama za sheria Makadara 1984 – 1985 na Mahakama za Kibera 1986 – 1987.

Yeye alichangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya sheria ya familia na hasa ugawaji wa mali ya ndoa pamoja na sheria ya kikatiba na utawala.

Kutoka mwaka wa 1990 – 2002 alikuwa mwanachama wa harakati za upinzani wa kisiasa ambao walipigania demokrasia ya vyama vingi nchini Kenya katika miaka ya 1990 wakati Kenya ilikuwa chini ya utawala wa Daniel Moi.
Alikuwa mmoja wa waliotengeneza chama cha NARC kilichoshinda kura za 2003 na kumaliza miongo minee ya utawala wa KANU.
Alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa NARC Novemba 15 2008.
Alikuwa waziri wa kwanza kujiuzulu kwa hiyari yake tangu 2003.

No comments:

Post a Comment