Pages

Monday, 27 February 2012

VITUKO



Mwanamke mmjo ameshangazwa sana alipofungua fridge yake na kupata bata aliyechinjwa na bwanake na kumweka kwenye fridge bado yungali hai.

UKWELI BARANI AFRIKA



Jangwa la Sahara ndilo jangwa kubwa na lenye joto ulimwenguni.

Kipchoge Keino


Kipchoge ("Kip") Keino ni Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Kenya na mkimbiaji aliyestaafu akiwa na ushindi wa medali za dhahabu mara mbili kwenye Mashindano ya Olimpiki. Alizaliwa Januari 17, 1940 huko Kipsamo, Wilaya ya Nandi, Kenya.Wazazi wake wote walifariki akiwa changa na kukuzwa na shanagazi.
Alianza kuonyesha ufundi wake wa kukimbia kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola huko Perth, Australia alipochukua nafasi ya kumi na moja. Kwenye Mashindano ya Olimpiki ya Majira ya Joto mwaka 1964 alimaliza wa tano kwenye mbio za mita 5000.
Agosti 27, 1965, Keino alivunja rekodi ya dunia ya mita 3000 kwa sekunde sita. Katika Mashindano ya Mataifa ya Afrika alishinda medali mbili za dhahabu kwa umbali wa mita 1500 na 5000. Baadaye alikuja kuvunja rekodi ya dunia iliyokuwa ikishikiliwa na Ron Clarke ya mita 5000 kwa kukimbia kwa muda wa 13:24:2.
JE WAJUA
Aliwahi cheza mchezo wa raga.
Alijiunga na Kenya Police baada ya skuli.

Friday, 24 February 2012

VITUKO



Yaya amshambulia mwajiri wake kwa makonde na makofi, kwa sababu alipewa Uji anywe huku mwajiri na wanawe wakinywa Chai kwa Vitafuno. Kutokana na Yaya alisema afadhali aiishi njaa kuliko kunywa Uji ilhali anaishi mjini. Baada ya mwajiri wake kwenda kazini alikunywa Chai ya Mtoto na kujipikia chapati kumi na kuzila moja kwa moja.

Ngũgĩ wa Thiong'o


Alizaliwa Januari 5 1938, Kamirithu karibu na Limuru katika Kaunti ya Kiambu, alibatizwa James Ngugi.Ni mwandishi wa Kenya hapo zamani aliandika kwa Kiingereza lakini sasa anaandika kwa lugha ya Gikuyu. Kazi yake ni pamoja na Riwaya, Michezo, Hadithi fupi na Insha, pia yeye ni mwanzilishili na mhariri wa jarida la ligha ya Gikuyu, Mutiiri.

Alipata Elimu katika shule za Kamandura, Manguu na Kinyogori na kisha kuelekea katika shule ya Upili ya Alliance High School zote toka Kenya, baada ya hapo alizidisha masomo yake kwenye Chuo Kikuu cha Makerere huko Uganda na Chuo Kikuu cha Leeds huko Uiingereza.

Ngugi ni mpokeaji wa Udakitari za Heshima saba kutoka vyuo vikuu tofauti tofauti.
Riwaya yake ya kwanza Weep Not Child kilichochapishwa 1964, alikiandika akiwa Katika Chuo Kikuu cha Leeds huko Uiingereza, na kumfanya kuwa mwafrika wa kwanza kutoka Afrika Mashiriki kuchapisha katika Lugha ya Kiingereza.

Mwaka wa 1967 baada ya kuchapisha riwaya yake Agrain of Wheat aliwacha kuandika kwa Kiingereza akaacha pia Ukisto na kumfanya kubadilisha Jina lake James Ngungi hadi Ngugi wa Thiongo na akaanza kuandika katika asili yake ya Gikuyu na Kiswahili. Mwaka wa 1977alichapisha mchezo Ngaahika Ndeenda yani ( I will Marry When I want) ambacho kilimkasirisha makamu wa Rais wakiti ule Daniel Arap Moi alipoamuru kufungwa. Ali[pokuwa kizuizini katika gereza la Kamiti Maximum aliandika riwaya ya kwanza ya Kisasa katika Gikuyu Caitaani Mutharaba yaani (Devil on the Cross) kwenye karatasi gushi.
Baada ya kutoka kwake hakurejeshewa kazi yake kama profesa katika Chuo Kikuu cha Nairobi, na familia yake ilikuwa inasumbuliwa kutokana na maadishi yake kuhusu kukosekana kwa haki na serikali ya kidikteta hata hivyo kulazimika kuishi uhamishoni. Alirudi baada ya miaka 22 wakati Moi alitoka Ofisini.

Tarehe 8 Agosti 2004 Ngugi alirejea Kenya kama ziara ya kuzuru Afrika Mashariki.Agosti 11, majambazi waliingia nyumbani kwake na kudhulumiwa pamoja na mke wake, na kuiba fedha na kompyuta jambo ambalo lilimfanya arudi Marekani hadi sasa.

Amechapisha riwaya, michezo,na hadithi fupi zaidi ya 30.

UKWELI BARANI AFRIKA



Je wajua Vita vya Pili vya Congo vilivyoanza 1998 na vilihusisha Nchi nane za Afrika ndivyo vita vikubwa katika historia ya Afrika. Wastani watu milioni 5.4 walifariki kutokana na vita hivyo na kuwa vita ambavyo watu wengi walifariki tangu vita vikuu vya dunia vya II. Vita hivi vilikamilika mwaka 2006 lakini uadui bado unaendelea hadi leo.

VITUKO



Yaya amshambulia mwajiri wake kwa makonde na makofi, kwa sababu alipewa Uji anywe huku mwajiri na wanawe wakinywa Chai kwa Vitafuno. Kutokana na Yaya alisema afadhali aiishi njaa kuliko kunywa Uji ilhali anaishi mjini. Baada ya mwajiri wake kwenda kazini alikunywa Chai ya Mtoto na kujipikia chapati kumi na kuzila moja kwa moja.

Thursday, 23 February 2012

UKWELI BARANI AFRIKA



Je wajua kwamba Liberia na Uhabeshi (Ethiopia) ndizo Nchi za peke barani Afrika ambazo hazikuwania uhuru wake maanake wakoloni hakufika huko.

VITUKO



Polisi wa trafiki wameshtuka na kuwachwa vinywa wazii ambapo walimuona dereva asiyekuwa na mguu mmoja na bila mikono.
Jamma huyo mwenye umri wa miaka 40 alijifunza kuendesha gari baada ya operesheni mara tatu alikimbizana na polisi kwa dakika kumi bila kushikwa na akawawacha.Kabla ya hayo siku tatu zilizopita alikimbizana na polisi kwa kilomita 120 na kuwashinda.

