Alizaliwa
1781 - 1828 alikuwa kiongozi wa Wazulu
aliyebadilisha ukoo mdogo wa Kinguni
kuwa kabila au taifa kubwa lililotawala maeneo mapana ya Afrika
Kusini
hasa Natal
ya leo.
Sifa
zake zimetokana na uwezo wa kupanusha utawala wake kutoka eneo ndogo
la 260 km² kuwa 28.500 km², kuvunja nguvu ya makabila mengine na
kuyaunganisha na taifa lake. Katika historia ya kijeshi ya Afrika
alianzisha mbinu mpya zilizopanusha uwezo na enzi yake. Sifa hizi,
jinsi ilivyo mara nyingi na viongozi wanaotegemea nguvu ya kijeshi,
zimeenda pamoja na vita na uharibufu mwingi. Miaka ya Shaka
ilianzisha kipindi cha mfecane
yaani "uharibifu" kinachokumbukwa na mataifa mengi ya
Afrika Kusini.
Jina
lake linatokana na neno la kizulu "iShaka" linalomaanisha
mdudu ambaye katika imani ya utamaduni wa Kizulu anasemekana kuvuruga
hedhi ya kinamama. Jina hili ni dalili la kuzaliwa nje ya ndoa. Hivyo
miaka ya kwanza ya Shaka ilikuwa miaka migumu bila baba jambo ambalo
lilimfanya aone kama anadharauliwa na watu wengine. Utoto huu
ulisababisha hasira ndani yake akalipiza kisasi baadaye.
Kama
kijana Shaka alikaa kwa kabila kubwa zaidi ya Mthethwa
alikoingia pamoja na hirima yake katika jeshi. Wakati ule ukoo wa
Wazulu ulikubali Wamthehtwa kuwa mabwana wao. Chifu wa Mthethwa
alikuwa Dingiswayo
aliyeanzisha utaratibu mpya wa impi
yaani kupanga watu wake vitani katika vikundi na kuwa na ngazi
mbalimbali za mamlaka. Shaka alihudumia miaka sita katika vita za
Dingiswayo akawa hodari sana na kujifunza uongozi alioboresha
baadaye.
Baada
ya kifo cha babake Shaka alirudi kwa Wazulu kwa msaada wa Dingiswayo
akachukua uongozi mnamo mwaka 1812. Baada ya kuwa kiongozi akalipiza
kisasi maadui wa utoto wake akiwaua kwa njia mbalimbali.
Shaka
aliendelea kukubali ubwana wa Mthethwa na Dingiswayo hadi akauwawa
vitani na kabila la Ndwandwe
mwaka 1817. Lakini pamoja na hayo alipigana vita na makabila madogo
jirani. Mbinu yake ilikuwa kuwashambulia waliompinga au kuwa hatari
kwake; wanawake na watoto waliingizwa katika ukoo wake, pamoja na
wanajeshi wa kiadui wasiouawa lakini waliokubali kumfuata baada ya
kushindwa. Kwa njia hiyo ukoo mdogo wa Wazulu uliendelea kukua.
Katika
miaka iliyofuata Shaka aliendelea kushambulia vikundi vya jirani na
kuwaingiza katika utawala wake. Makabila mengine walimfuata bila vita
wakikubali uongozi wake na kuingiza vijana wao katika impi au vikosi
vya kijeshi vya Shaka. Alituma viongozi au majenerali wake pamoja na
impi pande mbalimbali hadi Msumbiji
au pia Zimbabwe. Vikundi kama Ndebele huko Zimbabwe
au hata Wangoni
katika Tanzania
ni matokeo ya matembezi ya impi za kizulu zilizoenda mbali na
kupoteza mawasiliano na nyumbani.
Vita
hizi zilisababisha makabila mengine kukimbia na kuhamahama
wakishambulia majirani zao hivyo kupanusha eneo la vita katika nchi
mbali na Wazulu wenyewe. Kipindi hiki kinakumbukwa kwa majina kama
"mfecane" (Kizulu)
au "difaqane" (Kisotho)
kuwa miaka 30 ya vita na kifo.
Pamoja
na hayo makabila mengine kama Wasotho,
Waswazi,
Wandebele
au Wagaza
walioshambuliwa walijifunza mbinu za kijeshi wakifaulu kujitetea na
kuanzisha mataifa makubwa yakiunganisha wenyewe koo na makabila
madogo zaidi.
Utawala
wa Shaka ulikuwa na tabia za kinyama zilizosababisha chuki nyingi
dhidi yake. Baada ya kifo cha mamake Nandi alikuwa na hasira kiasi
cha kuuwa watu 7000 kati ya wanajeshi wake kwa kosa la kutoonyesha
huzuni ya kutosha na kuamuru kipindi cha kufunga miezi mitatu.
Aliamuru mashamba yasilimwe kwa mwaka mmoja na kila mwanamke
aliyeonekana kuwa na mimba katika kipindi hiki aliuawa pamoja na
mumewe. Wataalamu wengine huona ya kwamba wakati ule Shaka alionekana
kuwa na kichaa. Maadui walifanya mipango dhidi yake mwishowe aliuawa
na ndugu zake. Mwaka 1828 impi nyingi zilikuwa mbali vitani ikuli
ikawa bila ulinzi wa kutosha. Kaka zake Dingane na Mhlangana walimwua
na kutupa maiti shimoni.
Dingane
alimfuata Shaka akaua vingozi wengi waliokuwa waaminifu kwa Shaka.
Alilazimisha
watu wake kuacha vyandalua na viatu na kutembea pekupeku. Hii
iliongeza kasi ya impi zake na uwezo wao wa kushambulia haraka.
Inasemekana ya kwamba Shaka aliuwa wote waliolalamika walipoamriwa
kuacha viatu vyao.
No comments:
Post a Comment