
Abedi
Pele alikuwa mmoja wa waanzilishi wa mpira wa miguu ya Afrika katika
Ulaya. Ni mmoja wa wachezaji wa kwanza wa Afrika kuchezea soka kwenye
vilabu vya Ulaya kama vile Uswisi, Ujerumani na pia Italia, ni
maarufu huko Ufaransa alikochezea sana haswa kwenye kilabu cha
Marseille katika Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati wa miaka ya 1990.
Aliondika
Ghana kwenda Qatar baada ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka wa 1982.
Baada ya miaka michache alirudi Ghana na akakosa kusajiliwa na klabu
ya Kotoko kisha baadaye alijiunga na kilabu ya AS Dragons FC de
l'Oueme ya Benin. Alirudi Ghana na kujiunga na timu ya Real Tamale
United kwa Muhula mmoja. Alianza soka yake ya kimaaifa huko Ufaransa
na klabu ya Chamois Niort, Montpellier na Lille kisha akajiunga na
Olympique Marseille, baadaye alihamia Lyon.
Alikuwa
nahodha wa timu ya soka ya Ghana kwa miaka 6 tangu 1992 – 1998 na
alikuwa mwafrika wa kwanza kumaliza katika nafasi ya kwanza ya
mchezaji bora wa FIFA orodha ya mwaka 1991 na 1992. Ni mchezaji bora
wa Afrika ameshinda tuzo kadha wa kadha zikiwemo Shirikisho la soka
Afrika, Tuzo la mchezaji bora la BBC, alituzwa pia kuwa mchezaji bora
katika kombe la mataifa la Afrika 1992 na aalikuwa man of the match
katika fainali ya mechi ya kihistoria ya Ligi ya Mabingwa ya Ulaya
kati ya Marseille na Milan mwaka 1993.
Ana
mtoto ambaye pia alifuata nyayo zake na pia anachezea timu ya
nyumbani ya Ghana na alikuwa miongoni mwa wachezaji waliokuwa kwenye
Kombe la Afrika lililokamilika hapo jana.
Abedi
Pele Ayew alizindua mnara wake huko Equitorial Guinea wakati wa
michezo hiyo kwa kuwa mchezaji bora kuwahi tika barani Afrika.
No comments:
Post a Comment