Wole Soyinka


Akinwande Oluwole au "Wole" Soyinka ni mwandishi Mnageria .Wengi wanamwona kama mwandishi bora wa michezo ya kuigiziwa Afrika. Ni mwandishi na mtungi wa Mashairi na pia michezo ya kuigiza.
Alizaliwa tar. Julai 13, 1934 kwa wazazi Wayoruba huko Abeokuta, Nigeria. Alisoma shule ya msingi kwao Abeokuta halafu shule ya sekondari ya Ibadan,kisha akasomea fasihi kwenye Chuohicho cha Ibadan (1952-1954) na Leeds (Uingereza) 1954-1957.
Alifundisha fasihi kwenye vyuo vikuu vya Lagos, Ibadan, na Ife.
Soyinka aligongana mara nyingi na serikali za kidikteta za nchi yake akipinga pia udikteta katika nchi mbalimbali kama vile utawala wa Mugabe huko Zimbabwe.
Hasa wakati wa udikteta wa jenerali Sami Abacha (1993-1998) Soyinka alijikuta hatarini. Akaondoka Nigeria akaishi nje alipopata kuwa profesa wa fasihi kwenye Chuo Kikuu cha Emory (Atlanta - Marekani).
Februari 6 2012 Soyinka alisema kwamba yuko miongoni mwa watu maarufu na mashuhuri wanaolengwa kuuwawa na kundi la Boko Haram.
Baada ya mwisho wa utawala wa kijeshi mwaka 1999 Soyinka alikubali nafasi kwenye chuo kikuu cha Ife kwa masharti ya kwamba mwanajeshi mstaafu hatakuwa kamwe chansela wa chuo kikuu kile.
Mwaka 2005 Soyinka akawa profesa kwenye chuo kikuu cha Nevada, Marekani.
Wole Soyinka amemwoa mke wake Laide wana watoto wanne. Aliwahi kuwa na watoto wawili kabla ya kuoa.
JE WAJUA
Ni Mshindi wa kwanza Mwafrika kupewa Tuzo ya Nobel ya fasihi (mwaka wa 1986)
Mwaka 1994 aliteuliwa kuwa balozi wa nia njema kwa{UNESCO}Umoja wa Mataifa la Elimu,Sayansi,na Utamaduni kwa ajili ya kukuza Utamaduni wa Kiafrika, haki za binadamu, Uhuru wa Kujieleza, Vyombo vya habari na mawasiliano.
Ameandika zaidi ya michezo 20.

Wednesday, 22 February 2012

VITUKO



Mtu alilazimishwa akiwa ameshikiwa bastola kupeleka majambazi nyumbani kwake, ambapo aliwekewa supper glue kwenye baiskeli yake ya mazoezi na kulazimishwa kuvua nguo zake zote na kuketi hapo, kisha nyumba yake kuporwa.
Msemaji wa huduma za dharura alisema jamaa huyo aliwekewa super glue kwenye mikono, miguu na pia midomo yake.
Jamaa huyo mwenye umri wa miaka 50 aliokolewa masaa matatu baadaye wakati mpenzi wake alifika nyumbani.

Ali Mazrui


Ali Mazrui Al'amin alizaliwa Februari 1933 huko Mombasa Kenya, ni mwandishi wa Kisiasa kuhusu Afrika na masomo ya kiislamu.Yeye ni Profesa wa Albert Schweitzer na mkurugenzi wa Taasisi ya Utamaduni ya Global katika Chuo Kikuu cha Binghamton huko Binghaton, New York.
Mazrui alisomea katika shule za Mombasa, nchini Kenya, alipata B.A yake kutoka Chuo Kikuu cha Manchester nchini Uingereza mwaka 1960 na M.A yake kutoka Chuo Kikuu cha Columbia huko New York mwaka 1961, na Shahada ya Udaktari (Dph ) kutoka Chuo Kikuu cha Oxford mwaka 1966.
Baada ya kukamilisha elimu yake katika Chuo kikuu cha Oxford, Mazrui alijiunga na chuo kikuu cha Makerere( kampala Uganda) ambapo aliwahi kuwa mkuu wa Idara ya Sayansi ya Siasana Mkuu wa Kitivo cha Sayansi ya Jamii. Mwaka wa 1973 alilazimika kwenda uhamishoni na Idi Amin.Mwaka 1974 alijiunga na kitivo cha Chuo kikuu cha Michigan kama Profesa na baadaye aliteuliwa Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo ya Afroamerican na Afrika (1978-1989).
Utafiti na maslahi yake ni pamoja siasa za Afrika, Utamaduni wa siasa za kimataifa, Uislamu wa Kisiasa na Uhusiano wa Kaskazini na Kusini, ni mwandishi wa vitabu zaidi ya ishirini.
JE WAJUA
Mbali na uteuzi wake kama profesa wa Albert Schweitzer katika sayansi ya siasa, mafunzo ya Afrika, filosofia, Ufafanuzi na Utamaduni Mkurugenzi wa Taasisi ya Utamaduni ya Global, Mazrui pia ana nyadhifa zingine tatu katika chuo kiku cha Jos nchini Nigeria,na chuo kikuu cha Cornell huko New York na pia ni kansela wa Jomo Kenyatta chuo kikuu cha Kilimo na Teknolojia.
Mwaka wa 2005, Mazrui Ali alichaguliwa wa 73 kwenye orodha ya wasomi 100 duniani na gazeti la Prospective la Uingereza na pia la Foreighn Policy la Marekani.
Hivi sasa ana zaidi ya nyadhifa 8 katika nchi tatu.
Pia yeye huchangia mara kwa mara katika magazeti ya Kenya, Uganda na Afrika Kusini.
Ana tuzo zaidi ya kumi kutoka nchi mbalimbali na vyuo Vikuu mbalimbali.

Tuesday, 21 February 2012

Robert Mugabe


Robert Gabriel Mugabe amekuwa kiongozi wa Zimbabwe tangu 1980. Yeye ni mwenyekiti wa chama tawala cha ZANU. 1980 alikuwa waziri mkuu na 1987 Rais wa Zimbabwe. Kabla ya wakati ule aliongoza upinzani wa ZANU dhidi ya serikali ya walowezi Waingereza nchini waliofuata siasa ya ubaguzi wa rangi.
Mugabe alirudiwa katika uchaguzi mbalimbali. Tangu mwaka 2000 uchaguzi hizi zimekuwa mashakani kutokana na matishio na matumizi ya mabavu dhidi ya wapinzani. Utawala wa Mugabe umeitwa wa kidikteta tangu mwaka 2002. Kutokana na mashtaka dhidi ya serikali ya Mugabe ya kudharau haki za binadamu, nchi ya Zimbabwe ilisimamishwa ndani ya Jumuiya ya Madola. Mugabe pamoja na mawaziri wake na viongozi wa chama chake hawaruhusiwi kusafiri kwenda nchi za Umoja wa Ulaya na Marekani.
Mwanzoni mwa utawala wake Mugabe alisifiwa kujenga uchumi na sera ya elimu nchini. Zimbabwe ilikuwa nchi iliyouza vyakula vingi nje. Tangu mwanzo wa milenia mpya pamoja na mashtaki ya udikteta hali ya uchumi ulirudi nyuma. Takriban milioni mbili ya raia wa Zimbabwe wameondoka nchini wakikaa kama wakimbizi Afrika Kusini.


