Pages

Thursday, 23 February 2012

Wole Soyinka


Akinwande Oluwole au "Wole" Soyinka ni mwandishi Mnageria .Wengi wanamwona kama mwandishi bora wa michezo ya kuigiziwa Afrika. Ni mwandishi na mtungi wa Mashairi na pia michezo ya kuigiza.
Alizaliwa tar. Julai 13, 1934 kwa wazazi Wayoruba huko Abeokuta, Nigeria. Alisoma shule ya msingi kwao Abeokuta halafu shule ya sekondari ya Ibadan,kisha akasomea fasihi kwenye Chuohicho cha Ibadan (1952-1954) na Leeds (Uingereza) 1954-1957.
Alifundisha fasihi kwenye vyuo vikuu vya Lagos, Ibadan, na Ife.
Soyinka aligongana mara nyingi na serikali za kidikteta za nchi yake akipinga pia udikteta katika nchi mbalimbali kama vile utawala wa Mugabe huko Zimbabwe.
Hasa wakati wa udikteta wa jenerali Sami Abacha (1993-1998) Soyinka alijikuta hatarini. Akaondoka Nigeria akaishi nje alipopata kuwa profesa wa fasihi kwenye Chuo Kikuu cha Emory (Atlanta - Marekani).
Februari 6 2012 Soyinka alisema kwamba yuko miongoni mwa watu maarufu na mashuhuri wanaolengwa kuuwawa na kundi la Boko Haram.
Baada ya mwisho wa utawala wa kijeshi mwaka 1999 Soyinka alikubali nafasi kwenye chuo kikuu cha Ife kwa masharti ya kwamba mwanajeshi mstaafu hatakuwa kamwe chansela wa chuo kikuu kile.
Mwaka 2005 Soyinka akawa profesa kwenye chuo kikuu cha Nevada, Marekani.
Wole Soyinka amemwoa mke wake Laide wana watoto wanne. Aliwahi kuwa na watoto wawili kabla ya kuoa.
JE WAJUA
Ni Mshindi wa kwanza Mwafrika kupewa Tuzo ya Nobel ya fasihi (mwaka wa 1986)
Mwaka 1994 aliteuliwa kuwa balozi wa nia njema kwa{UNESCO}Umoja wa Mataifa la Elimu,Sayansi,na Utamaduni kwa ajili ya kukuza Utamaduni wa Kiafrika, haki za binadamu, Uhuru wa Kujieleza, Vyombo vya habari na mawasiliano.
Ameandika zaidi ya michezo 20.

No comments:

Post a Comment