Pages

Friday, 17 February 2012

ROGER MILLA



Alizaliwa kama Albert Roger Miller Mooh tarehe 20 Mei 1952 ni mwanasoka mstaafu kutoka Cameroon aliyecheza kama Mshambuliaji. Alikuwa mwafrika wa kwanza ambaye Nyota yake iling'aa katika kandanda kimataifa. Alichezea timu yake ya Camerron mara tatu kwenye Kombe la Dunia.
Alipata mafanikio mengi akiwa na kiaka 38 umri ambao washambulizi wengi hustaafu wakifika. Alifunga mabao manne kwenye Kombe la Dunia mwaka1990, bao lililompa umaarufu na kumfanywa kukumbukwa ni lile wakicheza na Colombia ambapo alionyesha ujuzi na mahanjam yake na kumchenga kipa Rene Higuitana kufunga katika yadi 35 kutoka lango lake na kusaidia Cameroon kufika robo fainali ikawa timu ya kwanza kutoka Afrika kifikia kiwango hicho.

Pia anakumbukwa kwa ishara yake ya kusherehekea bao alipofunga, kwa kukimbia hadi kwenye kibendera cha kona na kuanza kucheza ngoma.
Pele wa Brazil alimtaja miongoni mwa wachezaji 125 waliosifika kwenye mchezo huo ambao bado wanaishi.

Alizaliwa katika mji mkuu wa Yaounde'. Alianza kucheza soka akiwa na miaka 13 kwenye klabu ya Douala na akiwa na miaka 18 alishinda ligi yake ya kwanza. Mwaka wa 1974 alipewa tuzo la mchezaji bora wa Afrika. Mwaka wa 1977 alihamia ulaya na kuchezea klabu ya Valenciennes huko Ufaransa, hata hivyo aliwekwa kwenye timu ya hifadhi miaka miwili. Mwaka wa 1979 alijiunga na AS Monaco lakini bado akajipata palepale kwenye hifadhi,mwaka uliofuatia alijiunga na klabu ya Bastia lakini bado hakustawi, hatimaye akapata umaarufu kwenye klabu ya Saint-Etienne mwaka 1984.

Alichezea timu yake ya Cameroon mara ya kwanza mwaka wa 1978, alikuwa pia miongoni mwa wachezaji wa timu hiyo waliocheza Kombe la Dunia mwaka wa 1982, na bao lake lilikataliwa wakicheza dhidi ya Peru. Miaka miwili baadaye alikuwa katika kikosi cha mashindano ya Michezo ya Olimpiki ya 1984 huko Los Angeles ,California. Alistaafu kutoka soka ya kimataifa mwaka 1987 na kuhamia Reunion katrika Bahari ya Hindi.

Hata hivyo, mwaka 1990, alipokea simu kutoka kwa Rais wa Cameroon wakati ule Paul Biya ambaye alimsihi na kumbembeleza kutoka ustaafuni na kujiunga tena na timu taifa. Alikubali na kwenda Italia na Indomitable Lions kucheza Kombe la Dunia 1990.

Alijitokeza kama mchezaji kama mchezaji mashuhuri kwenye Kombe hilo kwa kufunga mabao manne, mawili kwenye muda wa nyongeza na pia jinsi alivyo yasherehekea mabao hayo yote manne.
Bao lake la pili dhidi ya Colombia mwaka huo ndilo lililokuwa mada kwenye Kombe la Dunia 2010 na kuwa kwenye matangazo ya Coca Cola.

Mwaka wa 1994 alirudi tena kucheza kwenye Kombe la Dunia akiwa na umri wa 42, na kuwa mchezaji mkongwe kucheza kwenye Kombe la Dunia, Cameroon wakabwagwa nje katika hatua ya makundi lakini kama kawa Milla alifunga bao dhidi ya Urusi na kuweka redi kama mfungaji mkongwe kwenye dimba hilo.

Kutokana na umaarufu wake Pepe Kalle alimwimbia wimbo.

No comments:

Post a Comment