Pages

Tuesday, 7 February 2012


Steve Biko

Steve Bantu Biko alikuwa akifahamika kama mwanaharakati anayepiga vita dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, mnamo miaka ya 1960 na 1970.
Biko alikuwa kiongozi wa wanafunzi, baadae akaanzisha vuguvugu la Black Consciouness Movement (Harakati za kujitambua kwa watu weusi). Vuguvugu hili lilipata nguvu sana na kuenea katika miji mingi yenye idadi kubwa ya watu weusi.
Mauti yalimfikia baada ya kutiwa mbaroni na kuteswa na maaskari wa serikali ya kibaguzi. Biko alijulikana kama jabali la harakati dhidi ya ubaguzi wa rangi. Wakati yupo hai, alikuwa akiandika sana masuala ya harakati za kujaribu kuwatia nguvu watu weusi na aliweza kuwa maarufu kwa wito wake wa kusema kwamba "black is beautiful" akimaanisha kwamba "mtu mweusi ni mzuri." Alielezea maana ya msemo huu ni: "mtu, ni sawa kama ulivyo mtu, lakini anza kujiangalia mwenye ukiwa kama binaadamu.
Stephen Bantu Biko alizaliwa mjini King Williams Town, ndani ya jimbo la Eastern Cape nchini Afrika Kusini 18 Desemba, 1946 . Biko alikuwa mwananfunzi wa Chuo Kikuu cha Natal Medical School.
Hapo awali Biko alikuwa akijishughulisha na masuala ya kutafuta "Umoja wa Umma wa Wanafunzi Afrika Kusini" (National Union of South African Students), baada ya kuweza kuwaadikisha watu weusi, wahindi, na watu weupe pia, kwamba wakiwa kama wanfunzi wanahitaji jumuiya itakayokuwa inawaangalia wanafunzi.

Mnamo tarehe 18 Agosti ya mwaka 1977, Biko alitiwa nguvuni na mapolisi kwa kosa la ugaidi kifungu namba 83 cha 1967 cha nchini Afrika Kusini. Steve Biko alipatwa na majeraha makubwa kichwani baada ya kukamatwa na mapolisi na kuanza kumpa kipigo kisichokuwa na kifani. Wakamfunga na minyororo katika kidirisha cha machuma kwa muda wa siku nzima.
Mnamo tarehe 11 Septemba ya mwaka 1977 polisi walimfunga Biko nyuma ya gari aina ya Land Rover, akiwa uchi, na kuanza kuendesha gari kwa umbali wa km 1,200. Alikufa mda mchache baada ya kujiri katika jela ya Pretoria, mnamo tarehe 12 Septemba ya mwaka 1977.
Polisi wakatangaza kwamba kifo chake kilisababishwa na njaa kali. Biko alikutwa na majeraha makubwa kichwani kwake, ambapo mengi yalionekana kama ushaidi mkali kuwa jamaa alifanyiwa kitendo cha kiukatili na hao waliomkamata. Kisha mwandishi wa habari na kiongozi wa kisiasa wa sasa, Bi. Helen Zille, alifuchua ukweli uliojificha juu ya kifo cha Biko.
Mwaka uliofuata tarehe 2 Februari 1978, jaji mkuu wa Eastern Cape alitoa tamko la kusema kwamba hatotoa hukumu kwa askari yoyote yule aliyehusika kwa kukamatwa na kutiwa kuizini kwa Biko. Wakati kesi inaendelea, ilitangazwa kuwa majeraha yote yaliyokuwa kichwani kwa Biko, ilikuwa ni kutaka kujaribu kujiua mwenyewe, na haikumaanisha kuwa Biko alipigwa.
Baada ya hujma na mazungushano ya huku na kule ikabidi iundwe "Tume ya ukweli na upatanishi" (Kwa Kiing:Truth and Reconciliation Commission), ambayo iliundwa kwa kufuata taratibu ndogo tu za kibaguzi, ilitaarifiwa mnamo 1997 kuwa moja kati ya maaskari watano wa kikosi cha usalama nchiini Afrika Kusini, alikubali kuwa yeye alichangia kuuawa kwa Biko, askari huyo ambaye alikuja kufa katika machafuko ya Soweto zidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika ya Kusini.
Mnamo tarehe 7 Oktoba mwaka 2003 Wizara ya Sheria ya Afrika Kusini ilitangaza rasmi kwamba maaskari watano walioshtakiwa kwa kosa la mauwaji ya Biko, hawato hukumiwa kwasababu hakuna ushaidi wa kotosha, ukweli ni kwamba muda wa kutoa hukumu pia nayo ushapita, hivyo hamna hukumu yoyote ile zidi ya maaskari hao.

1 comment: