
Basi kanisa hilo lenye waumini zaidi ya elfu moja kwa miezi mitatu walichangisha shilingi elfu mia mbili ambazo hazikutosha kufanya shughuli hiyo. Jumapili iliyofuata, waumini walichangisha elfu hamsini nazo pesa zote kwa jumla zikawa laki mbili hamsini elfu.
Ghafla kwa bahati mbaya,kundi la majambazi sita waliojihami kwa bunduki waliingia kanisani na kuamuru kila mtu alale chini huku wakichukua zile pesa ambazo zilikuwa zimechangishwa. Wakaamuru kila mtu atoe alichokuwa nacho. Ajabu ni kwamba majambazi hao walikusanya shilingi milioni kumi pamoja na zile laki mbili hamsini elfu.
Amini usiamini majambazi wale walimkabidhi mhubiri yule pesa zote walizokusanya kwajili ya kurekebisha kanisa kisha wakatoweka.
Sasa hebu tafakali kati ya mhubiri,waumini na majambazi,nani aliye na makosa? Milioni 3.5 ziliwashinda waumini kuchangisha kwa miezi mitatu lakini milioni kumi zapatikana kwa masaa mawili.
No comments:
Post a Comment