Steve Biko
Biko alikuwa kiongozi wa wanafunzi,
baadae akaanzisha vuguvugu la Black
Consciouness Movement
(Harakati za kujitambua kwa watu weusi). Vuguvugu hili lilipata nguvu
sana na kuenea katika miji mingi yenye idadi kubwa ya watu weusi.
Mauti yalimfikia baada ya kutiwa mbaroni
na kuteswa na maaskari wa serikali ya kibaguzi. Biko alijulikana kama
jabali la harakati dhidi ya ubaguzi wa rangi. Wakati yupo hai,
alikuwa akiandika sana masuala ya harakati za kujaribu kuwatia nguvu
watu weusi na aliweza kuwa maarufu kwa wito wake wa kusema kwamba
"black is beautiful" akimaanisha kwamba "mtu mweusi ni
mzuri." Alielezea maana ya msemo huu ni: "mtu, ni sawa kama
ulivyo mtu, lakini anza kujiangalia mwenye ukiwa kama binaadamu.
Stephen Bantu Biko alizaliwa mjini
King
Williams Town, ndani ya
jimbo la Eastern
Cape nchini Afrika
Kusini 18
Desemba, 1946
. Biko alikuwa mwananfunzi wa Chuo Kikuu cha Natal Medical School.
Hapo awali Biko alikuwa akijishughulisha
na masuala ya kutafuta "Umoja wa Umma wa Wanafunzi Afrika
Kusini" (National Union of South African Students), baada ya
kuweza kuwaadikisha watu weusi, wahindi, na watu weupe pia, kwamba
wakiwa kama wanfunzi wanahitaji jumuiya itakayokuwa inawaangalia
wanafunzi.
Mnamo tarehe 18
Agosti ya mwaka
1977,
Biko alitiwa nguvuni na mapolisi kwa kosa la ugaidi kifungu namba 83
cha 1967 cha nchini Afrika
Kusini. Steve Biko alipatwa
na majeraha makubwa kichwani baada ya kukamatwa na mapolisi na kuanza
kumpa kipigo kisichokuwa na kifani. Wakamfunga na minyororo katika
kidirisha cha machuma kwa muda wa siku nzima.
Mnamo tarehe 11
Septemba ya mwaka 1977
polisi walimfunga Biko nyuma ya gari aina ya Land Rover, akiwa uchi,
na kuanza kuendesha gari kwa umbali wa km 1,200. Alikufa mda mchache
baada ya kujiri katika jela ya Pretoria, mnamo tarehe 12
Septemba ya mwaka 1977.
Polisi wakatangaza kwamba kifo chake
kilisababishwa na njaa kali. Biko alikutwa na majeraha makubwa
kichwani kwake, ambapo mengi yalionekana kama ushaidi mkali kuwa
jamaa alifanyiwa kitendo cha kiukatili na hao waliomkamata. Kisha
mwandishi wa habari na kiongozi wa kisiasa wa sasa, Bi. Helen
Zille, alifuchua ukweli
uliojificha juu ya kifo cha Biko.
Mwaka uliofuata tarehe 2
Februari 1978,
jaji mkuu wa Eastern Cape alitoa tamko la kusema kwamba hatotoa
hukumu kwa askari yoyote yule aliyehusika kwa kukamatwa na kutiwa
kuizini kwa Biko. Wakati kesi inaendelea, ilitangazwa kuwa majeraha
yote yaliyokuwa kichwani kwa Biko, ilikuwa ni kutaka kujaribu kujiua
mwenyewe, na haikumaanisha kuwa Biko alipigwa.
Baada ya hujma na mazungushano ya huku na
kule ikabidi iundwe "Tume ya ukweli na upatanishi" (Kwa
Kiing:Truth and Reconciliation Commission), ambayo iliundwa kwa
kufuata taratibu ndogo tu za kibaguzi, ilitaarifiwa mnamo 1997 kuwa
moja kati ya maaskari watano wa kikosi cha usalama nchiini Afrika
Kusini, alikubali kuwa yeye alichangia kuuawa kwa Biko, askari huyo
ambaye alikuja kufa katika machafuko ya Soweto zidi ya ubaguzi wa
rangi nchini Afrika ya Kusini.
Mnamo tarehe 7
Oktoba mwaka 2003
Wizara ya Sheria ya Afrika Kusini ilitangaza rasmi kwamba maaskari
watano walioshtakiwa kwa kosa la mauwaji ya Biko, hawato hukumiwa
kwasababu hakuna ushaidi wa kotosha, ukweli ni kwamba muda wa kutoa
hukumu pia nayo ushapita, hivyo hamna hukumu yoyote ile zidi ya
maaskari hao.
kazi nzuri
ReplyDelete