Alizaliwa
Januari 5 1938, Kamirithu karibu na Limuru katika Kaunti ya Kiambu,
alibatizwa James Ngugi.Ni mwandishi wa Kenya hapo zamani aliandika
kwa Kiingereza lakini sasa anaandika kwa lugha ya Gikuyu. Kazi yake
ni pamoja na Riwaya, Michezo, Hadithi fupi na Insha, pia yeye ni
mwanzilishili na mhariri wa jarida la ligha ya Gikuyu, Mutiiri.
Alipata
Elimu katika shule za Kamandura, Manguu na Kinyogori na kisha
kuelekea katika shule ya Upili ya Alliance High School zote toka
Kenya, baada ya hapo alizidisha masomo yake kwenye Chuo Kikuu cha
Makerere huko Uganda na Chuo Kikuu cha Leeds huko Uiingereza.
Ngugi
ni mpokeaji wa Udakitari za Heshima saba kutoka vyuo vikuu tofauti
tofauti.
Riwaya
yake ya kwanza Weep Not Child kilichochapishwa 1964, alikiandika
akiwa Katika Chuo Kikuu cha Leeds huko Uiingereza, na kumfanya kuwa
mwafrika wa kwanza kutoka Afrika Mashiriki kuchapisha katika Lugha ya
Kiingereza.
Mwaka
wa 1967 baada ya kuchapisha riwaya yake Agrain of Wheat aliwacha
kuandika kwa Kiingereza akaacha pia Ukisto na kumfanya kubadilisha
Jina lake James Ngungi hadi Ngugi wa Thiongo na akaanza kuandika
katika asili yake ya Gikuyu na Kiswahili. Mwaka wa 1977alichapisha
mchezo Ngaahika Ndeenda yani ( I will Marry When I want) ambacho
kilimkasirisha makamu wa Rais wakiti ule Daniel Arap Moi alipoamuru
kufungwa. Ali[pokuwa kizuizini katika gereza la Kamiti Maximum
aliandika riwaya ya kwanza ya Kisasa katika Gikuyu Caitaani Mutharaba
yaani (Devil on the Cross) kwenye karatasi gushi.
Baada
ya kutoka kwake hakurejeshewa kazi yake kama profesa katika Chuo
Kikuu cha Nairobi, na familia yake ilikuwa inasumbuliwa kutokana na
maadishi yake kuhusu kukosekana kwa haki na serikali ya kidikteta
hata hivyo kulazimika kuishi uhamishoni. Alirudi baada ya miaka 22
wakati Moi alitoka Ofisini.
Tarehe
8 Agosti 2004 Ngugi alirejea Kenya kama ziara ya kuzuru Afrika
Mashariki.Agosti 11, majambazi waliingia nyumbani kwake na
kudhulumiwa pamoja na mke wake, na kuiba fedha na kompyuta jambo
ambalo lilimfanya arudi Marekani hadi sasa.
Amechapisha
riwaya, michezo,na hadithi fupi zaidi ya 30.
No comments:
Post a Comment