Pages

Tuesday, 21 February 2012

Robert Mugabe


Robert Gabriel Mugabe amekuwa kiongozi wa Zimbabwe tangu 1980. Yeye ni mwenyekiti wa chama tawala cha ZANU. 1980 alikuwa waziri mkuu na 1987 Rais wa Zimbabwe. Kabla ya wakati ule aliongoza upinzani wa ZANU dhidi ya serikali ya walowezi Waingereza nchini waliofuata siasa ya ubaguzi wa rangi.
Mugabe alirudiwa katika uchaguzi mbalimbali. Tangu mwaka 2000 uchaguzi hizi zimekuwa mashakani kutokana na matishio na matumizi ya mabavu dhidi ya wapinzani. Utawala wa Mugabe umeitwa wa kidikteta tangu mwaka 2002. Kutokana na mashtaka dhidi ya serikali ya Mugabe ya kudharau haki za binadamu, nchi ya Zimbabwe ilisimamishwa ndani ya Jumuiya ya Madola. Mugabe pamoja na mawaziri wake na viongozi wa chama chake hawaruhusiwi kusafiri kwenda nchi za Umoja wa Ulaya na Marekani.
Mwanzoni mwa utawala wake Mugabe alisifiwa kujenga uchumi na sera ya elimu nchini. Zimbabwe ilikuwa nchi iliyouza vyakula vingi nje. Tangu mwanzo wa milenia mpya pamoja na mashtaki ya udikteta hali ya uchumi ulirudi nyuma. Takriban milioni mbili ya raia wa Zimbabwe wameondoka nchini wakikaa kama wakimbizi Afrika Kusini.


Baada tu ya kushika madaraka, Mugabe aliamua kuimarisha jeshi lake la kumlinda (liitwalo Gukurahundi) ambalo lilijengwa na watu kutoka kabila lake la wa-Shona. Nchi hiyo ilikuwa tayari imegawanyika kikabila hata katika uchaguzi wa kwanza wa 1980, washona wote walimchagua Mugabe na Wa-Ndebele na wabunge kutoka chama cha ZANU. Wakati wandebele walichagua viongozi kutoka chama cha ZAPU kilichoongozwa na Joshua Nkomo.
Mara baada ya uchaguzi tu mwezi Novemba 1980 Mugabe alianza kampeni ya kuua kwa wingi watu wa kabila la wa-Ndebele ambao mji wao mkubwa unaitwa Bulawayo. Ingawa mauaji hayo hayakufikia kiwango cha yale ya Rwanda na Burundi, waliuawa wanawake, wanaume, watoto na hata vichanga vilivyokuwa matumboni. Mwaka 1981 pia Mugabe aliendelea kuua wandebele tukio ambalo halikutangazwa sana na vyombo vya habari. Kuanzia enzi hizo hadi leo raisi Mugabe amejaribu kushinda kila uchaguzi unaokuja nchini huko kwa kutumia nguvu za kikabila na mabavu.
Alizaliwa Februari 21,1924 katika Zvimba Wilaya ya kaskazini magharibi ya Salisbury katika kusini mwa Rhodesia kwa baba wa Malawi Gabriel Matibili na mama kutoka kwa kabila la Shona wote wakatoliki. Yeye ni mtoto wa tatu kwa watotot sita. Alikuwa na na ndugu wawili wakubwa, na mmoja wao, Micheal, alikuwa maarufu sana katika Kijijini. Ndugu wote wawili waliaga dunia alipokuwa mchanga na kumwacha na mdogo wake.Babake ambaye alikuwa seremala aliiacha familia yake mwaka 1934 baada ya kifo cha Micheal alipokuwa akitafuta kazi huko Bulawayo.


Mugabe alikuzwa katika mazingira ya kikatoliki na kusomea vyuo vya kikatoliki kama Marist Brothers na Jesuit. Kulingana na kakake Mugabe alikuwa mpole na rafiki wake mkubwa alikuwa vitabu.
Alihitimu kama mwalimu lakini aliondoka kwenda kusoma katika Fort Hare nchini Afrika Kusini alipokuwa huko alikutana na Julius Nyerere, Herbert Chitempo na Keneth Kaunda. Kisha alienda kusoma Salisbury 1953, Gwelo 1954, na Tanzania 1955-1957. Apo awali alifuzu na Shahada ya Sanaa kutoka chuo kikuu cha Fort Hare mwaka 1951. Mugabe hatimaye alipata digri zaidi ya sita akiwa akisafiri ikiwa ni pamoja na Shahada ya Utawala na shahada ya Elimu kutoka chuo kikuu cha Afrika Kusini na shahada ya Sayansi, shahada ya sheria na zingine nyingi tu zote kutoka chuo kikuu cha London. Digri ya sheria alipata alipokuwa gerezani nayo shahada ya uzamili ya sayansi ya chuma alipata akiwa waziri mkuu.


