Pages

Wednesday, 8 February 2012

Wangari Maathai



Alizaliwa 1 Aprili 1940 alikuwa mwanaharakati wa masuala ya mazingira na haki za wanawake kutoka nchini Kenya. Mwaka wa 2004 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani. Yeye ni mwanamke Mwafrika wa kwanza kupokea tuzo hilo. Pia, aliwahi kuwa mbunge wa Kenya na waziri msaidizi katika serikali ya Mwai Kibaki kati ya Januari 2003 hadi Novemba 2005.


Katika maandalizi ya uchaguzi wa 2007 Maathai alisimama upande wa rais Kibaki lakini hakuteuliwa na chama cha PNU akagombea kwa chama cha Mazingira Green Party lakini hakurudi bungeni.


Maathai alihudhuria shule ya msingi ya Ihithe,akiwa na miaka kumi na moja alisomea shule ya kikatoliki ya Mt. Cecilia huko Nyeri akiwa huko alikisoma Kiingereza na kukielewa vyema kisha akabadili dini na kuwa mkatoliki na kupata jina Mary Josphine alipomaliza masomo yake kule alijiunga na shule ya upili ya wasichana ya kikatoliki ya Loreto Convent, Limuru. Baada ya kuhitimu sekondari, alienda ng’ambo kusoma bayologia nchini Ujerumani na Marekani. Mwaka wa 1967, alipata shahada ya kwanza ya bayologia kutoka Chuo Kikuu cha Benedictine, Marekani. Aliendelea na masomo yake katika Chuo Kikuu cha Pittsburg ambako alipata shahada ya pili. Halafu alirudi Nairobi na kupata shahada ya udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi katika somo la udaktari wa wanyama. Kuanzia mwaka wa 1977, Maathai alikuwa profesa msaidizi wa anatomia ya wanyama huko Nairobi akiwa mwanamke wa kwanza kupata uprofesa katika chuo kikuu cha Nairobi.
Baadhi ya tuzo zake ni Tuzo ya Mwanamke wa Dunia (1983), Tuzo ya Goldman kwa Mazingira (1991), Elder of the Burning spear (2003) kutoka serikali ya Kenya, Tuzo ya Nobel ya Amani (2004), na Legion D’Honneur (2006) kutoka serikali ya Ufaransa.


Mwaka wa 1977, Maathai alianzisha shirika la Green Belt Movement ambalo linajihusisha hasa na mazingira, haki za raia na demokrasia.
Mwaka wa 1971 alikuwa mwanamke wa kwanza eneo la Afrika Mashariki kupata Ph.D


Mwaka wa 1969, Wangari Muta (jina lake la kuzaliwa) alifunga ndoa na Mwangi Maathai, mwanasiasa wa Kenya. Wana watoto watatu, Waweru, Wanjira na Muta, lakini walitengana baadaye.
Maathai na mume wake, Mwangi Mathai, walitengana mwaka 1977. Baada ya kujitenga kwa muda mrefu, Mwangi alipeleka kesi kotini kutaka talaka mwaka 1979. Mwangi alisema kwambaWangari alikuwa mwanamke mwenye akili nyingi na kwamba alikuwa "hawawezi kumdhibiti".Jaji alikata rufa kwa upande wa Mwangi na akawa ameshinda kesi hiyo. Muda mfupi baada ya kesi, katika mahojiano na gazeti la Viva, Maathai alisema kwamba hakimu yule hajui kazi yake ama alipata rushwa jambo ambalo lilimfanya kushtakiwa na kufungwa kwa miezi sita.

Muda mfupi baada ya talaka, mume wake wa zamani aliandika barua kupitia wakili wake, na kudai kuwa Maathai kuacha jina lake lakini badala yake alichagua kuongeza herufi "a" badala yake.

Oktoba 1989 Maathai alikuja kutambua kwamba serikali inataka kujanga jumba la orofa 60 katika uwanja wa Uhuru Park na jumba hilo lilikuwa liwe makao makuu ya chama cha KANU. Mpango huo ulikuwa pia kusimamisha sanamu ya rais wake ule rais Moi.Maathai aliandika barua kukataa mipango hiyo lakini zilipuuzwa na serikali na kuzidi wakamwiita mwanamke mwenye kichaa.

Tarehe 12 Desemba, katika Uwanja wa Uhuru Park, katika hotuba ya kuadhimisha uhuru wa Kenya , Rais Moi alimshauri Maathai kuwa mwanamke sahihi katika utamaduni wa Afrika na kuwapa watu heshima na kuwa na utulivu.

Mwaka wa 2004 alipata tuzo la Amani la Nobel na kuwa mwanamke wa kwanza kutoka Afrika na mwanaharakati wa mazingira kupata tuzo hilo.

Wangari Maathai alifariki kutokana na matatizo yanayotokana na saratani ya ovary wakati alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Nairobi tarehe 25 Septemba 2011.

No comments:

Post a Comment