Baada tu ya kushika madaraka, Mugabe aliamua kuimarisha jeshi lake la kumlinda (liitwalo Gukurahundi) ambalo lilijengwa na watu kutoka kabila lake la wa-Shona. Nchi hiyo ilikuwa tayari imegawanyika kikabila hata katika uchaguzi wa kwanza wa 1980, washona wote walimchagua Mugabe na Wa-Ndebele na wabunge kutoka chama cha ZANU. Wakati wandebele walichagua viongozi kutoka chama cha ZAPU kilichoongozwa na Joshua Nkomo.
Mara baada ya uchaguzi tu mwezi Novemba 1980 Mugabe alianza kampeni ya kuua kwa wingi watu wa kabila la wa-Ndebele ambao mji wao mkubwa unaitwa Bulawayo. Ingawa mauaji hayo hayakufikia kiwango cha yale ya Rwanda na Burundi, waliuawa wanawake, wanaume, watoto na hata vichanga vilivyokuwa matumboni. Mwaka 1981 pia Mugabe aliendelea kuua wandebele tukio ambalo halikutangazwa sana na vyombo vya habari. Kuanzia enzi hizo hadi leo raisi Mugabe amejaribu kushinda kila uchaguzi unaokuja nchini huko kwa kutumia nguvu za kikabila na mabavu.
Alizaliwa Februari 21,1924 katika Zvimba Wilaya ya kaskazini magharibi ya Salisbury katika kusini mwa Rhodesia kwa baba wa Malawi Gabriel Matibili na mama kutoka kwa kabila la Shona wote wakatoliki. Yeye ni mtoto wa tatu kwa watotot sita. Alikuwa na na ndugu wawili wakubwa, na mmoja wao, Micheal, alikuwa maarufu sana katika Kijijini. Ndugu wote wawili waliaga dunia alipokuwa mchanga na kumwacha na mdogo wake.Babake ambaye alikuwa seremala aliiacha familia yake mwaka 1934 baada ya kifo cha Micheal alipokuwa akitafuta kazi huko Bulawayo.


Mugabe alikuzwa katika mazingira ya kikatoliki na kusomea vyuo vya kikatoliki kama Marist Brothers na Jesuit. Kulingana na kakake Mugabe alikuwa mpole na rafiki wake mkubwa alikuwa vitabu.
Alihitimu kama mwalimu lakini aliondoka kwenda kusoma katika Fort Hare nchini Afrika Kusini alipokuwa huko alikutana na Julius Nyerere, Herbert Chitempo na Keneth Kaunda. Kisha alienda kusoma Salisbury 1953, Gwelo 1954, na Tanzania 1955-1957. Apo awali alifuzu na Shahada ya Sanaa kutoka chuo kikuu cha Fort Hare mwaka 1951. Mugabe hatimaye alipata digri zaidi ya sita akiwa akisafiri ikiwa ni pamoja na Shahada ya Utawala na shahada ya Elimu kutoka chuo kikuu cha Afrika Kusini na shahada ya Sayansi, shahada ya sheria na zingine nyingi tu zote kutoka chuo kikuu cha London. Digri ya sheria alipata alipokuwa gerezani nayo shahada ya uzamili ya sayansi ya chuma alipata akiwa waziri mkuu.


Baada ya kufuzu, Mugabe alifunza katika Chuo cha Mafunzo cha Chalimbana kilichoko Zambia toka 1955-1958, baada ya hapo amefundisha katika Apowa shule ya Sekondari katika Takoradi,katika mkoa wa magharibi mwa Ghana huko ndiko alikutana na Sally Hayfron ambaye walifunga ndoa mwezi wa Aprili 1961
Mugabe alirudi Kusini mwa Rhodesia na kujiunga na National Democratic Party{NDP} mwaka 1960 wakati wa utawala wa waziri mkuu Ian Smith. Mwaka 1980 Machi 4 Mugabe alishinda kura na kuwa waziri mkuu licha ya kutokana vitisho kutoka pande zote, kutoaminiana kutoka kwa vikosi vya usalama na kupata ripoti ya masanduku ya kura kupatikana kwenye barabara.
Mwaka 1987, nafasi ya Waziri mkuu ilifutiliwa mbalina Mugabe na kuwa Rais mtendaji wa Zimbabwe na kupata nguvu zaidi. Alichaguliwa tena mwaka 1990 na 1996 na mwaka 2002 huku kukiwa na madai ya kuenea kwa wizi wa kura na vitisho
Katika kiaka ya 1980 sera ya Mugabe ya Ujamaa ilionekana kukuza nchi hiyo, mwaka 1980 na 1981 uchumi wa Zimbabwe ulikuwa kwa asilimia 10.65 na 12.5% kutoka asilimia 2.7%. Kutokana na ripoti hiyo kwa mujibu wa Benki ya Dunia 1995 baada ya uhuru Zimbabwe ilitoa kipaumbele katika uwezekaji wa rasilimali na msaada kwa ajili ya kilimo cha wakulima wadogo wadogo.
Hata hivyo jamaa huyu ameshtumiwa kwa na mtazamo wa ubaguzi wa rangi kwa wazungu, pia jamaa huyu amekuwa suluhu katika upinzani wake kwa haki za ushoga.
Uchaguzi ujao ulikuwa ufanyike 2013, lakini umepelekwa mbele hadi 2012 kwa madai kwamba umri wake ni mkubwa licha ya hayo chama chake cha ZANU-PF kimesema kwamba bado atawania urais.
Kwa sasa yeye ndiye rais aliyehudumu kwa mda mrefu barani afrika, mwaka wa 2005 alipelekwa hospitalini kwa kuwa na mshtuko wa moyo jambo ambalo lilipeleka uvumi kwamba amefariki.


Mke wake wa kwanza Sally Hayfron aliaga dunia 1992 kwa shida ya figo mtoto wao wa pekee kijana Micheal Nhamodzenyika Mugabe aliyezaliwa septemba 27 1963 pia aliaga Desemba 26 1966 kutokana kutokana na malaria ya ubongo. Sally ambaye alikuwa pia mshauri mkuu wake wa kisiasa inasemekana kwamba baada ya kifo chake Mugabe alianza kuiongoza Zimbabwe vibaya.
Agosti 17 1996 alimuowa aliyekuwa karani wake Grace Marufu ambaye ni mchanga wake kwa miaka41 na wana watoto wawili naye, yeye tayari alikuwa na mimba ya Mugabe akiwa bado ana mke wake wa kwanza Sally na wakati huo Grace alikuwa kwenye ndoa yake na Stanley Goreraza, sasa mwanadiplomasia nchini Chini.Sasa wana watoto watatu naye.
USICHOJUA KUMHUSU
Anapoadhimisha miaka 88 leo anajulikana sana kwa kutumia pesa za watozwa ushuru kuadhimisha sherehe hizi.
Ndiye rais aliyesoma na ana shahada zaidi ya 16 ulimwenguni
Alifungwa jela miaka 10 kuanzia 1964 kwa kupinga utawala wa wakoloni.
Ndiye rais aliyeongoza kwa mda mrefu barani afrika.