Baada ya kufuzu, Mugabe alifunza katika Chuo cha Mafunzo cha Chalimbana kilichoko Zambia toka 1955-1958, baada ya hapo amefundisha katika Apowa shule ya Sekondari katika Takoradi,katika mkoa wa magharibi mwa Ghana huko ndiko alikutana na Sally Hayfron ambaye walifunga ndoa mwezi wa Aprili 1961
Mugabe alirudi Kusini mwa Rhodesia na kujiunga na National Democratic Party{NDP} mwaka 1960 wakati wa utawala wa waziri mkuu Ian Smith. Mwaka 1980 Machi 4 Mugabe alishinda kura na kuwa waziri mkuu licha ya kutokana vitisho kutoka pande zote, kutoaminiana kutoka kwa vikosi vya usalama na kupata ripoti ya masanduku ya kura kupatikana kwenye barabara.
Mwaka 1987, nafasi ya Waziri mkuu ilifutiliwa mbalina Mugabe na kuwa Rais mtendaji wa Zimbabwe na kupata nguvu zaidi. Alichaguliwa tena mwaka 1990 na 1996 na mwaka 2002 huku kukiwa na madai ya kuenea kwa wizi wa kura na vitisho
Katika kiaka ya 1980 sera ya Mugabe ya Ujamaa ilionekana kukuza nchi hiyo, mwaka 1980 na 1981 uchumi wa Zimbabwe ulikuwa kwa asilimia 10.65 na 12.5% kutoka asilimia 2.7%. Kutokana na ripoti hiyo kwa mujibu wa Benki ya Dunia 1995 baada ya uhuru Zimbabwe ilitoa kipaumbele katika uwezekaji wa rasilimali na msaada kwa ajili ya kilimo cha wakulima wadogo wadogo.
Hata hivyo jamaa huyu ameshtumiwa kwa na mtazamo wa ubaguzi wa rangi kwa wazungu, pia jamaa huyu amekuwa suluhu katika upinzani wake kwa haki za ushoga.
Uchaguzi ujao ulikuwa ufanyike 2013, lakini umepelekwa mbele hadi 2012 kwa madai kwamba umri wake ni mkubwa licha ya hayo chama chake cha ZANU-PF kimesema kwamba bado atawania urais.
Kwa sasa yeye ndiye rais aliyehudumu kwa mda mrefu barani afrika, mwaka wa 2005 alipelekwa hospitalini kwa kuwa na mshtuko wa moyo jambo ambalo lilipeleka uvumi kwamba amefariki.


Mke wake wa kwanza Sally Hayfron aliaga dunia 1992 kwa shida ya figo mtoto wao wa pekee kijana Micheal Nhamodzenyika Mugabe aliyezaliwa septemba 27 1963 pia aliaga Desemba 26 1966 kutokana kutokana na malaria ya ubongo. Sally ambaye alikuwa pia mshauri mkuu wake wa kisiasa inasemekana kwamba baada ya kifo chake Mugabe alianza kuiongoza Zimbabwe vibaya.
Agosti 17 1996 alimuowa aliyekuwa karani wake Grace Marufu ambaye ni mchanga wake kwa miaka41 na wana watoto wawili naye, yeye tayari alikuwa na mimba ya Mugabe akiwa bado ana mke wake wa kwanza Sally na wakati huo Grace alikuwa kwenye ndoa yake na Stanley Goreraza, sasa mwanadiplomasia nchini Chini.Sasa wana watoto watatu naye.
USICHOJUA KUMHUSU
Anapoadhimisha miaka 88 leo anajulikana sana kwa kutumia pesa za watozwa ushuru kuadhimisha sherehe hizi.
Ndiye rais aliyesoma na ana shahada zaidi ya 16 ulimwenguni
Alifungwa jela miaka 10 kuanzia 1964 kwa kupinga utawala wa wakoloni.
Ndiye rais aliyeongoza kwa mda mrefu barani afrika.

No comments:

Post a Comment