Ali
Mazrui Al'amin alizaliwa Februari 1933 huko Mombasa Kenya, ni
mwandishi wa Kisiasa kuhusu Afrika na masomo ya kiislamu.Yeye ni
Profesa wa Albert Schweitzer na mkurugenzi wa Taasisi ya Utamaduni
ya Global katika Chuo Kikuu cha Binghamton huko Binghaton, New York.
Mazrui
alisomea katika shule za Mombasa, nchini Kenya, alipata B.A yake
kutoka Chuo Kikuu cha Manchester nchini Uingereza mwaka 1960 na M.A
yake kutoka Chuo Kikuu cha Columbia huko New York mwaka 1961, na
Shahada ya Udaktari (Dph ) kutoka Chuo Kikuu cha Oxford mwaka 1966.
Baada
ya kukamilisha elimu yake katika Chuo kikuu cha Oxford, Mazrui
alijiunga na chuo kikuu cha Makerere( kampala Uganda) ambapo aliwahi
kuwa mkuu wa Idara ya Sayansi ya Siasana Mkuu wa Kitivo cha Sayansi
ya Jamii. Mwaka wa 1973 alilazimika kwenda uhamishoni na Idi
Amin.Mwaka 1974 alijiunga na kitivo cha Chuo kikuu cha Michigan kama
Profesa na baadaye aliteuliwa Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo ya
Afroamerican na Afrika (1978-1989).
Utafiti
na maslahi yake ni pamoja siasa za Afrika, Utamaduni wa siasa za
kimataifa, Uislamu wa Kisiasa na Uhusiano wa Kaskazini na Kusini, ni
mwandishi wa vitabu zaidi ya ishirini.
JE
WAJUA
Mbali
na uteuzi wake kama profesa wa Albert Schweitzer katika sayansi ya
siasa, mafunzo ya Afrika, filosofia, Ufafanuzi na Utamaduni
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utamaduni ya Global, Mazrui pia ana nyadhifa
zingine tatu katika chuo kiku cha Jos nchini Nigeria,na chuo kikuu
cha Cornell huko New York na pia ni kansela wa Jomo Kenyatta chuo
kikuu cha Kilimo na Teknolojia.
Mwaka
wa 2005, Mazrui Ali alichaguliwa wa 73 kwenye orodha ya wasomi 100
duniani na gazeti la Prospective la Uingereza na pia la Foreighn
Policy la Marekani.
Hivi
sasa ana zaidi ya nyadhifa 8 katika nchi tatu.
Pia
yeye huchangia mara kwa mara katika magazeti ya Kenya, Uganda na
Afrika Kusini.
Ana
tuzo zaidi ya kumi kutoka nchi mbalimbali na vyuo Vikuu mbalimbali.
No comments:
Post a Comment