VITUKO



Mwili wa mwanamme mmoja aliyefariki kwa miaka saba umepatikana kwenye chumba chake cha kulala kwenye kitanda chake. Jamaa huyo alikuwa na miaka59 alipofariki na hakuwa na kazi kulingana na habari za polisi.Habari zingine toka kwa polisi zinasema walipata sigara na tv ikiwa wazi.

Monday, 20 February 2012

MJADALA

JE, Wanaume wakisusia chakula toka jumatatu hadi ijuma watapata suluhisho la kupigwa na waume wao

VITUKO

Serikali ya nchi fulani imeingilia kati wakati mwanamke mmoja alijaribu kumuuza mme wake kwenye mtandao.
Katika matangazo yaliyobandikwa kwenye mtandao huo yalisema nauza mme wangu kwa vile nataka fedha. Alimfafanua mme wake kama aliyehitimu na anajua mapenzi aliongoza kwamba ana umri wa miaka 35, na angepewa dhahabu hangekataa.

MASHUJAA

CHINUA ACHEBE
Chinua Achebe Alizaliwa 16th Novemba, 1930. Ni mwandishi kutoka nchi ya Nigeria. Ameandika vitabu vingi vya riwaya, mashairi na insha. Hadithi zake zinatumia mitindo ya fasihi simulizi ya lugha yake ya asili, Kiigbo. Hata hivyo ameandika hasa kwa Kiingereza. Baadhi ya maandiko yake ni;
              i)1958, Things Fall Apart'
             ii)1960, No Longer At Ease"
            iii)1964, Arrow of God"
            iv)1973, Girls at War''
             v)1984, The Trouble with Nigeria''
            vi)1987, Anthills of the Savannah''
           vii)A Man of the People.
Achebe alipata umaarufu sana haswa kwa kitabu chake cha 'Things Fall Apart' alichochapisha 1959, na kitabu kinachosomwa sana barani Afrika wakati huu.
Alifuzu kwanye masomo yake ya sekondari na kupata udhamini kusomea shahada yake ya kwanza. Alipokuwa masomoni hakufurahishwa na Dini za Dunia na tamaduni za jadi za Afrika, na akaanza kuandika hadithi akiwa Chuo Kikuu. Baada ya kunitimu, alifanya kazi kwa huduma ya Utangazaji ya Nigeria na hatimaye Jijini Lagos.
Achebe huuandika riwaya zake kwa lugha ya Kiingereza na amejipata matatani kwa utaumizi wa lugha hii ya Kiingereza,'Lugha ya Wakoloni', katika fasihi ya Kiafrika.
Mtindo wake wa kuandika riwaya zake huzingatia mila na jamii ya Igbo, madhara ya mvuto wa Kikristo na tofauti upande maadili wakati na baada ya ukoloni. Pia amechapisha idadi ya hadithi fupi, vitabu vya watoto, na mkusanyo wa insha. Tangu mwaka wa 2009 amekuwa akifunza Chuo Kikuu cha David and Mirianna Fisher amekuwa pia profesa Mafunzo ya Afrika katika Chuo Kikuu cha Brown katika visiwa vya Rhode huko Marekani.
Achebe alisema kwamba alipokuwa mdogo wazazi wake waliwasimulia hadithi ambazo zilikuwa uti wa mgongo wa utamaduni wa Igbo na sehemu muhimu ya jamii. Alipata elimu yake kutoka kwa babake ambaye alikuwa akufunika paa na kuta za nyumba.
Riwaya yake ya kwaza Things Fall Apart kimekuwa riwaya muhimu katika fasihi ya Afrika, ana imeeuza zaidi ya nakala milioni 8 kote Duniani, pia kimetafsiriwa katika lugha 50 na kumfanya Achebe mwandishi bora wa Afirka ambaye kazi yake imetafsiriwa na kupata mafanikio zaidi alippochapisha kitabu chake cha kwanza.
Katika mwaka huo huo Things Fall Apart kilichapishwa, Achebe alipandishwa cheo hadi NBS na mkuu wa mtandao katika mkoa wa mashariki. Alihamia Enugu na kuanza majukumu yake ya kiutawala, akiwa huko alikutana na mwanamke mmoja aitwaye Christie Okoli, ambaye alikuzwa katika eneo hilo.
Achebe na Okoli wakawa marafiki wa karibu na Septemba 10,1961 wakafunga ndoa katika kanisa la Resurrection. Christie ameielezea ndoa yake kama ndoa ya aminifu na maelewano na wana tatoto tano.
Kitabu chake cha A Man of the People kilitumika hapa Kenya kama Riwaya kwa wanafunzi wa kidato cha nne.














Friday, 17 February 2012

ROGER MILLA



Alizaliwa kama Albert Roger Miller Mooh tarehe 20 Mei 1952 ni mwanasoka mstaafu kutoka Cameroon aliyecheza kama Mshambuliaji. Alikuwa mwafrika wa kwanza ambaye Nyota yake iling'aa katika kandanda kimataifa. Alichezea timu yake ya Camerron mara tatu kwenye Kombe la Dunia.
Alipata mafanikio mengi akiwa na kiaka 38 umri ambao washambulizi wengi hustaafu wakifika. Alifunga mabao manne kwenye Kombe la Dunia mwaka1990, bao lililompa umaarufu na kumfanywa kukumbukwa ni lile wakicheza na Colombia ambapo alionyesha ujuzi na mahanjam yake na kumchenga kipa Rene Higuitana kufunga katika yadi 35 kutoka lango lake na kusaidia Cameroon kufika robo fainali ikawa timu ya kwanza kutoka Afrika kifikia kiwango hicho.

Pia anakumbukwa kwa ishara yake ya kusherehekea bao alipofunga, kwa kukimbia hadi kwenye kibendera cha kona na kuanza kucheza ngoma.
Pele wa Brazil alimtaja miongoni mwa wachezaji 125 waliosifika kwenye mchezo huo ambao bado wanaishi.

Alizaliwa katika mji mkuu wa Yaounde'. Alianza kucheza soka akiwa na miaka 13 kwenye klabu ya Douala na akiwa na miaka 18 alishinda ligi yake ya kwanza. Mwaka wa 1974 alipewa tuzo la mchezaji bora wa Afrika. Mwaka wa 1977 alihamia ulaya na kuchezea klabu ya Valenciennes huko Ufaransa, hata hivyo aliwekwa kwenye timu ya hifadhi miaka miwili. Mwaka wa 1979 alijiunga na AS Monaco lakini bado akajipata palepale kwenye hifadhi,mwaka uliofuatia alijiunga na klabu ya Bastia lakini bado hakustawi, hatimaye akapata umaarufu kwenye klabu ya Saint-Etienne mwaka 1984.

Alichezea timu yake ya Cameroon mara ya kwanza mwaka wa 1978, alikuwa pia miongoni mwa wachezaji wa timu hiyo waliocheza Kombe la Dunia mwaka wa 1982, na bao lake lilikataliwa wakicheza dhidi ya Peru. Miaka miwili baadaye alikuwa katika kikosi cha mashindano ya Michezo ya Olimpiki ya 1984 huko Los Angeles ,California. Alistaafu kutoka soka ya kimataifa mwaka 1987 na kuhamia Reunion katrika Bahari ya Hindi.

