Pages

Friday, 10 February 2012

MBWEMBWE

                                                                                     SIKU MBAYA HUANZA ASUBUHI
Kulikuwa na jamaa huku Afrika Kusini alikuwa ameketi ndani ya bar huku akitazama kinywaji chake kwa nusu saa.
Kwa bahati katokea dereva mmoja wa lori ambaye amekuwa akiwasumbua watu sana kwenya bar hio. Moja kwa moja akafululiza na kunywa kinywaji chake jamaa yule na kuhakikisha kuwa amelimaliza. Amini usiamini, jamaa yule mwanaume mzima alianza kulia kama mtoto mchanga.
Dereva yule alishangaa sana na kumwomba jamaa yule msamaha na kusema kuwa alikuwa tu afanya mzaha na atamnunulia kinwaji kingine kulipiza alichokuwa amekunywa, lakini jamaa yule alimwambia dereva kuwa si kinywaji alichokuwa analilia bali ni masaibu yaliyomkabili  toka asubuhi. Alisema,"Leo asubuhi nilichelewa kwenda kazini naye bosi wangu akanifurusha kazini.
"Kutoka kazini sikuegesha gari langu vyema barabarani nalo likaibwa na wezi. Kupiga ripoti kwa polisi wao wamedinda kunipa usaidizi kwa sababu wanahitaji stakabadhi la gari hilo ambazo pia zilipotea. Nikachukua taxi kuelekea nyumbani. Kwa bahati mbaya nikasahau mkoba wangu wa pesa na sithakabadhi zangu zote za benki kwenye taxi. Kumuuliza dereva wa taxi akapinga kuwa hajaziona.
"Nilipofika nyumbani, nusura nizirai.Nilimpata mke wangu chumbani na shambaboy wangu. Ndiposa nikaja hapa ili kufikisha mwisho matatizo ambayo yananikumba. Nilipokuwa na tafakari kuhusu hayo, wewe ukaja na kunywa sumu yangu.

No comments:

Post a Comment