George Tawlon Manneh Oppong Ousman Weah Ni mwanakandanda mashuhuri duniani na mwanasiasa aliyegombea urais wa Liberia mwaka 2005. Weah alizaliwa Oktoba 1, 1966 katika jiji la Monrovia. Alikulia kitongoji Clara. Kabla ya kujiunga na soka ya kulipwa Weah alikuwa akifanya kazi katika Shirika la Mawasiliano la Liberia kama fundi wa simu.
Aliwania urais bila mafanikio katika uchaguzi wa mwaka 2005, na kupoteza kwa Ellen Johnson Sirleaf katika duru ya pili ya upigaji kura. Katika uchaguzi wa 2011 alikuwepo kwenye kinyang'anyiro hicho kama mgombea mwenza wa Winston Tubman.
Kielimu, Weah ana Shahada ya Kwanza ya Michezo toka Chuo Kikuu cha Parkwood, London, Uingereza. Mwaka 1999 alipata shahada ya Udakitari ya Heshima toka Chuo Kikuu cha A.M.E Zion nchini Liberia.

Licha ya mafanikio haya yote kwa vilabu hivi hakuweza kuleta utaalamu wake kwenye timu ya taifa ya Liberia licha ya kuwasaidia Kifedha na hata kuwa kocha wao, licha ya kutambulika kwenye vilabu na mchezaji aliyeimarika wa Afrika hajawahi kucheza kwenye Kombe la Dunia.
Mwaka 1995 Weah alipewa tuzo na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) na kuwa Mwanasoka Bora Duniani. Yeye ni mwanasoka wa pekee toka Afrika aliyewahi kupewa tuzo hiyo. Mwaka huo huo alichaguliwa kama Mwanasoka Bora Ulaya.
Alikuwa mwanasoka bora Afrika mwaka wa1989 akichezea klabu ya AC Monaco na 1995 akichezea klabu ya AC Milan
Ndiye mwanasoka wa pekee wa Afrika aliyechaguliwa mchezaji bora wa karne na kumweka miongoni mwa wachezaji wachache waliowahi kushinda tuzo hili kama vile Pele wa Brazil na Johan Crujiff.
Mwaka wa 1996 alipigwa marufuku kutocheza mechi sita kwa kumjeruhi mwenzake wa timu pinzani pua kwa madai ya ubaguzi wa rangi.
Weah amekuwa akitoa misaada kusaidia wananchi wa Liberia. Mwaka 2004 alipewa tuzo ya Arthur Ashe kwa juhudi zake za kusaidia kujenga nchi yake. Alitajwa pia kuwa balozi wa UNICEF
Ana watoto wanne George weah jr, Tita, Timothy na mmoja adopted kutoka Lebanon Samer Hodroj.
Alibadilika toka Ukristu hadi Uislamu kabla ya kubadilika alisema kwamba waislamu na wakristu ni kitu kimoja.
No comments:
Post a Comment