Hata hivyo, mwaka 1990, alipokea simu kutoka kwa Rais wa Cameroon wakati ule Paul Biya ambaye alimsihi na kumbembeleza kutoka ustaafuni na kujiunga tena na timu taifa. Alikubali na kwenda Italia na Indomitable Lions kucheza Kombe la Dunia 1990.

Alijitokeza kama mchezaji kama mchezaji mashuhuri kwenye Kombe hilo kwa kufunga mabao manne, mawili kwenye muda wa nyongeza na pia jinsi alivyo yasherehekea mabao hayo yote manne.
Bao lake la pili dhidi ya Colombia mwaka huo ndilo lililokuwa mada kwenye Kombe la Dunia 2010 na kuwa kwenye matangazo ya Coca Cola.

Mwaka wa 1994 alirudi tena kucheza kwenye Kombe la Dunia akiwa na umri wa 42, na kuwa mchezaji mkongwe kucheza kwenye Kombe la Dunia, Cameroon wakabwagwa nje katika hatua ya makundi lakini kama kawa Milla alifunga bao dhidi ya Urusi na kuweka redi kama mfungaji mkongwe kwenye dimba hilo.

Kutokana na umaarufu wake Pepe Kalle alimwimbia wimbo.

VITUKO



Jamma mmoja amekataa kumpa mwenzake kazi kwa madai kwamba mbwa wake ana ubaguzi wa rangi. Jamma huyo aliambia gazeti la nchi hiyo kwamba akimpa jamma huyo kazi mbwa wake atamuuma jamma huyo, na kwamba si yeye aliye na ubaguzi wa rangi ila ni mbwa wake.

Thursday, 16 February 2012

George Weah


George Tawlon Manneh Oppong Ousman Weah Ni mwanakandanda mashuhuri duniani na mwanasiasa aliyegombea urais wa Liberia mwaka 2005. Weah alizaliwa Oktoba 1, 1966 katika jiji la Monrovia. Alikulia  kitongoji Clara. Kabla ya kujiunga na soka ya kulipwa Weah alikuwa akifanya kazi katika Shirika la Mawasiliano la Liberia kama fundi wa simu.
Aliwania urais bila mafanikio katika uchaguzi wa mwaka 2005, na kupoteza kwa Ellen Johnson Sirleaf katika duru ya pili ya upigaji kura. Katika uchaguzi wa 2011 alikuwepo kwenye kinyang'anyiro hicho kama mgombea mwenza wa Winston Tubman.

Kielimu, Weah ana Shahada ya Kwanza ya Michezo toka Chuo Kikuu cha Parkwood, London, Uingereza. Mwaka 1999 alipata shahada ya Udakitari ya Heshima toka Chuo Kikuu cha A.M.E Zion nchini Liberia.
Weah alianza safari yake ya soka katika timu za Incincible Eleven na Tonnerre Yaounde,  nchini liberia na Cameroon mtawalia. Baada ya hapo alikwenda kucheza soka la kulipwa Ulaya mwaka 1988. Alijiunga na timu ya Monaco chini ya ukufunzi wa Arsen Wenger alipoongoza ushindi wa kombe la Ufaransa mwaka 1991. Baadaye alijiunga na Paris Saint Germain mwaka 1992-95. Aliiongoza timu hii kuchukua kombe la ligi ya Ufaransa mwaka 1994. Mwaka wa 1994-95 alikuwa mfungaji bora kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya U.E.F.A . Mwaka 1995-2000 alikuwa akiichezea timu ya AC Milan ambayo ilishinda ligi ya Italia mwaka 1996 na 1999. Mwaka 2000 aliondoka AC Milan na kujiunga na Chelsea, baada ya muda mfupi alijiunga na Manchester City na baadaye Olympique Marseille mwaka 2001. Alimaliza soka ya kulipwa akiwa na timu ya Al JAzira ya Falme wa Nchi za Kiarabu.
Licha ya mafanikio haya yote kwa vilabu hivi hakuweza kuleta utaalamu wake kwenye timu ya taifa ya Liberia licha ya kuwasaidia Kifedha na hata kuwa kocha wao, licha ya kutambulika kwenye vilabu na mchezaji aliyeimarika wa Afrika hajawahi kucheza kwenye Kombe la Dunia.
Mwaka 1995 Weah alipewa tuzo na Shirikisho la Soka Duniani  (FIFA) na kuwa Mwanasoka Bora Duniani. Yeye ni mwanasoka wa pekee toka Afrika aliyewahi kupewa tuzo hiyo. Mwaka huo huo alichaguliwa kama Mwanasoka Bora Ulaya.
Miaka za 1989, 1994,na 1995 alikuwa Mwanasoka Bora Afrika.
Alikuwa mwanasoka bora Afrika mwaka wa1989 akichezea klabu ya AC Monaco na 1995 akichezea klabu ya AC Milan
Ndiye mwanasoka wa pekee wa Afrika aliyechaguliwa mchezaji bora wa karne na kumweka miongoni mwa wachezaji wachache waliowahi kushinda tuzo hili kama vile Pele wa Brazil na Johan Crujiff.
Mwaka wa 1996 alipigwa marufuku kutocheza mechi sita kwa kumjeruhi mwenzake wa timu pinzani pua kwa madai ya ubaguzi wa rangi.
Weah amekuwa akitoa misaada kusaidia wananchi wa Liberia. Mwaka 2004 alipewa tuzo ya Arthur Ashe kwa juhudi zake za kusaidia kujenga nchi yake. Alitajwa pia kuwa balozi wa UNICEF
Ana watoto wanne George weah jr, Tita, Timothy na mmoja adopted kutoka Lebanon Samer Hodroj.
Alibadilika toka Ukristu hadi Uislamu kabla ya kubadilika alisema kwamba waislamu na wakristu ni kitu kimoja.


VITUKO



Mtoto mmoja alizaliwa na kuwashangaza wazazi wake kwa kuanza kutoa sauti kama ile ya ndege badala ya kutoa sauti ya mtoto mchanga.
Waliokaribu naye wanasema kwamba mtoto huyo mwenye umri wa miaka 6 akikasirika anatupa mikono yake kama mabawa ndege anavyo fanya mabawa yake
na ukizungumza naye anatoa sauti kama ya ndege.

MJADALA

Je ni lazima mke afahamu mshahara wa mume wake toa maoni yako

Shakira tweets about sea lion attack in Cape Town

Colombian pop superstar Shakira was attacked by a sea lion as she tried to photograph and pet a group of the animals during a vacation in Cape Town, she said on Wednesday on her Facebook page.

 
Shakira said she thought the animal had mistaken her Blackberry phone for a fish and gone after it Photo: AP
"I thought to myself how cute they were so I decided to get a bit closer than all of the other tourists and went down to a rock trying to pet them, doing a baby talk while taking pictures," she said on the social networking site, in an account written after the Sunday incident.
"Suddenly, one of them jumped out of the water so fast and impetuously that it got about one foot (20 centimetres) away from me, looked me in the eye, roared in fury and tried to bite me. Everyone there screamed, including me. I was paralysed by fear and couldn't move."
The singer, whose "Waka Waka" was the official song of the 2010 World Cup in South Africa, said her brother, "Super Tony", saved her by jumping over her and hauling her out of the sea lion's reach.
She said she and her brother both scratched themselves on the rocks while trying to protect themselves, and posted a picture of a small scrape on her hand.
Shakira said she thought the animal had mistaken her Blackberry phone for a fish and gone after it.

Wednesday, 15 February 2012

WATOTO WA MGANGA

Nchini Zambia wanawake wawili waliokuwa wamekwenda kumwona daktari,lakini walipokuwa wakimsubiri daktari huyo walizungumzia matatizo yao.
Mmoja alisema," Natamani sana kupata mtoto kuliko kitu kingine duniani, lakini nadhani haitawezekana."
Wapili akajibu," Mie pia nilidhani kuwa haiwezekani lakini mambo yakabadilika ndiposa niko hapa. Natarajia kupata mtoto kwa miezi mitatu zijazo."
"Basi niambie ulifanya vipi," akajibu.
"Mimi nilimtembelea mganga wa kienyeji."
Wa kwanza akajibu," Nimefanya hivyo nikiwa na mume wangu mwanzoni mwa mwaka huu lakini haikunifaidi."
Mwanamke wa pili akaangua kicheko na kumnong'onezea mwenzake kuwa,"Basi dada siku nyingine ukimtembelea mganga huyo usiende na bwanako."

VITUKO



Baada ya siku ya Valentine mwanamme mmoja amewashangaza watu kwa kuwa mwanamme wa peke na mzee kabisa kwa kumuowa msichana kipenzi chake cha roho aliyemwacha na umri wa miaka 22. Mzee huyo ambaye ana miaka 96 alifunga ndoa na mpenziye nyumbani kwake baada ya kuchumbiana kwa miaka 22.

ABEDI AYEW



Anajulikana kitaalamu kama Abedi Pele, alizaliwa Novemba 5 1964 alikuwa mchezaji wa zamani na nahodha wa Ghana. Alipata umaarafuru akichezea soka katika Ligue 1 ya Ufaransa na Lille OSC na Olypique Marseille. Alipewa jina la utani la ''Pele'' katika kutambua uwezo wake mkuu kulinanishwa na mchezaji wa Brazil Pele.

Abedi Pele alikuwa mmoja wa waanzilishi wa mpira wa miguu ya Afrika katika Ulaya. Ni mmoja wa wachezaji wa kwanza wa Afrika kuchezea soka kwenye vilabu vya Ulaya kama vile Uswisi, Ujerumani na pia Italia, ni maarufu huko Ufaransa alikochezea sana haswa kwenye kilabu cha Marseille katika Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati wa miaka ya 1990.

Aliondika Ghana kwenda Qatar baada ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka wa 1982. Baada ya miaka michache alirudi Ghana na akakosa kusajiliwa na klabu ya Kotoko kisha baadaye alijiunga na kilabu ya AS Dragons FC de l'Oueme ya Benin. Alirudi Ghana na kujiunga na timu ya Real Tamale United kwa Muhula mmoja. Alianza soka yake ya kimaaifa huko Ufaransa na klabu ya Chamois Niort, Montpellier na Lille kisha akajiunga na Olympique Marseille, baadaye alihamia Lyon.

Alikuwa nahodha wa timu ya soka ya Ghana kwa miaka 6 tangu 1992 – 1998 na alikuwa mwafrika wa kwanza kumaliza katika nafasi ya kwanza ya mchezaji bora wa FIFA orodha ya mwaka 1991 na 1992. Ni mchezaji bora wa Afrika ameshinda tuzo kadha wa kadha zikiwemo Shirikisho la soka Afrika, Tuzo la mchezaji bora la BBC, alituzwa pia kuwa mchezaji bora katika kombe la mataifa la Afrika 1992 na aalikuwa man of the match katika fainali ya mechi ya kihistoria ya Ligi ya Mabingwa ya Ulaya kati ya Marseille na Milan mwaka 1993.

Ana mtoto ambaye pia alifuata nyayo zake na pia anachezea timu ya nyumbani ya Ghana na alikuwa miongoni mwa wachezaji waliokuwa kwenye Kombe la Afrika lililokamilika hapo jana.

Abedi Pele Ayew alizindua mnara wake huko Equitorial Guinea wakati wa michezo hiyo kwa kuwa mchezaji bora kuwahi tika barani Afrika.

Tuesday, 14 February 2012

Show ya Pepea Afrika inawatakieni nyote Valentine Njema muisherekee poa kwa amani na mapendo.
Furahikieni nyote siku hii na muwakumbuke watoto wagonjwa walioko hospitalini. Asanteni sana kwa kusikiliza PEPEA AFRIKA.

Monday, 13 February 2012

KALUSHA BWALYA


 Alizaliwa Agosti 16 1963 huko Mfululira.Anajulikana sana kwa urahisi kama Kalusha. Alikuwa kocha wa Zambia na pia mwanakandanda, ni mchezaji wa Zambia aliye imarika zaidi katika soka na mfungaji bora zaidi na anajulikana kama mchezaji maarufu kuwahi kucheza soka nchini Zambia. Alitajwa kama mchezaji bora wa mwaka kutoka Afrika 1988 na gazeti la France Football na kuorodheshwa miongoni mwa wachezaji bora duniani na FIFA mwaka wa 1996 kisha kuchaguliwa na akawa nambari 14 wachezaji bora wa dunia.

Alianza kujishughulisha na soka utotoni mwake kama vijana wengine wa Kiafrika, yeye na marafiki wake walicheza huko mitaani na hapo ndipo aliaanza kupata ujuzi kwenye mchezo huo. Walikuwa wakicheza miguu mitupu kwa mpira uliotengenezwa kwa makaratasi.Kila mara walikuwa wakicheza na ndugu ya ambapo karibu kila mara walishinda.

Kalusha aliona mechi nyingi sana akiwa bado na umri mdogo, akiwa na umri wa miaka14 alikuwa tayari kashaanza kucheza mechi za Ligi na klabu ya Blackpool.Bwalya alikuwa mjumbe wa kikosi cha kitaifa ambacho walishiriki katika Michezo ya Olimpiki ya 1988 na kuweka alama yake kwa kufunga mabao matatu katika ushindi wa 4 – 0 dhidi ya Italia.

Ingawa alikuwa nahodha wa timu ya taifa ya kandanda wakati wa mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia 1994, Kalusha hakuwa kwenye ndege ya iliyoanguka Aprili27 1993 wakati timu nzima na wasimamizi wa soka walifariki wakati ndege hiyo ilianguka kwenye bahari ya Atlantic kwenye ufuo wa Gabon. Kisha alianza kutafuta na kutengeneza timu nyingine ya taifa

Yeye ndiye alikuwa mchezaji-kocha wakati wa mechi za kufuzu kombe la dunia mwaka 2006. Tarehe 5 septemba 2004, Zambia ilicheza na Liberia, na mechi ilikuwa sare bin sare, Kalu alivyokuwa akijulikana wakati ule mwenye umri wa miaka 41, aliingia kwenye kipindi cha pili na ilikuwa mechi yake ya 147na kufunga bao lake la 100, akasema amefunga bao hilo kwa ajili ya Nchi yake. Hata hivyo, Zambia ilikuwa ya tatu kwenye kundi hilo na kushindwa kufuzu kwa Kombe la Dunia Mwaka 2006. Tunavyozungumza sasa hivi yeye ndiye msimamizi wa soka nchini humo na alikuwepo Zambia ikishinda Kombe la Bara Afrika tarehe 12 Januari 2012.

MBWEMBWE

                NANI ALIYE  NA MAKOSA HAPA

Friday, 10 February 2012

MBWEMBWE

                                                                                     SIKU MBAYA HUANZA ASUBUHI
Kulikuwa na jamaa huku Afrika Kusini alikuwa ameketi ndani ya bar huku akitazama kinywaji chake kwa nusu saa.
Kwa bahati katokea dereva mmoja wa lori ambaye amekuwa akiwasumbua watu sana kwenya bar hio. Moja kwa moja akafululiza na kunywa kinywaji chake jamaa yule na kuhakikisha kuwa amelimaliza. Amini usiamini, jamaa yule mwanaume mzima alianza kulia kama mtoto mchanga.
Dereva yule alishangaa sana na kumwomba jamaa yule msamaha na kusema kuwa alikuwa tu afanya mzaha na atamnunulia kinwaji kingine kulipiza alichokuwa amekunywa, lakini jamaa yule alimwambia dereva kuwa si kinywaji alichokuwa analilia bali ni masaibu yaliyomkabili  toka asubuhi. Alisema,"Leo asubuhi nilichelewa kwenda kazini naye bosi wangu akanifurusha kazini.
"Kutoka kazini sikuegesha gari langu vyema barabarani nalo likaibwa na wezi. Kupiga ripoti kwa polisi wao wamedinda kunipa usaidizi kwa sababu wanahitaji stakabadhi la gari hilo ambazo pia zilipotea. Nikachukua taxi kuelekea nyumbani. Kwa bahati mbaya nikasahau mkoba wangu wa pesa na sithakabadhi zangu zote za benki kwenye taxi. Kumuuliza dereva wa taxi akapinga kuwa hajaziona.
"Nilipofika nyumbani, nusura nizirai.Nilimpata mke wangu chumbani na shambaboy wangu. Ndiposa nikaja hapa ili kufikisha mwisho matatizo ambayo yananikumba. Nilipokuwa na tafakari kuhusu hayo, wewe ukaja na kunywa sumu yangu.

VITUKO



Refferre mmoja ambaye aliangusha kaptula yake wakati wa mechi ya wanawake ya raga amesimamishwa kazi kwa muda wa wiki 18.
Msimamizi wa chama cha raga cha wanawake alisema reffa huyo aliyetoa kaptula yake kimakusudi atachukuliwa hatua nyingine baada ya hiyo. Wachezaji nao walisema walishtuka na walioona ndio maana walipoteza mchezo

Shaka


  Alizaliwa 1781 - 1828 alikuwa kiongozi wa Wazulu aliyebadilisha ukoo mdogo wa Kinguni kuwa kabila au taifa kubwa lililotawala maeneo mapana ya Afrika Kusini hasa Natal ya leo.
Sifa zake zimetokana na uwezo wa kupanusha utawala wake kutoka eneo ndogo la 260 km² kuwa 28.500 km², kuvunja nguvu ya makabila mengine na kuyaunganisha na taifa lake. Katika historia ya kijeshi ya Afrika alianzisha mbinu mpya zilizopanusha uwezo na enzi yake. Sifa hizi, jinsi ilivyo mara nyingi na viongozi wanaotegemea nguvu ya kijeshi, zimeenda pamoja na vita na uharibufu mwingi. Miaka ya Shaka ilianzisha kipindi cha mfecane yaani "uharibifu" kinachokumbukwa na mataifa mengi ya Afrika Kusini.


Jina lake linatokana na neno la kizulu "iShaka" linalomaanisha mdudu ambaye katika imani ya utamaduni wa Kizulu anasemekana kuvuruga hedhi ya kinamama. Jina hili ni dalili la kuzaliwa nje ya ndoa. Hivyo miaka ya kwanza ya Shaka ilikuwa miaka migumu bila baba jambo ambalo lilimfanya aone kama anadharauliwa na watu wengine. Utoto huu ulisababisha hasira ndani yake akalipiza kisasi baadaye.

Kama kijana Shaka alikaa kwa kabila kubwa zaidi ya Mthethwa alikoingia pamoja na hirima yake katika jeshi. Wakati ule ukoo wa Wazulu ulikubali Wamthehtwa kuwa mabwana wao. Chifu wa Mthethwa alikuwa Dingiswayo aliyeanzisha utaratibu mpya wa impi yaani kupanga watu wake vitani katika vikundi na kuwa na ngazi mbalimbali za mamlaka. Shaka alihudumia miaka sita katika vita za Dingiswayo akawa hodari sana na kujifunza uongozi alioboresha baadaye.
Baada ya kifo cha babake Shaka alirudi kwa Wazulu kwa msaada wa Dingiswayo akachukua uongozi mnamo mwaka 1812. Baada ya kuwa kiongozi akalipiza kisasi maadui wa utoto wake akiwaua kwa njia mbalimbali.
Shaka aliendelea kukubali ubwana wa Mthethwa na Dingiswayo hadi akauwawa vitani na kabila la Ndwandwe mwaka 1817. Lakini pamoja na hayo alipigana vita na makabila madogo jirani. Mbinu yake ilikuwa kuwashambulia waliompinga au kuwa hatari kwake; wanawake na watoto waliingizwa katika ukoo wake, pamoja na wanajeshi wa kiadui wasiouawa lakini waliokubali kumfuata baada ya kushindwa. Kwa njia hiyo ukoo mdogo wa Wazulu uliendelea kukua.

Katika miaka iliyofuata Shaka aliendelea kushambulia vikundi vya jirani na kuwaingiza katika utawala wake. Makabila mengine walimfuata bila vita wakikubali uongozi wake na kuingiza vijana wao katika impi au vikosi vya kijeshi vya Shaka. Alituma viongozi au majenerali wake pamoja na impi pande mbalimbali hadi Msumbiji au pia Zimbabwe. Vikundi kama Ndebele huko Zimbabwe au hata Wangoni katika Tanzania ni matokeo ya matembezi ya impi za kizulu zilizoenda mbali na kupoteza mawasiliano na nyumbani.
Vita hizi zilisababisha makabila mengine kukimbia na kuhamahama wakishambulia majirani zao hivyo kupanusha eneo la vita katika nchi mbali na Wazulu wenyewe. Kipindi hiki kinakumbukwa kwa majina kama "mfecane" (Kizulu) au "difaqane" (Kisotho) kuwa miaka 30 ya vita na kifo.
Pamoja na hayo makabila mengine kama Wasotho, Waswazi, Wandebele au Wagaza walioshambuliwa walijifunza mbinu za kijeshi wakifaulu kujitetea na kuanzisha mataifa makubwa yakiunganisha wenyewe koo na makabila madogo zaidi.
Utawala wa Shaka ulikuwa na tabia za kinyama zilizosababisha chuki nyingi dhidi yake. Baada ya kifo cha mamake Nandi alikuwa na hasira kiasi cha kuuwa watu 7000 kati ya wanajeshi wake kwa kosa la kutoonyesha huzuni ya kutosha na kuamuru kipindi cha kufunga miezi mitatu. Aliamuru mashamba yasilimwe kwa mwaka mmoja na kila mwanamke aliyeonekana kuwa na mimba katika kipindi hiki aliuawa pamoja na mumewe. Wataalamu wengine huona ya kwamba wakati ule Shaka alionekana kuwa na kichaa. Maadui walifanya mipango dhidi yake mwishowe aliuawa na ndugu zake. Mwaka 1828 impi nyingi zilikuwa mbali vitani ikuli ikawa bila ulinzi wa kutosha. Kaka zake Dingane na Mhlangana walimwua na kutupa maiti shimoni.
Dingane alimfuata Shaka akaua vingozi wengi waliokuwa waaminifu kwa Shaka.
Alilazimisha watu wake kuacha vyandalua na viatu na kutembea pekupeku. Hii iliongeza kasi ya impi zake na uwezo wao wa kushambulia haraka. Inasemekana ya kwamba Shaka aliuwa wote waliolalamika walipoamriwa kuacha viatu vyao.


Wednesday, 8 February 2012

VITUKO



Kuna simu mpaya ya rununu ambayo inawajulisha watu kuhusu choo cha umma ambacho kiko karibu nao. Simu hiyo iliyozinduliwa na askari wa baraza katika nchi fulani, unahitaji kutuma ujumbe mfupi kwa nambari 80097 ukitanguliza na jina Choo kisha utaletewa maelezo zaii kuhusu choo ambacho kiko karibu nawe.

Wangari Maathai



Alizaliwa 1 Aprili 1940 alikuwa mwanaharakati wa masuala ya mazingira na haki za wanawake kutoka nchini Kenya. Mwaka wa 2004 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani. Yeye ni mwanamke Mwafrika wa kwanza kupokea tuzo hilo. Pia, aliwahi kuwa mbunge wa Kenya na waziri msaidizi katika serikali ya Mwai Kibaki kati ya Januari 2003 hadi Novemba 2005.


Katika maandalizi ya uchaguzi wa 2007 Maathai alisimama upande wa rais Kibaki lakini hakuteuliwa na chama cha PNU akagombea kwa chama cha Mazingira Green Party lakini hakurudi bungeni.


Maathai alihudhuria shule ya msingi ya Ihithe,akiwa na miaka kumi na moja alisomea shule ya kikatoliki ya Mt. Cecilia huko Nyeri akiwa huko alikisoma Kiingereza na kukielewa vyema kisha akabadili dini na kuwa mkatoliki na kupata jina Mary Josphine alipomaliza masomo yake kule alijiunga na shule ya upili ya wasichana ya kikatoliki ya Loreto Convent, Limuru. Baada ya kuhitimu sekondari, alienda ng’ambo kusoma bayologia nchini Ujerumani na Marekani. Mwaka wa 1967, alipata shahada ya kwanza ya bayologia kutoka Chuo Kikuu cha Benedictine, Marekani. Aliendelea na masomo yake katika Chuo Kikuu cha Pittsburg ambako alipata shahada ya pili. Halafu alirudi Nairobi na kupata shahada ya udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi katika somo la udaktari wa wanyama. Kuanzia mwaka wa 1977, Maathai alikuwa profesa msaidizi wa anatomia ya wanyama huko Nairobi akiwa mwanamke wa kwanza kupata uprofesa katika chuo kikuu cha Nairobi.
Baadhi ya tuzo zake ni Tuzo ya Mwanamke wa Dunia (1983), Tuzo ya Goldman kwa Mazingira (1991), Elder of the Burning spear (2003) kutoka serikali ya Kenya, Tuzo ya Nobel ya Amani (2004), na Legion D’Honneur (2006) kutoka serikali ya Ufaransa.


Mwaka wa 1977, Maathai alianzisha shirika la Green Belt Movement ambalo linajihusisha hasa na mazingira, haki za raia na demokrasia.
Mwaka wa 1971 alikuwa mwanamke wa kwanza eneo la Afrika Mashariki kupata Ph.D


Mwaka wa 1969, Wangari Muta (jina lake la kuzaliwa) alifunga ndoa na Mwangi Maathai, mwanasiasa wa Kenya. Wana watoto watatu, Waweru, Wanjira na Muta, lakini walitengana baadaye.
Maathai na mume wake, Mwangi Mathai, walitengana mwaka 1977. Baada ya kujitenga kwa muda mrefu, Mwangi alipeleka kesi kotini kutaka talaka mwaka 1979. Mwangi alisema kwambaWangari alikuwa mwanamke mwenye akili nyingi na kwamba alikuwa "hawawezi kumdhibiti".Jaji alikata rufa kwa upande wa Mwangi na akawa ameshinda kesi hiyo. Muda mfupi baada ya kesi, katika mahojiano na gazeti la Viva, Maathai alisema kwamba hakimu yule hajui kazi yake ama alipata rushwa jambo ambalo lilimfanya kushtakiwa na kufungwa kwa miezi sita.

Muda mfupi baada ya talaka, mume wake wa zamani aliandika barua kupitia wakili wake, na kudai kuwa Maathai kuacha jina lake lakini badala yake alichagua kuongeza herufi "a" badala yake.

Oktoba 1989 Maathai alikuja kutambua kwamba serikali inataka kujanga jumba la orofa 60 katika uwanja wa Uhuru Park na jumba hilo lilikuwa liwe makao makuu ya chama cha KANU. Mpango huo ulikuwa pia kusimamisha sanamu ya rais wake ule rais Moi.Maathai aliandika barua kukataa mipango hiyo lakini zilipuuzwa na serikali na kuzidi wakamwiita mwanamke mwenye kichaa.

Tarehe 12 Desemba, katika Uwanja wa Uhuru Park, katika hotuba ya kuadhimisha uhuru wa Kenya , Rais Moi alimshauri Maathai kuwa mwanamke sahihi katika utamaduni wa Afrika na kuwapa watu heshima na kuwa na utulivu.

Mwaka wa 2004 alipata tuzo la Amani la Nobel na kuwa mwanamke wa kwanza kutoka Afrika na mwanaharakati wa mazingira kupata tuzo hilo.

Wangari Maathai alifariki kutokana na matatizo yanayotokana na saratani ya ovary wakati alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Nairobi tarehe 25 Septemba 2011.